TECHMAN
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 2,651
- 1,125
Kijana wangu mmoja anasoma katika chuo fulani cha computer Arusha, Baada ya wiki moja ya masomo yake nikampa kazi fulani anisaidie lakini baada ya kugusa computer yangu akabaki akishangaa, nikamuuliza kwanini akasema hayo hajafundishwa. Nilipotazama course work zake nikakuta anafundishwa Introduction WINDOWS 95,98,200O AND ME upande wa msoffice nikakuta office 97,2003. Ikabidi niende katika chuo anachosoma, nikakuta kuna wanafunzi wengi sana wanachukua mafunzo ya computer. Sikuwenza kumpata muhusika wangazi za juu wa chuo ila niliemkuta nikamwambia wanafanya wizi mmbaya sana.