Utapeli wa kuzushiwa Watoto wetu kuumwa ghafla shuleni utasababisha ugonjwa ya moyo! TCRA chukueni hatua

Asubuhi hii baada ya kumpeleka mtoto shule nikapokea ujumbe huu wa simu:

"Habari ya saa hii mzazi uongozi wa shule tunapenda kukujulisha kwamba mwanao amepatwa na tatizo la ghafla huku shuleni. Kwa sasa tupo naye hospital mimi ni mwalimu"

Simu iliyotuma ujumbe huo ni 0712578670

Kila nilipojaribu kuipigia simu hii ilikuwa either busy au ilikuwa haipokelewi. Wapo hospitali gani ilikuwa mtihani mwingine.

Akili ikanituma kuwahi shule. Shuleni nilipofika, walimu walishangaa kwa kutokuwa na taarifa zozote kuhusiana na ujumbe huu na pia hapakuwa na tukio lolote lenye kuhusisha hospitali.

Jambo la kushukuru Mungu nimemwona mtoto yuko darasani bukheri wa afya.

Hali hii inatupeleka wapi?

Ninaandika haya huku mwili ungali wanitetemeka. Japo nashukuru Mungu halikuwa jambo la kweli lakini sidhani kuwa ilikuwa fair kuni subject kwenye degree hiyo ya stress.

Mamlaka husika zitulinde dhidi ya matepeli hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tahadhari kwa wazazi, huu ni utapeli mpya umeibuka! - JamiiForums

Sent using Vertu Signature Cobra
 
Hata mm nimetumiwa huu ujumbe. Ila mm sina mtoto. Nikajikagua P*mbu zangu nikaona zipi OK nikaendea na mishes
 
Mimi nilipigiwa simu na mwanamke mwenye lafudhi ya kichaga. Ananiambia mwanangu anaumwa. Nikashangaa mbona sina mtoto anayesoma Primary school. Leo baba yangu mzazi katumiwa message mtoto ameugua shuleni. Ni utapeli tu. Tuwe makini.
 
Nipe laki tu nimshushe busha huyo fala aliyetaka kukutapeli!
Nilikuona ulivyokuwa na presha hadi nguo ya ndani kuloa kwa jasho jingi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom