Utaratibu wa kulaza mabasi ya abiria Nzega uangaliwe upya

charrote

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,660
3,625
Salaam wakuu,
Kwa masikitiko makubwa naomba nizungumzie huu utaratibu wa kulaza mabasi ya abiria nzega,sijajua shida ni nini wakati unatoka mikoa mingine kuja dar es salaam basi linafika siku hiyo hiyo lakini ajabu ukiwa unatoka dar kwenda mikoa hasa ya kanda ya ziwa basi linalala nzega na safar inaendelea kesho. Si vibaya kwa basi kulala stendi "MPYA" ya Nzega ila niseme tu mazingira ya hiyo stendi mpya ya Nzega sio rafiki kabisa,kwanza huduma za vyoo ni mbovu sana ,kuna matundu matatu tu ya vyoo na bafu moja kwa kila jinsia. Haitoshi vyoo ni vichafu sana yani wale wasimamizi wanajua kuchaji tu pesa ya huduma na sio kusafisha vyoo,hii ni hatari kwa afya zetu hasa sisi wanawake.
Kitu kingine ni abiria kulazimika kulala wamekaa kwenye siti za basi kwani hakuna nyumba za wageni maeneo ya karibu ,sasa hapo ukiamka kesho unakuwa kama zombie akili imezubaa kabisa,.
Cha mwisho usalama wa abiria stendi mpya ya Nzega ni mdogo mno ,kuna vibaka pale sijapata kuona ole wako utoke uende uwani unakuta washapiga sachi begi.

Ushauri wangu serikali ifanye juhudi za maksudi kuboresha stendi mpya ya Nzega,abiria tunapitia mateso makubwa.vyoo viongezwe,walau boma LA kuwasitiri "walala nje" liwepo,usalama wa wasafiri uimarishwe ili basi Watanzania waendelee kuongeza maksi katika utawala wa awamu hii ya hapa kazi tu.
Muwe na Jumapili njema
 
Duu kulala Nzega kwa safari ya Mwz nikuzidi kuwatesa abiria kwakweli.... Yaani mtu ameshida amekaa siku nzima na bado unamlaza kitako akiamka anaendelea na safari
Hiyo isikie tu,ni mbaya aisee
 
Achana na miundombinu ya stand mpya na vibaka.. "kwanini mabus yalale njiani?"
Si yamefungwa vidhibiti mwendo? Kama ni utekaji polisi si kazi yao kupambana na majambazi?

Ndipo ninapoingiwa na hofu na wanausalama barabarani, pamoja na uwepo wa ving'amuzi lakini kusimamishwa ni kila walipo askari, kwanini kisitumike kituo kimoja tu katika kila mkoa
 
Hivi kama mabasi yanaingia dar mpaka saa nne usiku, maana yake yametembea toka saa kumi na mbili jioni mpaka saa nne hiyo usiku gizani, tena madereva wakiwa wamechoka ila hamna ajali wala ujambazi. Kwa nini kama imeshindikana kusafiri muda wowote usiku basi mabasi hayo yaruhusiwe kuanza safari hata saa tisa usiku na madereva wanakuwa fresh zaidi? Mfano wa dar wakitoka saa tisa au kumi alfajiri, wakifika morogoro saa moja asubuhi si haba kwamba huko waelekeako watawahi fika.
 
Sumatra wana kambia utaratibu huo ni lazima pia wizara nyingine zihusishwe kwani enda ajari itatokea saa kumi afrajili vyombo vya uokozi vitaweza patikana? je hospital muda huo za kupokea wahanga zitakuwa wazi?japo hata hizo zinazotokea mchana tu ni majanga msaada ndio huo watu wana kandamizwa na contena vyombo vya uokozi hakuna!!
 
Imeanza lini hii ya kulala Nzega tena, nachojua yale mabasi ya kujikongoja huwa yanalala shinyanga lkn ukipanda kina Kisbo, kibo safari au kidia one mnatoboa Mwanza
 
Ndipo ninapoingiwa na hofu na wanausalama barabarani, pamoja na uwepo wa ving'amuzi lakini kusimamishwa ni kila walipo askari, kwanini kisitumike kituo kimoja tu katika kila mkoa
Urasimu......
 
Mabasi machache yakifika nzega mapema kuna njia ya vumbi inachepuka unaenda kutokea karibu na kahama japokua pana mwendo pia... Big up Zube bus
 
Salaam wakuu,
Kwa masikitiko makubwa naomba nizungumzie huu utaratibu wa kulaza mabasi ya abiria nzega,sijajua shida ni nini wakati unatoka mikoa mingine kuja dar es salaam basi linafika siku hiyo hiyo lakini ajabu ukiwa unatoka dar kwenda mikoa hasa ya kanda ya ziwa basi linalala nzega na safar inaendelea kesho. Si vibaya kwa basi kulala stendi "MPYA" ya Nzega ila niseme tu mazingira ya hiyo stendi mpya ya Nzega sio rafiki kabisa,kwanza huduma za vyoo ni mbovu sana ,kuna matundu matatu tu ya vyoo na bafu moja kwa kila jinsia. Haitoshi vyoo ni vichafu sana yani wale wasimamizi wanajua kuchaji tu pesa ya huduma na sio kusafisha vyoo,hii ni hatari kwa afya zetu hasa sisi wanawake.
Kitu kingine ni abiria kulazimika kulala wamekaa kwenye siti za basi kwani hakuna nyumba za wageni maeneo ya karibu ,sasa hapo ukiamka kesho unakuwa kama zombie akili imezubaa kabisa,.
Cha mwisho usalama wa abiria stendi mpya ya Nzega ni mdogo mno ,kuna vibaka pale sijapata kuona ole wako utoke uende uwani unakuta washapiga sachi begi.

Ushauri wangu serikali ifanye juhudi za maksudi kuboresha stendi mpya ya Nzega,abiria tunapitia mateso makubwa.vyoo viongezwe,walau boma LA kuwasitiri "walala nje" liwepo,usalama wa wasafiri uimarishwe ili basi Watanzania waendelee kuongeza maksi katika utawala wa awamu hii ya hapa kazi tu.
Muwe na Jumapili njema
Nakubaliana na wewe kabisa maana na mimi hiyo kero ilinikuta ni zaidi ya mateso ni afadhali kupanda ndege kuliko mateso utakayokutana nayo kwenye basi
 
Mimi sioni sababu ya bus kulala njiani kabisa,cha muhimu kila basi au kila kampuni ya basi ilazimishwe kuwa na madereva wawili wawili kwa safari za mbali kuanzia km 500 na kuendelea 1200km (Dar to mza)n.k.
Wasaidiane njiani kwa masaa watakatokubaliana wao kwa wao na kabla safari kuanza safari abiria mnatamburishwa kuwa madereva wenu ni Kimti na Nkoi watakuwa wanabadirishana gari kwa masaa kadhaa na hii inatoka Dar to Mza hakuna kulala njiani.Mbona inawezekana?
Masuala ya kulazana njiani huku mnangatwa na mbu stand,pa kulala shida,pa kula shida,usalama shida,mnalala kwenye bus huku mnajampiana sio sawa kabisa!!!
 
Salaam wakuu,
Kwa masikitiko makubwa naomba nizungumzie huu utaratibu wa kulaza mabasi ya abiria nzega,sijajua shida ni nini wakati unatoka mikoa mingine kuja dar es salaam basi linafika siku hiyo hiyo lakini ajabu ukiwa unatoka dar kwenda mikoa hasa ya kanda ya ziwa basi linalala nzega na safar inaendelea kesho. Si vibaya kwa basi kulala stendi "MPYA" ya Nzega ila niseme tu mazingira ya hiyo stendi mpya ya Nzega sio rafiki kabisa,kwanza huduma za vyoo ni mbovu sana ,kuna matundu matatu tu ya vyoo na bafu moja kwa kila jinsia. Haitoshi vyoo ni vichafu sana yani wale wasimamizi wanajua kuchaji tu pesa ya huduma na sio kusafisha vyoo,hii ni hatari kwa afya zetu hasa sisi wanawake.
Kitu kingine ni abiria kulazimika kulala wamekaa kwenye siti za basi kwani hakuna nyumba za wageni maeneo ya karibu ,sasa hapo ukiamka kesho unakuwa kama zombie akili imezubaa kabisa,.
Cha mwisho usalama wa abiria stendi mpya ya Nzega ni mdogo mno ,kuna vibaka pale sijapata kuona ole wako utoke uende uwani unakuta washapiga sachi begi.

Ushauri wangu serikali ifanye juhudi za maksudi kuboresha stendi mpya ya Nzega,abiria tunapitia mateso makubwa.vyoo viongezwe,walau boma LA kuwasitiri "walala nje" liwepo,usalama wa wasafiri uimarishwe ili basi Watanzania waendelee kuongeza maksi katika utawala wa awamu hii ya hapa kazi tu.
Muwe na Jumapili njema
Mkuu kwani Siku hizi hawalali tena Shinyanga?
Mbona Nzega ni mbali?
Halafu Kuondoka Dar Wameshaanza SAA 11alfajiri? Au ni SAA. 12 alfajiri?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom