Utapeli mpya waibuka Dar

Sio kweli, out of 100 people who are rich only 5 are rich thru clean deals!!!

If you want to remain poor, adopt principles za Sophist!!

Una evidence mkuu? Halafu, unazungumzia matajiri wa nchi gani?
 
Hii hadithi imetungwa.

Hamna kitu kama hii imetokea popote.
Kama imewahi kutokea, basi ni mafala walioikwapua kwenye Internet wakajaribu kutumia mbinu hii kutapeli.

Zitaletwa nyingi tu, tungo za mfano huu. Wateja wa tungo hizi ni magazeti ya mfano wa Global publishers!
Mkuu LazyDog na wengineo...

Mimi binafsi dakika kama 10 zilizopita nimepigiwa simu kama hiyo hiyo, maelezo yaleyale, watu inaelekea pia ni walewale... Nimetoa taarifa polisi (makao makuu) lakini nilichoambulia kuambiwa ni kuwa niende kule...

Nimewapa hadi namba wanazotumia, nimewatumia hata sms wanazotuma.

Najua polisi yetu ina uzembe mkubwa sana, hawajali, wananchi wanaumizwa sana na utapeli wa namna hii.

Ni rahisi kwao ku-trace source ya simu hizi, ni rahisi kwao kuweza kuwanasa wakitaka lakini inaelekea hawana hata mpango wa kufanya hivyo... Ndo Tanzania yetu!

Mkuu amini usiamini, nimepigiwa simu ya namna hiyo dakika kama 10 zilizopita!
 
Nimeona Polisi haiwezi kutoa ushirikiano, nimewajibu kuwa siko interested... Guess what? Nikatukanwa F*ck You!

Nikawajibu kiungwana "Endeleza utapeli wenu kwa wengine lakini yana mwisho haya"
 
Nimeona Polisi haiwezi kutoa ushirikiano, nimewajibu kuwa siko interested... Guess what? Nikatukanwa F*ck You!

Nikawajibu kiungwana "Endeleza utapeli wenu kwa wengine lakini yana mwisho haya"

Pole sana mkuu,

Ukitaka polisi waje wambie kuna magendo hapa wanakuja spidi kwa vile wenyewe wataenda kuuza.
 
Hii hadithi imetungwa.

Hamna kitu kama hii imetokea popote.
Kama imewahi kutokea, basi ni mafala walioikwapua kwenye Internet wakajaribu kutumia mbinu hii kutapeli.

Zitaletwa nyingi tu, tungo za mfano huu. Wateja wa tungo hizi ni magazeti ya mfano wa Global publishers!

Ndugu ni bora ukaamini, kuna mtu ambaye namfahamu, amepoteza 3m kwenye sakata hili, hamu hana.
 
Principle 1:
Duniani hakuna bahati ya mapato bila kufanya kazi.
principle 2:
Utavuna tu pale ulipopanda. - Utavuna kile ulichopanda . . . Na sio cha mwenzio....
Principle 3:
Mapato hutokana na kazi halali, si vinginevyo.
you can say that again!! Amen
 
Mimi wasijaribu kabisa............nina machungu ya utapeli, sio hawa lakini na ni siku nyingi!!! Wakiingia tu kwangu, huyo Dr au watever ninayekutana nae, nampasua pua kwanza! halafu mengine baadae!!

umeshaona mtu anaishi dar lakini anapelekwa mahabusu Mpanda? Acha bana
 
Hii hadithi imetungwa.

Hamna kitu kama hii imetokea popote.
Kama imewahi kutokea, basi ni mafala walioikwapua kwenye Internet wakajaribu kutumia mbinu hii kutapeli.

Zitaletwa nyingi tu, tungo za mfano huu. Wateja wa tungo hizi ni magazeti ya mfano wa Global publishers!

Mkuu Lazydog, hii story nilivosoma ni sawasawa kabisa na ndgu yangu mmoja alivyotapeliwa ..yaani maelezo ni sawia kabisa. Nakuhakikishia nafahamu watu si chini ya watatu ambao wamepata hii zakhma! Kifupi tu ni kuwa hawa jamaa na polisi lao moja, kwa jinsi ninavyoona.
 
Hata mimi walisha mvaa mamsapu; akawashtukia akapiga polisi na akawaambia wanipigie mimi, hawakupiga wakaachana naye. Kwa hiyo sio ya kutunga-watch out folks !
 
Mbona mimi mwenyewe nakutana nazo nyingi tu,wameshaniletea madini feki(hawakujua kama mimi nina uelewa kiasi juu ya germstone).wakaniletea ishu inayofanana na hiyo lakini kwa mfumo mwingine(mtu anajifanya kalikamata dili lakini hana pesa hivyo wewe ndo utoe,biashara ya kununua hapa kuuza pale),ila kwenye biashara lazima tukubali kurisk lakini sio kutapeliwa,kuna njia za kumjua mtu tapeli first of all,wanalenga kwenye high returns ili ukose utulivu wa kifikra,wanakujenga tamaa,hivyo utulivu wa akili ni kikwazo cha matapeli
 
POLISI Kanda Dar es Salaam imewatahadharisha wananchi, makampuni, taasisi mbalimbali nchini kujihadhari na wimbi la utapeli lililoibuka hivi karibuni la matapeli kutumia majina ya viongozi wa Serikali, mawaziri kujipatia fedha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova amesema kumezuka wimbi la utapeli wa kupiga simu na kutapeli mamilioni ya fedha kwenye taasisi mbalimbali wakijifanya ni mawaziri.

Amesema kuwa watu hao hupiga simu na kujifanya wao ni waziri fulani na hata kuiga sauti ya waziri huyo na kusema na kuamuru apewe kiasi Fulani cha fedha kw kujifanya ana shida ya fedha kwa ajili ya ada, safari au hata matumizi mengine.

Amesema wakishaambiwa wazifuate, matapeli hao huwatuma madereva wenye magari ya serikali, yenye namba za bandia za STK na SU na kujifanya ni madereva wa mawaziri hao na wanafata fedha hizo.

Na baadae wakijaribu kuwasiliana na viongozi hao hushangaa na kukiri hawajatuma mtu yeyote kuchukua fedha.

Amesema kuwa wimbi hilo limeibuka sasa katika jiji la Dar es Salaam na matukio kadhaa yamesharipotiwa polisi na kuwataka wananchi wafanyabiashara kuwa makini sana.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3575478&&Cat=1
 
I think the heading is misleading....utapeli ulio mpya ni kwa waliotumia akili kidogo kuingilia utapeli uliozoeleka wa mawaziri ...kuamuru wapewe kiasi fulani cha fedha...ingebidi kiwe utapeli wa mawaziri waingiliwa, hao madereva waliozoa kutumwa na kuona fedha zinachotwa tu ku kutumwa bila hata maandishi kwanini na wao wasichote?
 
Utapeli huu umemkuta mwenzetu.

Ndugu wapendwa,
>
> Story ifuatayo ni ya kweli maana imenitokea mimi
> binafsi jana tarehe 11/11/2009. Najua kwa kiasi fulani
> itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni
> vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije
> mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa
> kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza
> kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza
> kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni
> watu wanaotufahamu vizuri.
>
> Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo
> likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye
> alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa
> jina na career background details zangu sikuwa na
> shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama
> ifuatavyo:
>
> TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.
> Mimi: Nzuri
>
> Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?
> Mimi: Hapana, nani mwenzangu?
> Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na
> uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World
> food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.
> Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba
> sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa
> wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana, after all
> alikuwa hajasema anachotaka)
>
> Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama
> unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna
> maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha
> vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa
> Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana
> MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises.
> Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda
> tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo
> madawa akanidhulumu na
> kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa
> mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri
> contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa
> ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii
> kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on
> delivery!
>
> NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi
> hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just
> another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya
> successfully.
>
> Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?
>
> Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr.
> Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier
> wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa
> kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid
> solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi.
> Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation,
> alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.
>
> Basi
> wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate
> kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na
> strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa
> kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake,
> ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi
> ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala
> yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa
> anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya
> chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa
> angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni
> kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million.
>
> Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya
> kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata
> ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa
> maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe
> kwa bosi wake for further final details.
>
> Basi wandugu kama mnavyonijua
> katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili
> nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata
> calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd
> 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd
> 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU
> tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on
> in my head!
>
> Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake
> ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:
>
> MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new
> supplier?
> MIMI: YES
> MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid
> solution; we are looking for 50 pairs?
> MIMI: Yes I have sufficeint stock
> Mzungu: what is your price per pair?
> Mimi:$1700
> Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to
> be paid in dollars or TZS
> MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local
> currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha
> kuwa ni International businessman)
> Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be
> paid cash or by cheque?
> Mimi:Cash
> Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new
> supplier we need this liquid urgently possibly today, and
> since you have said you have enough
> stock we are taking off this morning from Kigoma coming to
> Dar, please arrange for the transport to take us to
> Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most
> importantly make sure you bring one pair of the sample with
> you.
> Mimi: No problem at all I have been in this business for
> quite sometime now you can be sure everthing will be fine.
>
> Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque
> book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample
> yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank
> nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa
> sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa
> anaelekea
> Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo
> tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha
> gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi
> mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija.
> Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi
> wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo
> fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana
> akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample
> kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka!
> NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana
> akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa
> itakamilishwa saa nane.
>
> Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri,
> nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza
> bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000
> nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (Kumbuka
> mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).
>
> Basi mimi mbio nikaenda
> airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize
> biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna
> kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi
> tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride
> nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza
> akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita,
> nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last
> week.
>
> Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na
> mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na
> makabila mengine.
>
> So guys thats my story for yesterday!
 
3rd time hii mambo inabandikwa hapa JF, ndani ya wiki moja!
Nishacomment sana , now wll be silent!
 
Jumamosi tarehe 23/01/2010 nilipigiwa simu kutoka namba+243 999 043 477 kutoka kwa jamaa mmoja anaitwa Frank analisema yupo kongo DRC akaniambaia kuwa ananifahamu na nilimpa namba yangu tulipokutana kariakoo. Jamaa anaongea english ya kenya hivi. Ananiambia kuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya wachina inayonunua madini na kusafirisha nje ya CONGo.

Jumapili alinipigia simu mara mbili tukaongea kiurafiki tu na mara ya tatu alipopiga sikupokea. Ila jumatatu tarehe 25/01/2010 alinipigia simu ahsubuhi saa tatu dakika 31 akanieleza kuwa ana deal anataka niifanye naye. Kuwa kuna dawa inaitwa MAYORDANE inayotumika kwa farasi ulaya na dawa hii ni ya farasi dume. inauzwa dola 120,000. ameniambia kuwa mnunuzi wake ambaye yupo ufaransa hawezi kwenda kongo kutokana na hali ya amani kule, hivyo kama naweza kutrade kutoka Dar es salaam itakuwa poa na yeye atamtuma jamaa yake mwenye hiyo dawa ili tukutane dar nikisha wasiliana na Mzungu. Mzungu anaitwa Mr. david namba yake ni +336 158 986 90. ameniambia nimpigie ili tukubaliane kwamba anaweza kuja Tz kununua hiyo dawa. Bado sijampigia hadi sasa.

Kwa kuwa nina mashaka na huyu mtu kwamba sifahamiani naye (kwani kumbukumbu zangu haziongopi) pia kwa kuwa sipendi kushiriki deal chafu (za chini ya meza) niliamua kumshirikisha mwana JF mmoja ambapo aliniambia na yeye walishamtafuta kwa njia hiyo, hna hizi deal zinafanywa na watu wanaomfahamu mpigiwaji simu ili wamwingze ktk deal hizi kwa minajili ya kummaliza. Mwana JF huyo aliniambia kuwa alitoa taarifa kwa polisi kupitia ofisi ya DCI tangu kati kati ya mwaka jana lakini hakuna chochote kilichofanyika. Nikapata mashaka sana kama vyombo vya usalama vya nchi hii vipo kwa ajili ya kuwalinda viongozi tu na si raia zake pale ambapo kuna harufu ya kufanyika frauds za namna hii.

Nipotayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuwatia nguvuni hawa spinners ili kupunguza wimbi la uhalifu wa kimataifa unaoinyemelea tanzania....

Nimetoa taarifa na ninaomba msaada jamani
 
scam!............
AU BLACKMAILING!...
mwambie georgieporgie akusaidie kumtrace!jamaa yupo fit
 
Ni wazo zuri sana kuwatia nguvuni watu hawa. nINGEKUWA mimi ningewasiliana na watu wa usalama, nikiona wananirusha NACHUKUA SHERIA MKONONI.
 
Back
Top Bottom