Kwangu mimi naona huu mfumo ni bora kuliko wa kukaa foleni. Unaingia benki, ukiona namba yako iko mbali sana unaweza kukadiria itachukua muda gani kabla namba yako haijafika then kama unashughuli nyingine ya kufanya katika kipindi hicho unaenda kufanya kisha unarudi kuchukua huduma yako.
Mimi niliwahi kuingia CRDB tawi la Millenium towers, baada ya kuona namba yangu iko mbali na kuna mtu ananisubiri Kimara, nikaenda kuattend issue ya Kimara baada ya kama saa mbili nikarudi nikakuta bado watu kama ishirini namba yangu ifikiwe nikasubiri nikapata huduma.
Kitu ambacho mabenki yetu yangefanya ni kutafuta namna bora zaidi ya kupunguza muda wa mtu kukaa Benki kana Kwamba kwenda benki ni kazi ya siku nzima, either wafungue matawi mengi zaidi kama wakiona wateja wamekuwa wengi au waongeze mashine za kuingiza hela( ATM).
Wafanye study kujua ni huduma zipi zinazosababisha watu wawe wengi ndani ya benki kwani kama kuchukua hela ATM zipo, kama watu wanahitaji kuchukua kiasi zaidi ya kinachoruhusiwa na benki basi wakiongeze nk nk