Utaratibu wa kupima Ukimwi bongo una maswali mengi kuliko majibu: Kuna haja ya kuboresha

Kwanza kabisa niseme! utaratibu Wa kupima ukimwi mbali na kuwepo maswali mazito lakini pia siyo rafiki hasa kwa wanaume!

  • Sijawahi kuelewa kwanini mtu akishapimwa, bado anatakiwa ku-comfirm tena na tena after three months anapimwa second round, halafu tena after three months third round!..Kwanini miezi yote tisa jaman?
  • miezi yote hiyo tisa yakusubili kurudia kupima kiuhalisia mapenzi huyo mtu anakuwa anafanya na nani?
  • Kama kupima mara moja siyo sahihi, Je; Zile damu za kuchangia watu huwa zinapimwa Mara ngapi nakupelekewa wagonjwa pasipokusubili miezi tisa, Je damu hizo huwa siyo salama?
Naomba mwenye majibu tafadhali; Maana naona huo utaratibu siyo rafiki kwa wanaume kabisa ndiyo maana tunakimbiaga majibu
Mkuu mada zako huwa kama za masihara lakini kama zina hoja kubwa sana!
 
mkuu ndio hari ilivyo hivyo kweli au unatania tu.
Nitanie mkuu,wewe ukitaka kuamini siku utakayoumwa hata maralia nenda mwananyamala hospital au palestina sinza,au hospitali yoyote ya serikali,omba kumuona dokta.natumaini utaleta mrejesho hapa
 
Issue ni kwamba ukienda hospital , ukitoa damu tu lazima HIV ipimwe , inapimwa ili madaktari wapunguze ulakini kwenye kukupa huduma ,
 
Kwanza kabisa niseme! utaratibu Wa kupima ukimwi mbali na kuwepo maswali mazito lakini pia siyo rafiki hasa kwa wanaume!

  • Sijawahi kuelewa kwanini mtu akishapimwa, bado anatakiwa ku-comfirm tena na tena after three months anapimwa second round, halafu tena after three months third round!..Kwanini miezi yote tisa jaman?
  • miezi yote hiyo tisa yakusubili kurudia kupima kiuhalisia mapenzi huyo mtu anakuwa anafanya na nani?
  • Kama kupima mara moja siyo sahihi, Je; Zile damu za kuchangia watu huwa zinapimwa Mara ngapi nakupelekewa wagonjwa pasipokusubili miezi tisa, Je damu hizo huwa siyo salama?
Naomba mwenye majibu tafadhali; Maana naona huo utaratibu siyo rafiki kwa wanaume kabisa ndiyo maana tunakimbiaga majibu
Hoja zako zote zina maelezo ya kitaalam, kama hutajali tembelea kituo chochote cha tiba haswa kinachotoa huduma kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI watakupa majibu unayohitaji
 
mambo yote ya Jf huwa niyakitaalam !! tunajuzana tu,
 
Nikipita bira kucoment ntakua sijaitendea haki taaluma yangu.

Kwanza mleta mada pole kwa experience yako Kama umekutana nayo bayana . ...mbali na hivyo nikuombe uwe mpole na ukubari kujifunza na kuheshimu taaluma za watu.

Wataalamu wa afya ni watu makini na mara nyingi utenda kazi zao kwa weredi mkubwa kwa kuzingatia evidence based medicine.

Nikijibu maswali yako kwa ufupi ni kuwa , zoezi zima la upimaji Lina miongozo yake.

Ukweli ni kuwa kwa current guideline ya upimaji wa HIV hauitaji kurudia zaidi ya Mara mbili na kipimo cha Kwanza na cha pili hutofautiana kwa week 4 tu, yaaani mwezi mmoja.

Pili ni vizuri kutambua kuwa Kuna kitu kitaalum tunakiita "window period" hiki ni kipindi ambacho toka umepata maambukizo hadi kipindi tunapoweza kugundua Kama umeambukizwa hasa kwa kutumia detection of antibodies against HIV Kutokana na vipimo tunavyovitumia kupima HIV yaaani rapid HIV test (SD Bioline /Unigold). Kwa HIV huwa ni muda wa 2-4wks ndipo mwili utengeneza antibodies dhidi ya HIV , na vipimo tuvitumiavyo ni vile vinavyotest uwepo wa antibodies hizi mwilini .

