Katiba tuitakayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba tuitakayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 21, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KATIBATUITAKAYO
  KITABU 2
  KWA NINI TUUJADILI MUUNGANO
  Kimetayarishwa na:
  BARAZA LAKATIBA
  ZANZIBAR
  2012
  Imesaidiwa na:
  Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA)


  Utangulizi

  Kama tunavyojuakuwa Tanzania, yaani pande mbili za Muungano za Zanzibar na Tanganyika zimokatika kushiriki mjadala wa kitaifa wa Uundwaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, mjadala ambao ni wa kwanza wa kiwango chake kwa takribanmiaka 50 ya Muungnao tokea kuundwa kwake hapo 26 April, 1964.
  Fursa yakushauriwa wananchi moja kwa moja inakuja kwa mara ya kwanza katika Muunganoambao umeundiwa Kamati kadhaa, umeleta vuta nikuvute kadhaa, na ambao hadi leouna maeneo kadhaa ambayo undani wake, upana wake na kina chake haujulikani kwasababu za kimuundo na kiutekelezaji.
  Kwa upande waZanzibar Muungano ulikuja kwa ghafla mno ikiwa ni takriban siku 100 tu, tangukufanyika kwa mapinduzi ya 1964, ni wazi kuwa nchi ilikuwa haijatulia na imokatika mchakamchaka wa mapinduzi. Kwa upande wa Tanganyika ambayo ilipata uhuruDisemba 1961 na Muungano kuundwa 26 Aprili 1964, ikiwa ni zaidi ya miaka miwilibaada ya Uhuru wao, ilikuwa ni muda wa kutosha wa kujenga utulivu na uzoefu wandani ya nchi.
  Ndani ya mjadalaujao wa Katiba kuna mambo mengi ya kujadili lakini kwa Wazanzibari hakuna lenyeumuhimu zaidi kuliko suala la Muungano. Sheria yaMabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 haikatazi kuujadili Muungano, baliinaelekeza Tume ya Katiba kuzingatia ‘misingi mikuu ya kitaifa na maadili yajamii’, ikiwemo uwepo wa Jamhuri ya Muungano.
  Ni suala laMuungano lililo muhimu kwa Wazanzibari kwa sababu ndilo suala lililowaunganishana sehemu ya pili ya Muungano na pia ndilo suala ambalo kuwekwa sawa kwakekutaleta mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi kwa Zanzibar ambapo hali hiyo katika miaka hii yaMuungano imekuwa tete na isiyotabirika.
  Kumekuwakukielezwa kuwa kuna Kero za Muungano. Kwa hakika hizo si kero bali ni matatizoyaliopo ndani ya Katiba inayoshindwa kukidhi haja za wakati na matumaini yawatu wa pande mbili za Muungano na huku Zanzibarwakihisi kwa mfumo ulivyo hivi sasa kuna haja ya kubadilisha mizania.
  Kwa kuwa Zanzibar ina Katiba yake wenyewe ambayo, kwa muundo wasasa wa Muungano ndio yenye mamlaka kuhusiana na masuala yote yaliyo ya Zanzibar ambayo si ya Muungano, na hiyo itahakikisha hajana matumaini yao.Kwa upande mwengine marekebisha katika suala la Muungano ndiko kutatoa fursakwa Wazanzibari kupata haki zao, katika Muungano zitazotolewa kwa usawa kadriilivyo kwa kujali na kujua nchi hizi ni sawa katika Muungano.
  Baraza la Katiba, kwa kujua umuhimu waWazanzibari kujadili Muungano wakati Mjadala wa Katiba utapokuwa unaendelea, limeandaakijitabu hiki kwa kutoa hoja 18 za kwanini Wazanzibari wajikite kwa nguvu zaozote kuujadili Muungano wakati wa Mjadala wa Katiba.

  Bila ya shaka zaweza kuwepo hoja nyenginenyingi ambazo wananchi kwa njia moja au nyengine wanazijua na hivyowataziongezea na hizi, ili ipatikane na isikike sauti moja juu ya namna ganiWazanzibari wanataka Muungano wa Tanzania uwe baada ya kupitishwakwa Katiba Mpya 2014.

  Kuujadili kwa kina kutawezesha kilaupungufu kuonekana na kwa hivyo kila kipengele kurekebishwa kwa kujali maslahiyao na kwa hivyo kuweza kusaidia kufikia uamuzi bora zaidi wakati wa kupigaKura ya Maoni utapofika ili kupitisha Katiba Mpya.

  Kama alivyosema Rais wa Zanzibar Dk Ali Muhammed Shein katika hotubayake ya Sherehe za Miaka 48 ya Mapinduzi, Januari 12, 2012, kuwa kila mtu atoemaoni yake kwa uwazi na uhuru na hakuna ataebughudhiwa au kudharauliwa.

  Na kwa hivyo Baraza la Katiba linatengezajukwaa kwa mjadala huo kwa upande wa Zanzibar natunataraji kuwa kila mmoja atatumia fursa atayoipata kutoa maoni yake ambayohakika kila maoni yatakuwa na uzito wake katika kutetea haki na maslahi ya Zanzibar.

  Baadhi ya hoja hizi zinatokana nauwasilishaji uliofanywa na Awadh Ali Said (Mwanasheria) katika mfululizo wamijadala iliyokuwa ikiandaliwa na Baraza la Katiba, na kuongezewa na Ally Saleh(Mwanasheria) ambaye pia ndie aliyeandika kijitabu hichi kwa niaba ya Baraza laKatiba, Zanzibar.

  KWA NINI TUUJADILI MUUNGANO

  Hoja 18 zaBaraza la Katiba, juu ya Kwa Nini Tuujadili Muungano ni hizi zifuatazo: 1. Kuundwa kwake Kuundwa kwaMuungano wa Tanzania kunaudhaifu wa kisheria kama ambavyo imeshawahi kuelezwamara kadhaa na wanasheria na wanasiasa kadhaa wa kadhaa. Ni Muungano ambaoulianzishwa kwa utashi wa viongozi wawili wa kisiasa wakiwa ni Marais wa nchimbili huru, lakini mambo ya msingi yakiwa hayajazingatiwa. Ni utaratibuunaokubalika kimataifa na kisheria hata kufuatwa na nchi za Jumuia ya Madola,ambazo kwa kuwa Zanzibar na Tanganyika zote zilikuwa kwa njia moja au nyenginechini ya Himaya ya Uingereza, kwamba viongozi wakuu wa nchi wanaweza kuingiaMikataba ya Kimataifa kwa niaba ya nchi zao.Hivyo viongozi wakuu wawili maraisAman abeid Karume na Julius Nyerere wakaingia mkataba wa kuunganisha nchi zao Utiaji huo wasaini ulishuhudiwa na viongozi kadhaa wa kila upande wakiwamo kwa upande waZanzibar Ali Mwinyigogo, Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na kwa upande wa Tanganyikawalikuwepo akina Ali Mwinyi Tambwe, Bhoke Munanka na Osca Kambona. Utiaji saini wa Mkataba wa Muunganohaukuhalalisha kukubaliwa na kuridhiwa kwa Muungano na watu wa Zanzibar. Na ndipo RaisAbeid Amani Karume wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar akaingia mkataba na RaisJulius Nyerere wa Serikali ya Tanganyika, lakini ilikuwa lazima hatua hiyoifuatiwe na ile ya kuridhia Mkataba huo, na Mabunge ya nchi zao - hili nisharti kwa mujibu wa mfumo wa kisheria, lakini pia lilifanywa ni sharti ndaniya Mkataba wa Muungano, (Kifungu cha 8) ambacho kilisema wazi kuwa baada yakusainiwa na viongozi hao Mkataba huo ulilazimika upate ridhaa ya mabunge yanchi zao. Upande wa Tanganyika ulitimiza sharti hilo kwa kupitishwa Sheria Namba 22, 1964,ambapo nakala kivuli ya Mkataba wa Muungano iliambatanishwa, na huku sotetunajua kuwa hadi hivi leo nakala halisi ya Mkataba wa Muungano haijaonekanahadharani. Nakala halisi yaMkataba wa Muungano imeshindwa kutolewa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,ambaye alisema katika Hati ya Kiapo kwenye kesi Namba 20, 2005 iliyofunguliwana Rashid Salim Adi na wenzake katika Mahkama kuu ya Zanzibar,kwamba Serikali ya Zanzibarhaina hati halisi ya Muungano. Bila ya shakahili ni suala sio tu la kushangaza lakini ni la aibu kwa Serikali kukosa kuwana Mkataba halisi wa kimataifa wa Muungano, na kwa hivyo si suala ambalo linafaa liendeleekufunikwa daima dawamu. Kama ambavyotumesema wakati Tanganyikailiridhia Mkataba huo Zanzibarhaikufanya hivyo jambo ambalo Rais wa Pili wa Zanzibar Aboud Jumbe katikakitabu chake cha The Partnership amesema ni mgogoro kamili wa kisheria. Zanzibar ikiwandio kwanza inatoka kwenye Mapinduzi na kusimamishwa Katiba ya Zanzibar yamwaka 1963, ilitunga Sheria iliyoitwa Legislative Powers Decree, Namba 1, 1964ambayo ilitoa mamlaka ya kutunga sheria kwa Baraza la Mapinduzi, na kwa hivyoBaraza hilo la Mapinduzi lingeweza kuwa Bunge la kuridhia Mkataba wa Kimataifauliokuwa umetiwa saini baina ya Karume na Nyerere na sharti hilo likiwa limetajwakwenye Mkataba wenyewe. Lakini watuwaliokuwa na dhamana ndani ya Serikali wakati huo pamoja na Jumbe wamesemaBaraza la Mapinduzi halikuridhia Mkataba huo. Ikumbukwe wakati huo Baraza laMapinduzi lilikuwa na mamlaka ya kikatiba ya kutunga sheria. WolfgangDourado, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwa wakati huo, kauli yake nihiyo hiyo na zaidi ananukuliwa akisema hivyo katika Mkutano wa Chama chaWanasheria wa Tanganyika (TLS) 1985, naaliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi kwa wakati huo, Salim Rashidamesema katika Hati ya Kiapo kwenye kesi ya Rashid Salim Adi na Wenzake kuwaMkataba wa Muungano haukuridhiwa na Baraza la Mapinduzi. Halafu pia msomianaeheshimika katika uwanja wa Katiba, Professa Issa Shivji amethibitishakupitia vitabu vyake viwili kile cha 1990 Legal Foundations of the Union ofTanganyika and Zanzibar na kile cha 2008 Pan-Africanism or Pragmatism. Lessons of the Tanganyika-Zanzibar Union kuwa hakuna pahala popote pale ambapo Mkataba wa Muungano inaonyeshaumeridhiwa na mdau wa pili yaani Zanzibar. Ila bila yashaka hoja inakuja kuwa hakuna ambae amechukua hatua moja mbele ya kusailiuhalali wa Muungano ambao unakosa sifa muhimu na awali kabisa ya kuridhiwa autuseme kwa usahihi zaidi kukosa kuridhiwa na upande mmoja na kwa hivyoukaruhusiwa kusonga mbele hadi leo. Na hio kwawakati huu ndio sababu muhimu ya kujadili Muungano, maana kama sharti muhimu hilo halikutimizwa ina maana kila kilichofuatia kinakosauhalali wa kisheria na wakati huu tukijadli kuja kwa Katiba Mpya hilo lazima liwe mbelekwenye ajenda. 2. Uhalali wa Muungano Muungano wowoteule hauwezi kusimama kwa matakwa ya viongozi tu kama ambavyo ilivyotokea katikaMuungano huu wa Tanzaniaambapo matakwa ya kisiasa ya Rais Abeid Karume na ya Rais Julius Nyerereyalikuwa ndio mbele. Matakwa yaviongozi si lazima yawe ni matakwa ya wananchi, kamaambavyo imeonekana sehemu nyengine nyingi ziliozoungana, ambapo juhudi zakuunganisha hazikuweza kusimama kwa sababu ya kukosa uhalali unaotokana nawananchi. Na ndivyo piainavyotokezea hapa kwetu hata baada ya miongo kadhaa, kupewa nguvu za kisheria,kubebwa kisiasa lakini kutokana na kukosekana kwa uhalali wa umma, Muunganohaujasimama kama ambavyo ingepaswa kuwa nakujivunia na kila mwananchi. Uhalali wa ummaunatokana na kuulizwa wananchi juu ya Muungano ambao sio tu utawahusu lakinipia utakuwa wao na kama ambavyo ilitajwa katika Mkataba wa Muungano kama hilolingefanywa mwaka mmoja baada ya Mkataba wa Muungano wa 1964. Sharti hilo la Mkataba wa Muunganolilizimwa na Rais Julius Nyerere wakati alipopitisha sheria ambayo alijipamadaraka ya kuahirisha kwa muda usiojulikana. Utaratibu ulikuwa umepangwa ndaniya Mkataba wa Muungano kuwepo kwa umma kuulizwa matakwa yao juu ya kuendelea au kutoendelea kwa Muunganohuo, lakini pia ingekuwa ndio njia ya kuupa uhalali Muungano wenyewe. Suala la uhalalikupitia sauti ya umma ni la muhimu katika kutekeleza matakwa ya demokrasia namara zote hufanyika kwa njia ya kuwepo Kura ya Maoni, ambapo mwananchi mmojammoja hutoa sauti yake na sharti hilola Kikatiba lilipaswa kutekelezwa. Wenzetu hivisasa wamepiga hatua kuuliza wananchi wao katika masuala mbali mbali ili kupatauhalali wa jambo lenye kugusa maslahi ya umma na ambalo uamuzi wake utajengaumoja baina yaobadala ya kuwagawa. Tumesikia nchizimefika hata kuwauliza wananchi wake juu ya vazi la Hijab kwamba livaliwehadharani au la, na hatimae sauti ya umma kupatiwa nguvu na sio kwa Serikalikuchukua uamuzi kivyakevyake tu. Na ndivyoilivyotokea hivi karibuni hapa kwetu pale Serikali ya Zanzibarilipoamua kupitisha Sheria ya Kura ya Maoni ya2010 ili kupata ridhaa ya wananchi kuundwa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja waKitaifa na kuridhiwa na umma kwa asilimia 66.4 Kwa kupata sautihiyo ya umma hata wale ambao walikataa kwa kupiga kura ya Hapana kwa asilimia33.6 lakini wamejua kuwa wameshindwa na wingi wa watu na sio kuburuzwa na kwahivyo kwa hali nyingi wameridhia kuwa na sauti ya umma na kwa hivyo kuimarishauhalali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa. Kwa hilolimeshindwa kufanyika, na kwa maana hiyo wananchi hawakuulizwa na hivyokutopatikana uhalali, basi ni sababu nyengine nzuri ya kwa nini tuujadiliMuungano ili pengine hatimae wananchi waulizwe kuukubali au kuukataa kwao kamaambavyo Mkataba wa Muungano ulielekeza na kudharauliwa na viongozi kwa miakayote. 3. Kutokuwepo utaratibu waupitiaji Muungano waTanzania umekosa utaratibu wa kisheria na kikatiba wa kufanyiwa mapitizi kamaambavyo ingepaswa kuwa ili kuulinda usichushe, usipitwe na wakati na usielemewena makosa ya kiutendaji na kisiasa. Kumekuwa navikao vingi vinavyofanyika na kamati nyingi zilizoundwa kuanzia za Waziri Mkuuna Waziri Kiongozi, Waziri Mkuu na Makamo wa Pili wa Rais na hata za wizara kwawizara kujadili zile ambazo zimekuwa zikiitwa kuwa ni matatizo au kero zaMuungano. Sababu kubwa yakuzuka vikao ni pale panapotoka matamshi kutoka upande mmoja wa Muungano ambayoyatatikisa taifa, basi huwa kama kutoka kwenyelepe la usingizi na kuitisha kikao cha kero za Muungano Hata palemaamuzi yanapofanywa kupitia vikao hivyo lakini utekelezaji wake umekuwaukishindikana kwa sababu vikao vyenye kufanya maamuzi hayo havina nguvu yakikatiba na kwa hivyo si vya lazima na haviwezi kulazimisha taasisi yoyote ilekutekeleza maamuzi yake zaidi ya kushawishi tu. Kwa hivyoimegeuka kuwa ni dasturi kwa watendaji kuamua kuheshimu maamuzi wanayotaka nakuyapuuza wasioyataka na wakijua hakuna litatakalokuwa kwa kufanya hivyo maanahakuna nguvu za kuwalazimisha. Imefika hadiRais Jakaya Kikwete akisema kuwa vikao hivyo ni muhimu kuwepo japo kuwa watuwasiwe na la kuzungumza lakini basi angalau wakutane kuwa kunywa chai kwapamoja. Na hilokwa hakika ni kuufanyia istihizai umuhimu wa pande za Muungano kuwa na wajibuwa kikatiba wa kukutana. AliyekuwaKiongozi wa Umoja wa Ulaya hapa Tanzania,Tim Clark aliiambia semina moja ya uongozi iliyofanyika huko Ngurudoto hakunakitu kilichoimarisha Umoja wa Ulaya (EU) kamakuwepo na utaratibu wa kuupitia Mkataba wa Umoja huo kila baada ya muda nakugundua makosa, ukwamaji au matatizo mapya mapema kabisa. Kutokuwepo kwavifungu vyenye muelekeo huo katika Katiba ya Tanzania ni sababu nzuri sana yakuujadili Muungano huo, ambao kwa kawaida lazima utazua matatizo ya kisiasa nakiutekelezaji ambayo lazima yapitiwe kwa wakati na sio kungoja mpakayamekusanyana na kuzua suitafahamu na mivutano. 4. Kero za Muungano Moja katikamsamiati ambao umepata maana na mtizamo mpya ni ule wa neno Kero. Neno hililimekuwa maarufu mno katika muktadha wa Muungano lakini haionekani kuwa namaana iliyozama bali linatumika kwa njia ya kueleaelea. Neno hililinatumiwa kuonesha mambo ambayo wadau wa Muungano (Zanzibarna Tanganyika) yanawakanganya,yanawasumbua na yanaleta mivutano baina yaona hasa katika suala la utekelezaji. Kwa kiasikikubwa Kero hizo zinakuja kwa sababu ya utata katika muundo wa Muunganowenyewe, muundo ambao unakataza maamuzi mengi kufanywa kwa sababu ya udhaifu wakimsingi. Kwa hakika hicho kinachoitwa Kero ingefaa ukaitwa ni utata. Muundo waMuungano wa Tanzaniaunatajwa kuwa ni maalum kwa sababu hakuna pengine popote duniani ambapo nchimbili zimeungana na Muungano huo ukawa ni wa utaratibu wa Mamlaka mbili ndaniya taifa moja. Tena mamlakahizo mbili moja ikiwa na mamlaka kamilifu au timilifu (Serikali ya Jamhuri yaMuungano) juu ya nchi zote mbili na moja ikiwa na mamlaka nusu juu ya eneo laupande mmoja wa Muungano (Serikali ya Zanzibar),lakini wakati huo mshirika mmoja wa Muungano (Tanganyika) akiwa ndani au chini yaMamlaka hiyo timilifu. Rais wa pili waZanzibar Alhaj Aboud Jumbe aliona hilo si sahihina alipothubutu kulisema hilo likamgharimumaisha yake ya kisiasa, lakini iko katika rekodi kwenye kitabu chake cha ThePartnership kwamba Muungano ambao ungepaswa kuwepo Tanzaniani wa Mamlaka Tatu yaani Zanzibar, Tanganyika naJamhuri ya Muungano. Muundo ulioposasa na ambao umeanza kutumika toka 1964 ulipaswa kuwa wa muda tu na sio wakudumu kama ambavyo umefanywa kuwa na kwahivyo kuwa chanzo cha hizo zinazoitwa Kero ambazo uhalisi wake ni Utata. Kwa muundoulivyo inaonekana kama kwamba Muungano huu umesimama katika msingi wa kwamba Zanzibar ilisalimu Mambo 11 katika Muungano ambayoyalifanywa kuwa ni ya Muungano, na mengine yote yaliobakia yalifanywa kuwa niya Zanzibar nakwa hivyo chini ya Mamlaka yake. Kwa muelekeo huohuo kumekuwa na dhana potofu kuwa Tanganyikanayo imefanya hivyo hivyo na kwa maana hiyo kama ilivyopoteza kiasi fulani chamamlaka fulani Zanzibar basi nayo Tanganyikapia ilisalimu madaraka yake ndani ya Muungano. Lakini ukweli nikuwa Tanganyika haikusalimuchochote kile katika Muungano kinyume na Zanzibarambayo imesalimisha Mambo 11. Tanganyikahaikusalimisha kwa sababu kama ingesalimutungejua mambo ambayo imechangia katika Muungano. Kwa kubakia namambo yake yote lakini pia kuwa msimamizi wa Mambo 11 ya Muungano na sasa Mambo22 ya Muungano, Tanganyika haikupoteza kitu ilazaidi imefaidika katika Muungano huu. Imebakia na mambo yake yote na juu yakeinasimamia Mambo ya Muungano. Na ndipo utatampaka leo unakuja panapotokea suala kuhusu mambo ambayo si ya Muungano naambayo yapo Tanganyika na Zanzibar, ambapo tabaan Serikali ya Muungano inavutiaupande wa Tanganyika zaidikuliko upande wa Zanzibar. Ila lililotokeani kuwa baada ya Zanzibar kusalimu Mambo 11 ndani ya Muungano, Tanganyikailijigeuza jina na umbo na kujiita Tanzania na ikayachukua mambo ambayoZanzibar imesalimu ndani ya Muungano pamoja na yake wenyewe na kugeuzwa kwapamoja kuwa ni ya Jamhuri ya Muungano ambapo jina ambalo lilikubaliwa litumikeni lile la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Jina hili nimuhimu kwa sababu lilitoa taswira halisi na ambayo ingekuwa ni endelevu kuwanchi zilizomo katika Muungano huu ni zile za Zanzibar na Tanganyika, lakini kwakubadilishwa jina na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiko kunakoletautata hivi sasa pindi Zanzibar ikidai kuwa bado ipo kama Zanzibar hata iwapoimo ndani ya Jamhuri ya Muungano.
  Utata ukazidikuwa mkubwa kulipoanza kufanyika mabadiliko ya majina halisi ya nchi za Tanganyika na Zanzibar, washirika wawili wa Muungano nakuanza kuitwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar au Tanzania Visiwani ambapohili linaonekana linapeleka zaidi kuua Uzanzibari.
  Kwa hali hiyowakati nchi ikielekea katika mjadala wa Katiba Mpya hii ni sababu tosha kuwakuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mjadala kuhusu Muungano
  5. Mgawano wa Madaraka

  Hakuna katika Katiba ya Jamhuri ya Muunganovipengele au kipengele kinachoweka masharti juu ya mgawano wa madaraka nakukosekana kwa hilo kumekuwa ni chanzo chamalalamiko makubwa juu ya namna madaraka yanavyotolewa au kupewa kwa mtu, aweni wa upande wa Tanganyikaau Zanzibar.

  Kukosekana kwa vipengele hivyo, na badalayake kumpa mamlaka yasio na kikomo Rais wa Tanzania, kumeondosha sio tu iledhamira ya kuwa nchi hizi zimeungana kuwa ni sawa, lakini pia uwezekano wakuendelea na Muungano huku sio tu zikiamini kuwa ni sawa lakini zitaendeleakuwa sawa.

  Ndani ya muundo wa Serikali ya Muunganokuwemo kwa Wazanzibari ni jambo la hiari tu ya Rais wa Muungano na kwa hivyokushirikishwa katika Serikali ya Muungano huwa ni suala la kualikwa tu namwenye mamlaka ya kualika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa kuwa hakuna maelekezo ya kikatiba,Serikali ya Jamhuri ya Muungano haiundwi kimizania wala kieneo au kiuwakilishi ilani jinsi ambavyo Rais anavyotaka au anavyoona na hilo lina ushahidi wa kutosha.

  Wakati wa kuundwa kwa Muungano ambapo Mamboya Muungano yalikuwa ni 11, Rais Nyerere alichagua Mawaziri 5 kutoka upande waZanzibar ambao walikuwa ni Abdularahman Babu, Kassim Hanga, Abdulaziz Twala,Hassan Nassor Moyo na Idriss Abdul Wakil.

  Hivi sasa ambapo Mambo ya Muungano ni 22basi Mawaziri wa Zanzibarndani ya Serikali ya Muungano ni 4 nao ni Professa Makame Mbarawa Mnyaa, SamiaSuluhu, Dk Hussein Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha na manaibu mawaziri.

  Ubaya au tatizo ni kuwa baadhi ya Wizarahuundwa huku zikiwa zinaingia katika mambo ambayo yametengwa kuwa ni ya Zanzibar na kwa hivyo kuleta utata kwa kuingilia Wizaraziliopo Zanzibarau kuteuliwa Mzanzibari kusimamia Wizara ambayo ndani yake kuna jambo ambalokikatiba halimuhusu.

  Kwa mfano uwepo wa Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa wakati kuna Jeshi la Kujenga Uchumi kwa upande waZanzibar; uwepo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo inajumuisha Magereza wakatikwa upande wa Zanzibar kuna Vyuo vya Mafunzo na pia uwepo wa Wizara ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo Ushirikiano wa Kimataifa si suala laMuungano.

  Mfano mzuri wa namna ambavyo madarakayanaweza kugawanwa na hilo kueleweka na wadau mapema umetolewa katikaMabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzbiar chini ya Aya ya 42 (2) ambapoumetandikwa utaratibu wa mgawano wa madaraka baada ya Uchaguzi Zanzibar nautaratibu huo ukafuatwa kikamilifu na ndipo kuja Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

  6. Nafasi ya Urais

  Urais ndio alamakubwa ya Muungano. Urais unashika nguvu zote za dola na kwa hivyo Mtanzaniaanaekuwa Rais ndiye mwenye amri ya mwisho katika uteuzi, kutangaza vita na haliya hatari, kumaliza maisha ya Mtanzania, kumsamehe kifungo chake nk. Rais kwa mujibuwa Katiba hapaswi kufuata ushauri wowote ule.

  Nafasi ya Uraishugombewa, lakini sivyo ilivyokuwa hapo mwanzo kabisa ambapo Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania alikuwa kwa njia ya makubaliano chini ya Mkataba waMuungano, ambapo Makamo wa Rais alikuwa akitoka Zanzibar moja kwa moja.

  Kwa mujibu waMkataba wa Muungano hiyo ilikuwa ni mipango ya muda na ilikuwa wananchiwaulizwe, kwa njia ya Kura ya Maoni au nyengine yoyote ambayo ingefaa, mwaka uliofuata yaani 1965, lakini tunajuakuwa Rais Julius Nyerere alisogeza au aliindoa fursa hiyo kwa muda usiojulikanana Kura ya Maoni hiyo haikufanyika tena.

  Kuanzia mwaka1970 Wazanzibari wakaanza kushirikikatika chaguzi za Tanzania kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano huku Makamo waRais akiwa moja kwa moja ni Rais wa Zanzibar , kama Mkataba wa Muunganounavyoeleza.

  Kupiga kura kwaWazanzibari katika uchaguzi wa Rais wa Tanzania kuanzia 1970 hadi 1990 hapakuwana athari yoyote kwa sababu idadi ya Wazanzibari wote ni sehemu ndogo tu yawapiga kura wote wa Tanzania na kwa kuwa kura ya Rais wa Jamhuri wa Muungano waTanzania ni jimbo moja tu la uchaguzi, matokeo ya aina yoyote ya Zanzibarhayangeweza kuathiri taswira ya Urais wa Muungano.

  Lakini iwapokungekua na kifungu cha Katiba kinachotaka idadi fulani ya wapiga kura waZanzibar waridhie Urais wa Muungano pengine hali ingekuwa ni nyengine, lakinikwa muda wote ridhaa ya Wazanzibari katika nafasi hii imekuwa haitakiwi kwanjia ya kura na kisanduku.

  Urais wa Tanzaniaulishikiliwa na Julius Nyerere kutoka 1964 hadi 1985, wakati Ali Hassan Mwinyiakiwa ni Mzanzibari aliposhika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 10 na kuanzia hapoBenjamin Mkapa amekaa miaka 10 na Jakaya Mrisho Kikwete yupo katika kipindichake cha pili kutimiza miaka 10.

  Ilikuwa ni mwaka1995 wakati mfumo mpya wa Mgombea Mwenza ulipoanzishwa sambamba na kusimamishwamfumo wa vyama vingi vya siasa na kuanzia hapo imekuwa ni lazima Mgombea Uraisawe na Mgombea Mwenza kutoka upande tofuati wa Tanzania anaotoka yeye Rais.

  Kuna mifano mingiya nchi zilizoungana ambapo nafasi ya Urais imekuwa ikizunguka ili kuonyeshaushiriki wa sehemu nyengine katika Muungano lakini pia kutoa fursa sawa zakushika nafasi hiyo na sio upande mmoja kuishika kwa ajili ya wingi wake wawapiga kura.

  Hii ni sababumoja ya kujadili Muungano ambapo fikra mpya zinaweza kuja juu ya namna yakupata kiongozi wa nchi ambapo si lazima atokane na kura za wananchi moja kwamoja, kadri ambavyo mapendekezo yatavyoweza kutolewa wakati wa Mjadala waKatiba.

  7. Orodha ya Mambo ya Muungano

  Orodha ya Mamboya Muungano kwa hali ilivyo sasa hakuna ambaye anaijua. Baadhi ya wataalamuwamekuwa wakitaja idadi inayotofautiana kwa mujibu wa unyumbuaji wa mambo hayokutokana na orodha ya Mambo 22 yaliyondani ya Katiba hivi sasa ambapo awali kabisa yalikuwa ni Mambo 11 kwa mujibuwa Mkataba wa Muungano.

  Dhana yakuimarisha Muungano siku zote imekuwa ni kumega mambo kutoka mamlaka yaZanzibar na kuyatia katika Muungano, kwa maana nyengine ni kuongeza nguvu zaMuungano nakuidhoofisha Zanzibar ndikomaana halisi za kuimairisha Muungano.

  Katika umegajihuo Zanzibar imebakia hivi sasa gamba tupu kwa sababu mambo yaliotiwa katikaOrodha ya Mambo ya Muungano ni yale ambayo ndio ya msingi kuiwezesha nchikusimama na kukosekana kwayo basi nchi hunywea na Zanzibar imenywea kiuchumikwa kuondoshwa mambo hayo kutoka milki yake.

  Hata pale ambapoZanzibar imejaribu kusimamia mamlaka yake ambayo kwa makosa yametiwa katikaOrodha ya Mambo ya Muungano kama suala la Ushirikiano wa Kimataifa, kupitiajuhudi za kutaka kujiunga na Jumuia ya Kiislamu ya OIC hapo mwaka 1992, Rais waZanzibar Dk Salmin Amour alinyamazishwa.

  Jamhuri yaMuungano ilitoa ahadi kujiunga na OIC kama Tanzania na sio kuiachia Zanzibarpeke yake, lakini hilo hadi sasa halijaweza kufanyika.

  Hali ya Zanzibarkukosa sifa ya kimataifa na hivyo kushindwa kujiunga na taasisi kama Shirika laSoka Duniani FIFA na mifano ambayo kila mara inakumbusha jinsi Zanzibarilivyosalimisha mamlaka yake hayo ndani ya Muungano.

  Kutoka Mambo 11ya Muungano sasa yapo Mambo 22 ya Muungano na suala kuu hapa linalokuja ni jeeuongezwaji wa mambo hayo yametimiza masharti ya uhalali mbali ya kwambayamekuwa yakipitishwa na Bunge?

  Muda mwingiimekuwa ikitolewa hoja kuwa Zanzibar imepoteza sifa ya kuwa dola na kukosa mamlakaya kujiunga na jumuia za kimataifa na kuingia mikataba ya kimataifa na ambapoinaeleweka kuwa Muungano wa Tanzania uliundwa kwa misingi hiyo na wakati huoZanzibar ilikuwa na mamlaka hayo, na kutokana na mamlaka hayo ndipoikasalimisha katika Muungano orodha ya Mambo 11 ya Muungano.

  Hoja tunayotakakutoa hapa ni kuwa kama Zanzibar ilishapoteza mamlaka yake ya kimataifa nakuingia kwenye mikataba ya kimataifa, sasa imewezekana vipi Zanzibar kutoamambo yalio ndani ya mamlaka yake na kuyatia katika orodha ya Muungano, ilhalihaina tena nguvu hizo?

  Kwa hivyo katikamambo yalioyoongezwa likiwemo suala la Mafuta kwa Sheria No 48, 1968 na mengineyote yaliofuatia hayana na hayawezi kuwa na uhalali kwa sababu utaratibu wakuchukua mamlaka hayo kutoka Zanzibar haungetosha tu kwa kupitisha sheria yaBunge bali kurudi kwa Zanzibar wenyewe kutaka ridhaa yake, jambo ambalohalikufanywa kwa sababu ya kukosekana utaratibu wa kufanya hivyo ndani yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano.

  Uvurugaji waMambo ya Muungano unaonekana pia katika suala la Makamo wa Rais wa Jamhuri yaMuungano katika Mkataba wa Muungano ambapo ametajwa kwa jina kuwa angekuwa Raiswa Zanzibar Abeid Amani Karume. Na akatumikia nafasi hiyo Aboud Jumbe na AliHassan Mwinyi, bila ya mabadiliko katika Mkataba wa Muungano ambao ulimtajaRais Abeid Karume kwa jina.

  Katika kipindicha 1985-1995 ambapo Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa madarakani kwenye nafasi yaUrais wa Tanzania, Zanzibar haikutoa Makamo wa Rais.

  Mabadiliko yakumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Tanzania yalifanywa kikatibamwaka 1992 wakati Tanzania ilipoingia katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 ambapo mfumowa Mgombea Mwenza ulianzishwa kwa kila chama kutakiwa kuwa na Mgombea Mwenzaanaetoka pande tofauti na Mgombea Urais wa kila chama.

  Mabadiliko hayoyanakosa uhalali wa kisiasa kwa sababu ile ile ambayo tumeitoa hapo juu kwambakama kulikuwa na haja ya kufanya mabadiliko ya msingi kama hayo ilipaswa kurudikatika Mkataba wa Muungano.

  Lakini pilikumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais ni kuvunja msingi muhimu waMuungano na pia ni kuondosha kiungo cha muhimu na lazima cha Zanzibar katikaMuungano ambapo hivi sasa Makamo Rais wa Tanzania anaechaguliwa kwa njia yaMgombea Mwenza hana uhusiano wowote na Mfumo wa Kiserikali wa Zanzibar.

  Cha muhimu pia nikuwa Makamo wa Rais wa Tanzania hana uhalali wa moja kwa moja wa kisiasa nabaraka za Wazanzibari kwa sababu hakupigiwa kura na hivyo hawezi kuwa sauti yaokatika jambo lolote la Muungano kwa sababu hakuwa na sera zozote juu ya Zanzibarambazo ametumwa na Wazanzibari akazisimamia. Kosa kubwa ambalo limefanyika nalinaendelea kufanyika ni kutouheshimu Mkataba wa Muungano, na badala yake kuipamamlaka katiba ambayo pia inautata kwa kukosa uhalali katika uundaji wake.

  Hii pia ni sababumuhimu sana ya suala la Muungano kujadiliwa kwa undani wakati wa Mjadala waKatiba utakapokuwa unaendelea.

  8. Mgongano wa Maslahi

  Kwa sehemu kubwaMuungano wowote ule wa nchi mbili au zaidi huwa unalalia katika sehemu kubwakwenye mambo ya kiuchumi kuliko yale ya kisiasa. Hasa hali huzidi iwapo,Muungano wenyewe umeendelea kuzibakisha nchi kusimamia mambo yake ya ndani.

  Ila hataMarekani, ambako Muungano wake ni tofauti na ambao ndani unaishia katikakiwango cha majimbo yaani States, ambapo majimbo hayo yanajisimamia wenyewe kwasehemu kubwa, mipaka ya kiuchumi imekuwa ya umuhimu sana kuweza kuulinda nakuendeleza umoja wa nchi hiyo.

