malisoka
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 1,860
- 2,639
Kuweni Makini na watu aina ya Machali.
Kuna mtu anaweza akahama chama na usipate shaka na maamzi yake! ILA bahati mbaya watu wengi hasa wanasiasa UCHWARA wamekuwa watafuta pesa na siyo watu wakutaka mabadiliko ya dhati katika kuijenga Tanzania iliyo imara..
Ni jambo la wazi kabisa kinachowasumbua wengi siyo kuijenga Tanzania bali ni kutafuta wapi watapata ahuweni ya maisha na jibu lahisi kwao imekuwa ni siasa. Bahati mbaya wanaofanya haya mambo ni watu wenye elimu zao..jaribu kufuatilia wajinga wengi wa siasa utagundua siyo watu mbumbumbu..
Mosses Machali ni kijana mdogo tu nadhani hana miaka 35 lakini ndani ya muda mfupi amezunguka vyama vyote vikubwa hapa Tanzania unavyojua, hivi unamwamini vipi mtu kama Machali..ni vipi ndani ya miaka isiyozidi KUMI uwe umemaliza vyama vyote vya siasa!
Machali kila anakoelekea lengo na dhamila yake kubwa ni kujipatia kipato..hivi kwa hali hii unategemea kijana wa namna hii ataaminika kwa jamii na watu wanaomzuka! sidhani kama hata mke wake anamwamini.
Machali, zawadi utakayoipata kesho ndani ya CCM ni kuandikwa kwenye page ndogo ya gazeti la UHURU kuwa Machali arudi CCM baada ya hapo rudi Kigoma ukauze DAGAA.
Eti Machali hana imani na Kafulila, hana imani na Zitto eti ana imani na Magufuli..hizi ni njaa za wazi wazi..
Asilimia kubwa ya vijana na wazee katika nchi hii wana tabia za akina Mosses, rudi nyuma kidogo kwa mzee Lipumba, Wasira nk. hawa ni watu wa matumbo tu na siyo lolote!
Bahati mbaya huyu kijana msaka ugali hajajua akili ya mh Rais.. mimi siyo mchawi ila unachokitafuta ndani ya CCM na kwa Magufuli hutakipata, kumbuka na wewe ni ng'ombe asiye na mkia! waulize ng'ombe walio na wasiyo na mkia wanavyosoma namba..
Nakutakia utamazaji mwema wa siasa na karibu uswahilini.
Wewe hujajua tu watu wa Chigoma wote wako hivyo hivyo ebu jaribu kuorodhesha wanasiasa walihama chama kimoja kwenda kingine Utaniamini tu. Ni wasumbufu sana. HATA kwenye mambo ya dini (makanisani) amini usiamini hawajatulia kabisa. Ni kama sample flani ya watu wa aina yake duniani. Labda wameathiriwa na kukaa mpakani mipakani maana huwezi kujua ni muha, mkongo, mhutu,mtusi na nk.
yupo bwana mmoja alihama chama fulani akahamia upinzania, akahama tena kurudi alikotoka na kupata ubunge na hata muda si mrefu akawa mwenyekiti wa chama hicho katika mkoa (hiyo ni chigoma).
Ukimuona mtu wa Chigoma mchukulie hivyo hivyo ila KUWA NAYE MAKINI IS NOT PERMANENT ALWAYS TEMPORARY!!!.