So unaweza kuwa negative siku ya kwanza kupima ila ukawa positive katika kipimo cha marudio. Ili kuhepuka tatizo hili ndiposa kipimo Cha marudio huwa ni mhimu kufanyika. Hii ni kwa faida ya mgonjwa na jamii kwa ujumla ili kupunguza chance ya kum -lable mtu Yuko negative kumbe Yuko positive, na subsquent consequences unaweza kuzi predict hasa kwa vijana wasio makini Kama mleta mada.

Note: wataalamu wa upimaji uhakikisha wanakupa maelezo ya kuzingatia ndani ya kipindi hicho Cha matazamio ya kipimo Cha pili.

Hata hivyo Kuna kipimo kingine cha PCR ambacho kinaweza kudetect kuwa una HIV ndani ya siku 3 toka umeambukizwa ila kwa bahati mbaya hatuvitumii routinely na havipo kila kituo Cha Afya.

Mwisho, usije ukapotosha umma kuwa damu inayochangiwa na wagonjwa ndo hiyo hiyo huenda kuongezewa mgonjwa direct; La hasha! Damu hiyo hupita katika mchakato wa vipimo mbalimbali Kama HIV na Hepatitis na cross matching ili kujua compatibility.

Mambo haya ni yakitaalamu hivyo mara nyingi hata ukimueleza mgonjwa au ndugu huwa si rahisi kuyaelewa ndiposa layman language utumika ili kutoa ujumbe.

Niitimishe kwa kusema

Ziko faida nyingi kwa kujua hali yako ya maambukizi.

Shime vijana jitokezeni kujua hali zenu.

Kuweni wadadisi ila msipotoshe jamii

Ukimwi ni halisi endelea kuchukua hatua.

Kind regards
PM
 
Mkuu kwa maono yako na kwa kua uko kitengo kabisa vipi spidi ya hili tatizo inapungua au ndio inaongezeka?
 
Kumbe ndobtumefika hapo.
Siku hizi kupima ni lazima tena siyo hiyari kama zamani,ukienda hospitali ya serikali kupima hata maralia lazima wakupime ukimwi,wakikuta signal zinasoma,unabebwa msobe msobe hadi kwenye ushauri nasaha,yaani kibabe tu!sasa wewe kaa hivyo hivyo
 
Mkuu kwa maono yako na kwa kua uko kitengo kabisa vipi spidi ya hili tatizo inapungua au ndio inaongezeka?
Matumaini yapo mkuu
Rate ya maambukizi na vifo vitokanavyo na Ukimwi vinaendelea kupungua ila tatizo bado ni kubwa na jitihada za kukabiliana na janga hili zinahitajika zaidi..
 
Siku hizi kupima ni lazima tena siyo hiyari kama zamani,ukienda hospitali ya serikali kupima hata maralia lazima wakupime ukimwi,wakikuta signal zinasoma,unabebwa msobe msobe hadi kwenye ushauri nasaha,yaani kibabe tu!sasa wewe kaa hivyo hivyo
msobemsobe mhh!!! kweli hii shoo ya kibabe
 
Msaada hapo.picha ya kwanza ni siku ya kwanza.picha ta pili ni siku ya pili baada ya masaa 26 kupita.kipimo ni kilekile sema sikukitupa baada ya kupima.tatizo ni kwa hiyo picha ya pili ambapo kuna vimistari kwa mbali sana vinaonekaba kwa hizo line za 1 na 2.maelezo kwanini kuna mabadiliko
IMG20190826220058.jpg
IMG20190828002250.jpg
 
Msaada hapo.picha ya kwanza ni siku ya kwanza.picha ta pili ni siku ya pili baada ya masaa 26 kupita.kipimo ni kilekile sema sikukitupa baada ya kupima.tatizo ni kwa hiyo picha ya pili ambapo kuna vimistari kwa mbali sana vinaonekaba kwa hizo line za 1 na 2.maelezo kwanini kuna mabadilikoView attachment 1191642View attachment 1191643
Si hujakitupa? Unasubiri mistari iwe mingi ukitupe sio? Unachokitafuta utakipata.

Hichi kipimo ni instant. Unadondosha damu na droplets zile unapokea majibu hapo hapo. Hiyo ya kukilaza kama kiporo cha ubwabwa unachokitafuta unakijua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom