Utapeli mpya waibuka Dar

Mkuu, jukumu la usalama wako linaanzia kwako mwenyewe... lazma na wewe uende polisi, inawezekana kabisa polisi wanfanya kazi yao ila wewe hujui bali uko kwenye surveillance tu hadi hao jamaa watakapokusogelea

kingine muhimu ni kwamba umeanika sana kiasi kwamba wanaweza kukuharibia

Pole sana Msanii na nina imani hili ni jambo dogo na utapata seurity na safety ya kutosha, amini nikuambiayo
 
kama hivyo ndivyo usalama upo hatarini vp na wale ni wasanii ata ungekula pesa yao akuna kesi kwani inakuwa nichambo mikunafulani waliibuka wa madawaya famigation nikawageuzia kibao wakaingia mitini
 
Msanii inaonekana ulitaka kusaniishwa!!! Tatizo umeanika mapema sana kiasi kwamba hata wenyewe wanaweza kupata khabar!! sababu wote hao wanaokusaniisha ni wabongo tu!! Wazungu siku izi wapo hadi kariakoo congo!! Unapewa no za nje unaongea na matapeli wa bongo walioko huko alafu wanawatuma wazungu wa kariakoo kuja kukusanii!! Na mara nyingi utapeli wa muda mrefu huwa wanahakikisha wanakuacha penyless!!!! Mi nakushauri toa taarifa polisi alafu achana nao kabisa. Sababu umeshawaanika wanaweza wakatumia mbinu nyingine ya kukusanii ukijua unawakamatisha kumbe unatapeliwa!!
 
Jumamosi tarehe 23/01/2010 nilipigiwa simu kutoka namba+243 999 043 477 kutoka kwa jamaa mmoja anaitwa Frank analisema yupo kongo DRC akaniambaia kuwa ananifahamu na nilimpa namba yangu tulipokutana kariakoo. Jamaa anaongea english ya kenya hivi. Ananiambia kuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya wachina inayonunua madini na kusafirisha nje ya CONGo.

Jumapili alinipigia simu mara mbili tukaongea kiurafiki tu na mara ya tatu alipopiga sikupokea. Ila jumatatu tarehe 25/01/2010 alinipigia simu ahsubuhi saa tatu dakika 31 akanieleza kuwa ana deal anataka niifanye naye. Kuwa kuna dawa inaitwa MAYORDANE inayotumika kwa farasi ulaya na dawa hii ni ya farasi dume. inauzwa dola 120,000. ameniambia kuwa mnunuzi wake ambaye yupo ufaransa hawezi kwenda kongo kutokana na hali ya amani kule, hivyo kama naweza kutrade kutoka Dar es salaam itakuwa poa na yeye atamtuma jamaa yake mwenye hiyo dawa ili tukutane dar nikisha wasiliana na Mzungu. Mzungu anaitwa Mr. david namba yake ni +336 158 986 90. ameniambia nimpigie ili tukubaliane kwamba anaweza kuja Tz kununua hiyo dawa. Bado sijampigia hadi sasa.

Kwa kuwa nina mashaka na huyu mtu kwamba sifahamiani naye (kwani kumbukumbu zangu haziongopi) pia kwa kuwa sipendi kushiriki deal chafu (za chini ya meza) niliamua kumshirikisha mwana JF mmoja ambapo aliniambia na yeye walishamtafuta kwa njia hiyo, hna hizi deal zinafanywa na watu wanaomfahamu mpigiwaji simu ili wamwingze ktk deal hizi kwa minajili ya kummaliza. Mwana JF huyo aliniambia kuwa alitoa taarifa kwa polisi kupitia ofisi ya DCI tangu kati kati ya mwaka jana lakini hakuna chochote kilichofanyika. Nikapata mashaka sana kama vyombo vya usalama vya nchi hii vipo kwa ajili ya kuwalinda viongozi tu na si raia zake pale ambapo kuna harufu ya kufanyika frauds za namna hii.

Nipotayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuwatia nguvuni hawa spinners ili kupunguza wimbi la uhalifu wa kimataifa unaoinyemelea tanzania....

Nimetoa taarifa na ninaomba msaada jamani
You were right by being suspicious. The best solution is tell him frankly that you are not interested in the business full stop. Jamaa hawa wameshaliza watu wengi sana na katika syndicate hizi kuna watu wa aina mbalimbali wahindi/wazungu/wakenya/wasenegal nk ndoano yao ni kukutia tamaa ya faida ya haraka haraka lakini at the end of the wanakuliza au hukuwacha with an empty bag na wewe kufanywa scapegoat ukatiwa nguvuni.
 
Back
Top Bottom