Utapeli zaidi wa Tigo huu hapa

Kwa muda sasa nilikuwa natilia mashaka ukweli kuhusu huduma ya Jaza Ujazwe ya kampuni ya simu ya Tigo.Jana nikakamia nikasema,lazima nihakikishe kama wanachosema ni kweli.Alas!It is all lies.

Baada ya kununua vocha yangu ya 1,000 nikajiunga na halichachi, nikaambiwa nitatumia YouTube bure kuanzia saa sita usiku mpaka sasa 12 asubuhi.Hii ilikuwa saa tisa jana. Kumbuka nina halichachi MB 150.Ilipofika saa sita nikaanza kutumia You Tube nikijua ni bure. Ghafla mtandao ukakata,kuangalia balance naambiwa nina MB 295 za YouTube tuu ikiwa na maana halichachi wamekomba!Nikaongeza halichachi MB 150 nikaendelea na YouTube,kuangalia balance halichachi inayoyoma, balance ya YouTube iko pale pale MB 295!Whooo,ajabu sana.Kumbe jamaa hata hiyo YouTube wanapima sio bure kuanzia saa sita mpaka asubuhi,halafu hata hizo MB wanazokupimia hawazitumii wanatumia za kwako!Utapeli mkubwaJamaa wanajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.TCRA mpo?
Nenda kwenye website ya tcra ndugu ujaze fomu ya malalamiko.
 
Hawa Tigo kuna Kifurushi wanacho cha Whatsapp na FB. Wanakupa 3GB kwa mwezi kwa sh 2000. Maajabu ni kuwa ukidownload au kustream fb video, wanatumia Halichachi lako. Wizi mtupu.
Itakuwa host url sio ya facebook...

Au lah definition ya charging waliyoidefine katika platform yao wameweka exceptions za huduma gani katika facebook ni bure na ipi inakula salio...

Mara nyingi hizi huduma huwa zina ujanja ujanja, definitions za charging policy huwa zina utofauti na kile watu wao wa marketing wanachokitangaza...

Mathalani kuna wakati mtandao wa simu unajinasibisha kwamba unatoa unlimited data, lakini nyuma ya pazia utakuta wanalimit speed etc
 
Kuna jambo ninahisi linaendelea kati ya Tigo na TCRA I know what i mean. Peleka malalamiko yako TCRA uone kama itachukua kwa umuhimu wowote....
 
Nimewapigia simu nimewaomba wanitoe kwenye hiyo promotion. Hawawezi kunitukana Kwa sms 20 za bure.
 
Hawa ni wezi mkuu wanakwambia umepewa Mb 100 kumbe ni kumi tigo acheni uhuni huu.
 
Kwa muda sasa nilikuwa natilia mashaka ukweli kuhusu huduma ya Jaza Ujazwe ya kampuni ya simu ya Tigo.Jana nikakamia nikasema,lazima nihakikishe kama wanachosema ni kweli.Alas!It is all lies.

Baada ya kununua vocha yangu ya 1,000 nikajiunga na halichachi, nikaambiwa nitatumia YouTube bure kuanzia saa sita usiku mpaka sasa 12 asubuhi.Hii ilikuwa saa tisa jana. Kumbuka nina halichachi MB 150.Ilipofika saa sita nikaanza kutumia You Tube nikijua ni bure. Ghafla mtandao ukakata,kuangalia balance naambiwa nina MB 295 za YouTube tuu ikiwa na maana halichachi wamekomba!Nikaongeza halichachi MB 150 nikaendelea na YouTube,kuangalia balance halichachi inayoyoma, balance ya YouTube iko pale pale MB 295!Whooo,ajabu sana.Kumbe jamaa hata hiyo YouTube wanapima sio bure kuanzia saa sita mpaka asubuhi,halafu hata hizo MB wanazokupimia hawazitumii wanatumia za kwako!Utapeli mkubwaJamaa wanajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.TCRA mpo?
Lile tangazo hujasikia vigezo na masharti kuzingatiwa
 
Nimewapigia simu nimewaomba wanitoe kwenye hiyo promotion. Hawawezi kunitukana Kwa sms 20 za bure.
Halafu hapo unakuta umejiunga tayari SMS bila kikomo. Au unapewa mb 600 za wasapu bure siku tatu na hapo umejiunga kifurushi cha wasapu mwezi... Ulaghai mtupu
 
Ni kwl kabisa hata MB 200 za chuo ZINAPOTEA kama SIAGI KIKAANGONI...hawa jamaa ni zaidi ya JOKA LA MAKENGEZA
 
TCRA wajibu hili na lile la vituo vya kurushia matangazo ya tv kama @dstv @startimes Azam TV n.k. kwanini hutonyeshwi channels za kibongo bure mpaka tulipie kifurushi?! Wahisi hata mikataba ya TCRA na TTCL iko kama ya madini aise!
Mkuu hawa ni watoto wa baba mmoja,ipo haja ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.Na it seems TCRA ni collaborators katika conspiracy hii, kwa nini hawayachukulii hatua haya makampuni ya simu pamoja na malalamiko yote haya? Tunawalaani Barrick kumbe tunao Barrick wengine, miongoni mwetu.
 
Kuna watu wana roho ngumu aseee.. kumbe bado tigo ina wateja. Hawa jamaa walinishinda tabia baada ya kuzoea kukata salio langu kila kukicha.

Siku moja nikajitoa ufahamu nikasema ngoja niwapigie customer care. Anaanza kujing'atang'ata mwenyewe. Nkamwomba aniangalizie call list yangu ya muda huu maana alisema nilimcall mtu wa airtel saa 11 na dak 27 asubuhi, bila aibu anataja namba yangu ya airtel ambayo ipo kwenye simu hiyohiyo yenye line ya tigo.
 
Back
Top Bottom