Utaratibu wa kumpa mama ukutunzie vyeti umekaaje?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
Kuna jamaa yangu fulani ana 32yrs ameoa, kaajiriwa na amepanga. Sasa wakati wa ukaguzi wa watumishi hewa akafunga safari ya 100km kwenda kwao kuchukua vyeti. Ananiambia akishahakikiwa atavirudisha. Anasema kwao ni salama zaidi. Ukiangalia makazi yake ni bora kuliko kwao.

Huu ni mfano tu ila nimekutana na watu kibao wamehifadhiwa vyetu na mama zao. Hivi ni kuchelewa kumature, irresponsibility au ni kitu gani?
 
Uko sahihi nadhani sio uoga pekee ipo sababu nyingine
Kwanza wengi inawahusu. Nashindwa kuelewa imekuaje mpaka sasa hata mimi baadhi ya vyeti vyangu anavyo mama yangu amenitunzia nyumbani kwake na najua vipo kwenye droo fulani.. Cha ajabu na yeye vyeti vyake kama vile vya shule au vya dini na yeye ametunziwa na mama yake (bibi yangu) hii desturi ipo familia nyingi
 
Hii nafikiri inatokana na trust aliyonayo mtu kwa kuamini kuwa vitakuwa salama lkn inaweza kwenda mbali zaidi ukianzia kwenye malezi ya utoto mtu amelelewa vp n
 
Kutokujiamini na uoga wa maisha.
Sio uoga kaka, wazazi wetu ni watunzaji sana, mimi nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ta sabini lakini cheti changu cha kuzaliwa na cha cliniki kipo kisafi mpaka leo utafikiri kina miaka kumi tu, kilikuwa kwa wazazi wangu nimekichukua mwaka jana tu, niko kwenye ndoa zaidi ya miaka 15 lakini chetu changu cha ndoa kiko kwa wazazi. Mwaka jana nikiwa kwa wazazi wakati napekua stoo nikakuta madaftari yangu ya math ya kidato cha pili about 20yrs ago, kwa wazazi wangu kuna nyaraka zina umri zaidi ya miaka 40. Kwa wazazi walio seto life sehemu moja, hawana kuhama hama, kitu kikiwekwa mahali utakikuta hapo for next 50 yrs, Sisi wandugu wa kuhamahama na leo uko mji huu kesho kule, unahamia mahali unakaa hotel mwaka mzima. kama unanyumba yako ziku unamwambia dada wa nyumbani afanye usafi unakuta kachoma docs za muhimu.
 
Sisi wa kupanga uswazi lazima vyeti vitunzwe mahala salama kama nyumbani nk, maake unawezi rudi toka kibaruani ukakuta gheto jeupe limesafishwa na panya road
 
Ukigundua mkeo ana kichaa cha kuvunja vitu pindi mtofautianapo, tambua kuwa ipo siku hasira yake itaaishia kwenye vyeti vyako hivyo kukaa navyo mwenyewe si salama peleka kwa mama.
 
Kuna jamaa yangu fulani ana 32yrs ameoa, kaajiriwa na amepanga. Sasa wakati wa ukaguzi wa watumishi hewa akafunga safari ya 100km kwenda kwao kuchukua vyeti. Ananiambia akishahakikiwa atavirudisha. Anasema kwao ni salama zaidi. Ukiangalia makazi yake ni bora kuliko kwao.

Huu ni mfano tu ila nimekutana na watu kibao wamehifadhiwa vyetu na mama zao. Hivi ni kuchelewa kumature, irresponsibility au ni kitu gani?
Kwa vile hata mimi nahifadhiwa baadhi ya vyeti na mama mpaka leo sina la kuchangia, isipokuwa kuhusu avatar yako tu. Hivi inamaanisha nini? mimi hata sijaielewa kabisa
 
Sio uoga kaka, wazazi wetu ni watunzaji sana, mimi nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ta sabini lakini cheti changu cha kuzaliwa na cha cliniki kipo kisafi mpaka leo utafikiri kina miaka kumi tu, kilikuwa kwa wazazi wangu nimekichukua mwaka jana tu, niko kwenye ndoa zaidi ya miaka 15 lakini chetu changu cha ndoa kiko kwa wazazi. Mwaka jana nikiwa kwa wazazi wakati napekua stoo nikakuta madaftari yangu ya math ya kidato cha pili about 20yrs ago, kwa wazazi wangu kuna nyaraka zina umri zaidi ya miaka 40. Kwa wazazi walio seto life sehemu moja, hawana kuhama hama, kitu kikiwekwa mahali utakikuta hapo for next 50 yrs, Sisi wandugu wa kuhamahama na leo uko mji huu kesho kule, unahamia mahali unakaa hotel mwaka mzima. kama unanyumba yako ziku unamwambia dada wa nyumbani afanye usafi unakuta kachoma docs za muhimu.[/QUOT
Ni kweli,pia kuhifadhi vitu mfano vyeti.Jaribu pia ku scan na kupitia kwa external hard disk drive,flash.Na waweza weka pahala mfano huko huko kwenu au pahala pa usalama zaidi.Kuwa na copies nyingi ya vyeti na nyaraka muhimu.Na si zihifadhiwe sehemu moja tu.Chagua sehemu mbili tofauti zenye usalama na hifadhi.Ajari mfano za moto huweza toke mara moja tu na zikaharibu kila kitu.Au hata kuibiwa...
 
Nafikiri vyeti vya shule, birth certificate wengi wanaacha nyumbani kwa wazazi maana huko ndio ikulu.
Kwa vijana kuhamahama ni kawaida mpaka hapo anapojenga nyumba yake vifaa muhimu huwa vinakaa kwa wazazi
 
Ni uoga wa maisha na kujidekeza tu.we baba zima la miaka 40 utashndwaje kutunza hayo makaratas yako mwenyewe?
 
Back
Top Bottom