Mabinti waliookoka hawavai hereni, mikufi, pete, na bangili.
Mabinti waliookoka hawajirembi kwa rangi za mdomo, rangi za uso, kucha wala rangi za macho.
Babinti waliookoka 'hawakaangi' nywele zao, wala hawasuki nywele wala hawajipambi kwa nguo za thamani kubwa.
Biblia inasema hivi katika 01 Timotheo 02:09-10:-
" 09: Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;10: bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu".