Utamtambuaje askari kanzu?

Utamtambuaje askari kanzu?

Sinkala

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Posts
1,773
Reaction score
688
Nimekuwa nikiona baadhi ya watuhumiwa wakiwa wameshikiliwa au kusindikizwa chini ya ulinzi wa wa askari wanaoitwa "Askari Kanzu". Juzi juzi mitaa ya barabara ya Nyerere maeneo ya njia panda Segerea nimeshashuhudia defender ikiwa inapita mitaani huku ikibeba watu waliovalia kiraia wakiwa nyuma ya gari huku wakishikilia silaha na kuyaamuru magari mengine yawapishe kwani gari lao lilikuwa katika mwendo wa kasi kama vile wanawahi tukio fulani. Nilipouliza watu pale nikaambiwa hao ni askari kanzu.

Nilipoangalia namba za usajili za gari lile niliona ni za kawaida tu (T nnn XXX), sio za magari ya Police (PT XXX). Sasa nilijiuliza maswali, hawa jamaa wamevalia kiraia, na gari lao lina namba za kiraia, lakini wameshika bunduki wakiwa katika mwendo wa kasi. Je, majambazi hawawezi kuwa katika hali waliyokuwa nayo wale askari kanzu?

Kauli mbiu ya jeshi la Polisi inayoitwa Polisi jamii itatekelezwaje iwapo mimi sijui nani ni askari na nani ni jambazi? Naombeni mnisaidie ninyi mnatumia njia gani kuwatambua askari kanzu.
 
Ukistaajab ya Musa......
Endelea kuishi shekhe mambo yao waachie wenyewe kwa sasa
 
Kwa hiyo utamtambua kwa kujifanya na wewe ni askari kanzu.
 
Hii ni hatari kweli kweli, vitu vingine vinafanyika bila kufiria athari zake. Majambazi wakipanda defender na kiturubai kwa juu kisha wakatoka kwa mwendo kasi na mitutu yao mabegani au ikiwa tayari imesetiwa dizaini ya Wakanzu wetu hapo ni balaa tupu, watapita na wabongo watapisha barabarani bila taabu.
 
Action and reaction are equal and opposite "askari kanzu = y.Jambazi" where y is a function of askari kanzu
 
Mkuu Sinkala askari kanzu katika hali ya kawaida kama hawamo kwenye defender basi ni ngumu kumtambua.
 
Hii ilishatokea, kuna jamaa alifuatwa na majambazi nyumbani kwake wakiwa na defender , wakagonga geti mlinzi akauliza kupitia kadirisha kadogo awasaidie nini, majambazi yakasema tunamuhitaji mzee anahitajika kituo cha polisi, ujumbe ukapelekwa kwa mzee, mzee akasema waambie nakuja ngoja niwapigie kituoni niwaulize kulikoni, majambazi kusikia hivyo wakatimua mbio na defender yao!

TUWE MACHO NA AKILI KUMKICHWA
 
Mkuu Sinkala askari kanzu katika hali ya kawaida kama hawamo kwenye defender basi ni ngumu kumtambua.
Thanks, lakini je, kwani defender zote ni mali ya Police?
 
Thanks, lakini je, kwani defender zote ni mali ya Police?

Zipo na za watu binafsi tena ukipita nayo mtaani wale wahalifu huwa wanakula kona utashangaa kijiwe cheupe gafla.
 
Aisee umenichekesha sana!

Kibaya zaidi wenye defender kama za polisi vile vibandiko kama Insurance wanapandika kwenye kioo cha mgongoni pale ukiona kio cha mbele cheupe hata ikipita walipo trafic wanajua wenzetu hao...wapo kazini.
 
Katika hii "nji" yetu ni vigumu sana kuwatofautisha askari kanzu na polisi. Ni wale wale. Serikali imewatelekeza wanajitafutia wenyewe kama kuku wa kienyeji. Usombe wkushukie watakung'ang'ania hata kwa dogo tu!
 
Back
Top Bottom