Utapeli mpya, magari, viwanja, nyumba kupitia simu za mkononi.

maju

Senior Member
Oct 20, 2011
118
28
Watanzania wenzangu kuna wizi mpya unaotumiwa na kampuni inayotoa huduma kushirikiana na makampuni yetu ya simu za mnkononi inayojitangaza kupitia radio ya clouds FM, kwamba wanauza magari, viwanja , kupangisha nyumba na kutafutia watu kazi.Utafiti uliofanyika umeonesha dhairi hii kampuni ni ya kitapeli na haina uwezo huo technically.Hawa wahuni wanachofanya ni kumiliki namba ya SHORT CODE mfano; 155xx ect, ambayo hutolewa ana TCRA kisha kuisajili kwenye makampuni ya simu ili wagawane mapato kwa kila sms zipitiazo kwenye SHORT CODE hiyo (kila sms Tshs. 500). Kisha huitangaza kwa nguvu zote kwenye Radio station husika. Mtanzania anayetuma sms huliwa pesa zake wakati hawa jamaa hawana hata database ya huduma husika, hata ofisi zao hawana hata miundombinu zaidi ya komputa ya muhudumu wa ofisi. Mwisho wa siku hawa jamaa hupitia kwenye makampuni ya simu kufuatilia sms zilizoingia ili wapate mgawo wao. Nawasihi watanzania tuwe makini na hizi promosheni za wizi zinazopitia short code zitolewazo na tcra kwenye simu za mkononi. Na TCRA wawe makini na watu wanaowapatia hizi short code kwani watanzania wanazidi kuibiwa na hawa matapeli.
 
Mwana wane - tunashukuru kutupunguzia RISK za maumivu, sijui kwanini TZ imekuwa ni chaka la kutuibia fedha?
 
Ni suala tu la what if (Je itakuwaje kama TCRA au mshika dhamana nae ana % yake???) maana hainingii akilini kuwa wanaweza mpa mtu shortcode ambaye hana hata sifa na uwezo, yaani wao binafsi kama ofisi hawajiridhishi kabla ya kutoa huduma kwa wateja wao??
 
MNAFIKIRI WATU WATAKULA WAPI KAMA HAWATUMII NJIA MBADALA NA AKILI..
KAZI hazipatikani, mtu afanyeje?? University zinaongezeka na kila mwaka zinamwaga ma-graduates mtaani..
Ili uishi mjini lazima utumie akili... Nyie endeleeni kulalamika, wenzenu wanafaidi kwakutumia akili na loop-holes kwenye system.
Go figure!!:hat:
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom