kuna utaratibu kwamba endapo utapoteza cheti chako cha kidato cha nne au cha sita haijalishi ni kwa namna gani iwe kuibiwa,kuunguliwa, kudondosha, kwenye ajali hata uje na evidence gani hutapatiwa cheti kingine, kinachofanyika km cheti hicho kitahitajika unapeleka maombi yako NECTA kuwajulisha kuwa cheti orginal kinahitajika mahali fulani mfano kwenye interview au kujiendeleza kimasomo. then wao NECTA pasi kupitia kwako wanastify matokeo yako na kuyatuma kule yanapohitajika. ni bora hata wangeweka penalty kuliko kushindwa kumpatia mtu cheti kingine pindi anapokumbwa na tatizo.imagine uko nje ya nchi na unahitaji cheti uriginal, uwasiliane na NECTA mpka waje watume hayo matokeo huko ulipo. cheti cha chuo kikuu, passport na vya kuzaliwa vyote una uwezo wa kuvipata pindi vinapopotea, why vya NECTA ishindikine, kwa hapa kuna umuhimu wa haka kautaratibu kuangaliwa upya