Utapeli wa Biashara za online

Bryce mziba

Member
Jul 20, 2018
22
8
Wakuu habari...

Siku hizi kama tunavojua kuna biashara nyingi sana za online huku ukifanyiwa delivery either free or malipo kidogo.

Japo ni rahisi kushawishika kwa ubora wa bidhaa wanazouza kulingana na uhitaji wako, kuna wauzaji wengine si waaminifu ni matapeli watakuaminisha ulipie nusu ya gharama ya bidhaa ukishapata mzigo unamalizia gharama ilobaki ila kinachotokea ukishalipia hiyo nusu gharama wanapotea kabisa.. kama ni simu hapokei na sms hazijibiwi unakua umeshatapeliwa tuweni makini nao mimi nimeshalizwa tayari aise.

NOTE: KWA ANAEJUA SEHEMU YA KURIPOTI HAWA MATAPELI HELA WAMESHACHUKUA NA BADO ANAPATIKANA KWENYE HIYO HIYO NO. YAKE MSAADA PLZ🙏🙏
 
Kikuu ni waamimifu mwezi ulopita niliagiza vitu vya kama 150000 yaani hakuna kilichopungua. Sema vilichelewa kidogo kama mwezi hivi badala ya wiki mbili walizonambia.
 
Poleni ninafanya biashara online pia changamoto ni pande zote

Nimebahatika kupigwa mara moja tu nilituma mzigo mteja akakimbia nao
 
Kwanza kabla hujanunua kitu online ni vizuri kufanya utafiti umfahamu huyo unaetaka kufanya nae biashara.Ikiwezekana uulize kama kuna yeyote amewahi kufanya biashara na mtu huyo wa online au kampuni hiyo.Tatu ukiwa na njema ya kuutaadharisha uma ni vizuri ukatuambia ni site gani hiyo uliyoingizwa mjini
 
Kununua au kuagiza kitu online kunahitaji umakini mkubwa sana, kuna mambo mengi sana unatakiwa kuangalia kabla ya kuagiza.
Kwa mfano:-
-Je huyo seller ana muda gani tangu aanze hio biashara
-Reviews zake zikoje kwa watu ambao walishawahi kununua kutoka kwake
Na mengine mengi.. hutakiwi kukurupuka hata kidogo kabla ya kununua chochote online.
 
Nenda kwenye page ya udaku yenye followers wengi ongea na mwenye page ya udaku kuwa utampa kiasi fulan ili amtangaze huyo mtu mwenye page ya biashara ni tapeli
Nenda hata kwa duller square.
 
Kununua au kuagiza kitu online kunahitaji umakini mkubwa sana, kuna mambo mengi sana unatakiwa kuangalia kabla ya kuagiza.
Kwa mfano:-
-Je huyo seller ana muda gani tangu aanze hio biashara
-Reviews zake zikoje kwa watu ambao walishawahi kununua kutoka kwake
Na mengine mengi.. hutakiwi kukurupuka hata kidogo kabla ya kununua chochote online.
Shukuran Mkuu
 
Kwanza kabla hujanunua kitu online ni vizuri kufanya utafiti umfahamu huyo unaetaka kufanya nae biashara.Ikiwezekana uulize kama kuna yeyote amewahi kufanya biashara na mtu huyo wa online au kampuni hiyo.Tatu ukiwa na njema ya kuutaadharisha uma ni vizuri ukatuambia ni site gani hiyo uliyoingizwa mjini
Kuna page nyingi sana instagram
Kuna jamaa anatumia account ya @Rashid_Electronics ni jambazi tapeli
 
Kuna page nyingi sana instagram
Kuna jamaa anatumia account ya @Rashid_Electronics ni jambazi tapeli
Mimi huwa naangalia kwenye comments tu..pages za kitapeli utakuwa wamezima au ku restrict comment section! Au unaweza kukuta anacomment mtu mmoja tu, kwa kila post! Ukiona hivyo achana na page hiyo
 
Back
Top Bottom