Utani kati ya makabila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utani kati ya makabila

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MaMkubwa1, Jan 11, 2012.

 1. M

  MaMkubwa1 Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamani hodi humu jamvini!
  Huenda swala hili limeshaongelewa huko nyuma ... mimi sijui maana mie ni mgeni. Lakini ni katika kutafuta ufahamu. Je UTANI kati ya makabila ulitokana na nini? Japo dhana hii ina mwelekeo wa kizamani / wa kale ukizingatia juhudi zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika kuelekea kwenye utaifa ikiwa ni pamoja na ndoa za watu wanaotoka makabila tofauti , lakini haimaanishi kutotafuta jinsi jamii tofauti zilivyoweza kupatana na kuishi katika msingi na mifumo fulani fulani. Hivyo kwa sasa tuongelee “utani” kati ya makabila. Je ulitokana na nini? Haya makundi yalichaguana vipi kuwa ‘watani”? Je hii ni dhana ya huku kwetu Tanzania tu au na kwingineko ipo?
   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wewe unaonaje kama MTz lazima ujue
   
 3. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Utani ulifuatia mnyukano, mapigano kati yao, heshima ikajengwa na wakaitana watani (MngoniVs Mnyamwezi/MngoniVs Mhehe ..... endeleza
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nadhani hata sasa hivi ili heshima iwepo lazima tuwanyuke kwanza CCM halafu baadaye atakuwa mtani wetu
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kuna mtu humu nataka nimnyuke ili badae awe mtani wangu.
   
 6. triza

  triza Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchaga na mpare.......... na wewe endelea
   
 7. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Kabila lenye watani wengi ni lipi? Nahisi WANGONI, sina uhakika
   
 8. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Msukuma vas Mzaramo, Mngoni Vs Mbena, Mluguru, Mfipa, Mnyakyusa, Msukuma, Mnyamwezi, Mmakonde, Mndengeloko, ........
   
 9. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,276
  Likes Received: 10,306
  Trophy Points: 280
  Samahani mmeenda nje ya mada. Mimi nitaenda moja kwa moja kwenye point.

  1. Kumbuka Asilimia kubwa ya watanzania ni wabantu. Kwa hiyo tumetokea kwenye jamii ya aina moja. Nakatika makabila ya kibantu yana dhana zifuatazo:-
  a. Mashemeji kutania.
  b. Babu na wajukuu. Na mengine mengi.
  Katika kugawanyika kwa makabila ya kibantu yaligawanyika na dhana hiyo hiyo. Na makabila yote haya unayo yaona yametokana na koo mbalimbali. Kwa hii mantiki matani haya yote ni ya kihistoria.

  2. Kuhusu nchi nyingine. Kwa uelewa wangu, kwa nchi za kibantu zinadesturi ileile. Lakini nchi ambazo si za wabantu si dhani kama wanautani huu. Maana mambo ya utani ni utamaduni wa kibantu, Katika kuelimisha, kukosoa, vilivile kuburudisha.
   
Loading...