Utamaduni wetu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamaduni wetu...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lizzy, Jul 18, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Naomba kuuliza hivi utamaduni wetu waTanzania ni upi haswa?!

  “utamaduni wetu“ ambao watu hua wanautumia kupinga mambo kibao japo haujulikani (maana ukiwaomba wauelezee wanashindwa) huo utamaduni ni upi?!

  Tukiweka dini pembeni (utamaduni tulioletewa na mzungu na mwarabu) tamaduni zetu kuhusiana na mavazi ni upi?Maana kila siku sikosi kusikia wanawake/wanaume wa Kiafrika wamesahau utamaduni wao siku hizi ni nguo za kubana na kuonyesha maungo.Tukifuata utamaduni wetu tunatakiwa tuvae mavazi ya aina gani?!

  Malezi kwa watoto yanatakiwa yawe ya aina gani!?

  Ndoa inatakiwa ichukuliwe vipi?!

  Infidelity inatakiwa ichukuliwe vipi?!

  Nafasi/tofauti kati ya mwanaume na mwanamke kwenye jamii iweje?!

  Hivi ni baadhi tu ya vitu nnavyokumbuka ambavyo watu hua wanatumia “utamaduni wetu“ either kuvikubali au kuvikataa pale wanapoona inawafaa.
  Sasa je huo utamaduni NI UPI!!?Tuelimishane tafadhani....
   
 2. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hii post imeanzishwa saa 1.27 ya tarehe 18 July 2011. mpaka sasa 1856Hrs hakuna input. This may either mean:

  1. utamaduni wetu unajulikana kinagaubaga, japo inawezekana haujaandikwa. the fact kwamba unajua nguo fupi na za kubana sio sehemu ya utamaduni wetu, that explains kuwa kumbe tunao utamaduni wetu (mila na desturi) zinazozungumzia ajenda hiyo. kwa hiyo kwa ufupi hakuna cha kuhangia kwenye hii mada. AU

  2. ni mada ngumu kuanza kuitambulisha hapa jukwaani. AU

  ni mawazo yangu tu kuchokoza michango!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  utamaduni wetu kwenye ndoa
  nikuwa
  mwanaume ataruhusiwa kuoa wanawake wengi atakavyoweza

  ili mradi kila mwanamke awe na nyumba yake na shamba lake.....

  huo ndo utamaduni...
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Utamaduni / Customs is not written on stone and always change overtime..., so utamaduni wetu is what is applicable and seen as normal currently

  Enzi za kuabudu miti na mizimu na kina dada kutembea kifua wazi na wengine kuvaa magamba ya miti na ngozi za wanyama is not applicable kwa sasa, kwahiyo utamaduni wetu wa sasa ni kama ifuatavyo
  • heshima kwa wakubwa na kuvaa mavazi ya heshima ambayo hayatakudhalilisha wewe au familia yako
  • Apart from muslims mke ni mmoja na sio busara kutoka nje ya ndoa
  • Malezi ya watoto inabidi yafate maadili yanayokubalika kwa jamii ingawa mtoto asipigwe kama ngoma
  • Infidelity has never and will never be Okay... labda enzi za Gentiles State au Old Stone Age
  • Wanawake nao wanaweza sio kama zamani kwahiyo wapewe fursa sawa na wanaume
  Remember what is applicable and okay now, may not be so tomorrow...
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Safi sana, swali zuri na vigugumizi vimeongezeka! Where r the rest of GThinkers, too tired to think eenh!

  Mie nasema, utamaduni wetu waafrica wa sasa ni haki sawa kwa wote; kuvaa mavazi kulingana na weather, function na trend. Na mwisho do whatever u feel like doing mradi huvunji sheria za nchi!
   
 6. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  tuwaulize CCM maana wao ndo tuliwapa dhamana ktk kipindi chote hicho! vinginevyo sisi hatuna jibu na Mungai alishabadilisha mitaala yote
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwani wa kenya au uganda ni upi?
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tujue kwanza yetu ndo tuulize ya jirani...ila hao wenzetu sio kawaida yao kuhusisha kila kitu na “utamaduni wetu“.
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Utamaduni wetu ulilikuwa Baba ndio kiongozi wa familia na ndugu kama vile Mjomba, Shangazi, Mama Mdogo. Mtoto wa dada yako, Mtoto wa kaka yako, hawa wote ni watu wako wa karibu sana.
  Lakini sasa mambo yamebadilika kina mama ndio wanaongoza nyumba, na mambo ya undugu hamna tena, inakuwa kama Ulaya na Marekani, familia ni Baba Mama na Mtoto hakuna tena kuongeza mtu
   
Loading...