Utamtambuaje askari kanzu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamtambuaje askari kanzu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sinkala, Jun 11, 2010.

 1. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikiona baadhi ya watuhumiwa wakiwa wameshikiliwa au kusindikizwa chini ya ulinzi wa wa askari wanaoitwa "Askari Kanzu". Juzi juzi mitaa ya barabara ya Nyerere maeneo ya njia panda Segerea nimeshashuhudia defender ikiwa inapita mitaani huku ikibeba watu waliovalia kiraia wakiwa nyuma ya gari huku wakishikilia silaha na kuyaamuru magari mengine yawapishe kwani gari lao lilikuwa katika mwendo wa kasi kama vile wanawahi tukio fulani. Nilipouliza watu pale nikaambiwa hao ni askari kanzu. Nilipoangalia namba za usajili za gari lile niliona ni za kawaida tu (T nnn XXX), sio za magari ya Police (PT XXX). Sasa nilijiuliza maswali, hawa jamaa wamevalia kiraia, na gari lao lina namba za kiraia, lakini wameshika bunduki wakiwa katika mwendo wa kasi. Je, majambazi hawawezi kuwa katika hali waliyokuwa nayo wale askari kanzu? Kauli mbiu ya jeshi la Polisi inayoitwa Polisi jamii itatekelezwaje iwapo mimi sijui nani ni askari na nani ni jambazi? Naombeni mnisaidie ninyi mnatumia njia gani kuwatambua askari kanzu.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ukistaajab ya Musa......
  Endelea kuishi shekhe mambo yao waachie wenyewe kwa sasa
   
 3. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Utawatambua kwa matendo yao - BTW: Askari Kanzu wengi ni ex-Majambazi!
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...and majambazi wengi ni EX-Askari Kanzu
   
 5. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo utamtambua kwa kujifanya na wewe ni askari kanzu.
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hii ni hatari kweli kweli, vitu vingine vinafanyika bila kufiria athari zake. Majambazi wakipanda defender na kiturubai kwa juu kisha wakatoka kwa mwendo kasi na mitutu yao mabegani au ikiwa tayari imesetiwa dizaini ya Wakanzu wetu hapo ni balaa tupu, watapita na wabongo watapisha barabarani bila taabu.
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Action and reaction are equal and opposite "askari kanzu = y.Jambazi" where y is a function of askari kanzu
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Sinkala askari kanzu katika hali ya kawaida kama hawamo kwenye defender basi ni ngumu kumtambua.
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii ilishatokea, kuna jamaa alifuatwa na majambazi nyumbani kwake wakiwa na defender , wakagonga geti mlinzi akauliza kupitia kadirisha kadogo awasaidie nini, majambazi yakasema tunamuhitaji mzee anahitajika kituo cha polisi, ujumbe ukapelekwa kwa mzee, mzee akasema waambie nakuja ngoja niwapigie kituoni niwaulize kulikoni, majambazi kusikia hivyo wakatimua mbio na defender yao! TUWE MACHO NA AKILI KUMKICHWA
   
 10. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Thanks, lakini je, kwani defender zote ni mali ya Police?
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Zipo na za watu binafsi tena ukipita nayo mtaani wale wahalifu huwa wanakula kona utashangaa kijiwe cheupe gafla.
   
 12. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aisee umenichekesha sana!
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kibaya zaidi wenye defender kama za polisi vile vibandiko kama Insurance wanapandika kwenye kioo cha mgongoni pale ukiona kio cha mbele cheupe hata ikipita walipo trafic wanajua wenzetu hao...wapo kazini.
   
 14. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni hatari sana
   
 15. H

  Hammer Member

  #15
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hii "nji" yetu ni vigumu sana kuwatofautisha askari kanzu na polisi. Ni wale wale. Serikali imewatelekeza wanajitafutia wenyewe kama kuku wa kienyeji. Usombe wkushukie watakung'ang'ania hata kwa dogo tu!
   
Loading...