charrote
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 1,673
- 3,641
Salaam wakuu,
Kwa masikitiko makubwa naomba nizungumzie huu utaratibu wa kulaza mabasi ya abiria nzega,sijajua shida ni nini wakati unatoka mikoa mingine kuja dar es salaam basi linafika siku hiyo hiyo lakini ajabu ukiwa unatoka dar kwenda mikoa hasa ya kanda ya ziwa basi linalala nzega na safar inaendelea kesho. Si vibaya kwa basi kulala stendi "MPYA" ya Nzega ila niseme tu mazingira ya hiyo stendi mpya ya Nzega sio rafiki kabisa,kwanza huduma za vyoo ni mbovu sana ,kuna matundu matatu tu ya vyoo na bafu moja kwa kila jinsia. Haitoshi vyoo ni vichafu sana yani wale wasimamizi wanajua kuchaji tu pesa ya huduma na sio kusafisha vyoo,hii ni hatari kwa afya zetu hasa sisi wanawake.
Kitu kingine ni abiria kulazimika kulala wamekaa kwenye siti za basi kwani hakuna nyumba za wageni maeneo ya karibu ,sasa hapo ukiamka kesho unakuwa kama zombie akili imezubaa kabisa,.
Cha mwisho usalama wa abiria stendi mpya ya Nzega ni mdogo mno ,kuna vibaka pale sijapata kuona ole wako utoke uende uwani unakuta washapiga sachi begi.
Ushauri wangu serikali ifanye juhudi za maksudi kuboresha stendi mpya ya Nzega,abiria tunapitia mateso makubwa.vyoo viongezwe,walau boma LA kuwasitiri "walala nje" liwepo,usalama wa wasafiri uimarishwe ili basi Watanzania waendelee kuongeza maksi katika utawala wa awamu hii ya hapa kazi tu.
Muwe na Jumapili njema