Utambulisho wa Joseph

Utambulisho wa Joseph

Tz7

New Member
Joined
Apr 10, 2025
Posts
4
Reaction score
5
Habari za wakati huu wanajukwaa wenzangu,

Naomba nitumie fursa hii kujitambulisha rasmi.
Naitwa Joseph Lucas Mkumbo, nina umri wa miaka 38 na ninatokea Utemini, mkoani Singida. Kwa sasa ninahudumu kama Manager Director wa kampuni ya Africa Sites Mineral, iliyopo Ikungi – Mang’onyi, mkoani Singida.

Kampuni yetu inajishughulisha na shughuli mbalimbali katika sekta ya madini, ikiwemo:

Uchimbaji wa madini ya aina zote,

Upimaji na tathmini ya maeneo ya madini (site analysis),

Na huduma za kitaalamu za kijiolojia (geological services & analysis) kwa mujibu wa viwango vya kitaalamu na kimataifa.


Mbali na shughuli hizo, pia ni Mwenyekiti wa UVCCM Utemini – Mkoa wa Singida, nikiwa pia mwanasiasa mkomavu mwenye dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa na kuliletea maendeleo kupitia ushirikiano wa kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Nimejiunga na JamiiForums kwa lengo la kujifunza, kuchangia mijadala yenye tija, na kushirikiana na wanajukwaa katika kuibua hoja na suluhisho kwa changamoto zinazotukabili kama jamii.

Najivunia kuwa sehemu ya “Great Thinkers”.
Karibuni kwa maoni, ushauri, na ushirikiano wa aina yoyote.

Asanteni sana.
 
Una uhakika kuwa mteule wa Rais ambayeni CCM atatenda haki kwenye kusimamia uchaguzi? Leteni mabadiliko ndani ya chama kwa kukataa vitu visivyo haki lla sivyo huna dhamira ili njema na ujana wako unakuwa bure kabisa
 
  • Thanks
Reactions: Tz7
Mkuu determine organization culture kbla hujajimaliza.

Kumbe na wewe ni chairman wa ongezeko la MATATIZO.
 
  • Thanks
Reactions: Tz7
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa maelezo mafupi kwa jamii yetu kufuatia mijadala mbalimbali iliyoibuka baada ya utambulisho wangu kwenye jukwaa hili. Nimeyasoma baadhi ya maoni na mitazamo, na kwa heshima kubwa, napenda kusema yafuatayo

Kwanza, najua kuwa kila jamii ina watu wa mitazamo tofauti, na kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni. Mimi ninayaheshimu mawazo yote — hata yale yasiyonifurahisha — kwa kuwa naamini mazungumzo ya wazi hujenga jamii iliyo huru na yenye fikra pana.

Pili, dhamira yangu si kujitafutia umaarufu wala kujipatia nafasi zisizo halali, bali ni kuchochea fikra mpya, kuonyesha kuwa kila kijana anaweza kuibuka kutoka mtaani na kufanya mambo makubwa — kupitia sanaa, ubunifu, au uongozi wa kijamii.

Filamu ninazozitayarisha kama Sweet Mamy na Litti Kidanka ni sehemu ya jitihada hizo; ni sauti ya waliokosa jukwaa, ni historia na simulizi za watu wetu, na ni nyenzo ya mabadiliko chanya.

Niko tayari kupokea ushauri, kukosolewa kwa heshima, na kushirikiana na yeyote mwenye nia njema kwa taifa letu. Tusitumie jukwaa hili kuumizana bali kujifunza, kujenga, na kuinua vipaji vya Watanzania.

Mimi ni Mtanzania kama ninyi, ninayependa nchi hii, na ninayeamini kuwa kila mmoja ana mchango wa kipekee katika ujenzi wa taifa.
 
Back
Top Bottom