  Ni hatari kabisakukosekana kueleweka mipaka ya kiuchumi ya kila sehemu kwani kwa kuwepo udhaifuhuo ndipo ambapo kunatokea mgongano wa kimaslahi, kwa kila upande kuvutiakwake.

  Muungano waTanzania kwa kiasi kikubwa umeshindwa kutengeneza mipaka hiyo ya kiuchumi bainaya pande mbili za Muungano, lakini umeshindwa kutambua uwepo wa Uchumi waVisiwa unaoistahikia Zanzibar na baya zaidi kuruhusu kuwepo na uchumiunaoshindana (Competitive) badala ya ule unaoungana mkono (Complementary) baina ya Tanzania Bara naZanzibar.

  Mara kadhaaimejitokeza pande hizi za Muungano kugombea vyanzo vile vile vya mapato na niwazi kuwa Zanzibar ilikuja kuona umuhimu baadae wa kuanzisha Mamlaka yake yaMapato ZRB ili kuviwahi vyanzo vya visije vikajumuishwa katika orodha ya vyanzovya Muungano.

  Mgongano waMaslahi umepelekea kuweko utonzaji kodi mara mbili (Double taxation) kwa bidhaazinazotoka nje ambazo zinapitia Zanzibar ambapo kwa hakika ili kuwezakushindana haitawezekana Zanzibar iwe na viwango sawa na Dar es salaam kwabidhaa zinazotoka nje na baadae kuingia Tanzania Bara.

  Wakati piainaeleweka kuwa Uchumi wa Visiwa hustawi katika kuwepo kwa sehemu zilizotengwakiuchumi (Exclusive Economic Zones), basi pia Tanzania Bara imeanzisha maeneokama hayo katika mwambao wa Bahari ya Hindi na kwa hivyo kutarajiwa kuwa naushindani na Zanzibar.

  Haya ni mamboambayo yanashawishi haja ya kujadili Muungano wa Tanzania kuelekea kwenyekutafuta Katiba Mpya ya nchi hii.

  9. Matumizi ya Muungano

  Kumekuwa namaneno mengi juu ya suala la matumizi ya Mambo ya Muungano. Na kwa mtizamo wamacho kuonekana kana kwamba Zanzibar haichangii katika Mambo ya Muungano namzigo wote kubebwa na Serikali ya Muungano, na kwa mnasaba huo huo kuonekana unabebwana Tanzania Bara.

  Miaka 50 kuelekeaMuungano, kumekuwa hakuna mchanganuo wa ipi ni gharama ya Mambo ya Muungano naipi ni gharama ya mambo ya Tanzania Bara na hivyo kuchanganywa kwa jumla,ilhali hilo likiwa si halali kikatiba. Hivyo, Muungano huu ni wa chungwa tatu katika mikobamiwili, inamaana mkoba mmoja ambao ni serikali ya Muungano umebeba chungwambili (Muungano na Tanganyika) na ya Zanzibar chungwa moja ambayo ni Zanzibar.

  Inaeleweka kabisakuwa kuna maeneo ya kiuchumi ya Muungano ambayo fedha zake zinapaswa zigawiwebaina ya pande mbili za Muungano, kwa sasa kwa mujibu wa utaratibu uliopo, ilikutenganisha ni kipi kinatumika wapi, jambo ambalo halifanyiki kwa sasa, nahiyo ndio hoja ya Zanzibar kuwa inachangia uendeshaji wa Muungano kwa kuwa wanasehemu kwenye vyanzo vya kiuchumi vya Muungano.

  Hali hiiinaifanya Zanzibar iamini kuwa upande wa pili unafaidi zaidi faida za kiuchumiza Muungano, ilhali upande wa Zanzibar haujui wala haujawahi kujulishwa juu yamapato yanayokusanywa kutoka vyanzo vya Muungano na kabisa haijawahi kutokeajuu ya matumizi yake.

  Kwa kujua kuwakutazuka masuala kuhusu Matumizi ya Muungano ndipo Katiba ya Tanzania imewekakifungu cha kuundwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Muungano, ambayo hadi hivi sasaimeshindikana kuundwa.

  10. Zanzibar Nchi si Nchi

  Hii ilikuwa nihoja kubwa baada ya matamshi ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda mwaka2008 aliposema katika masuala ya papo kwa papo katika Bunge la Jamhuri yaMuungano kuwa Zanzibar si Nchi na kupelekea mvutano mkubwa baina ya pande hizishiriki kwenye Muungano wa Tanzania.

  Hoja ya Pindaimejengwa katika dhana ya kimataifa kuwa panapotokea muungano na nchi kuingiakatika mkataba wa kimataifa na kusalimisha mamlaka yake, basi nchi hiyohupoteza sifa ya kuwa nchi mbele ya macho ya kimataifa, na hubaki kuwa nchindani ya hayo makubaliano mapya, kama hivyo ndivyo ilivyo.

  Kwa upande waZanzibar hoja hii haionekani kuwa na uzito kwa sababu katika makubalianoyaliopo ya Muungano wa Tanzania, basi Zanzibar inaendelea kuwa na kila sifa yakuwa nchi kama vile kuwa na mfumo kamili wa Mahakama, chombo cha kutunga sheriayaani Baraza la Wawakilishi. Na pia mamlaka ya Urais.

  Kwa mujibu waSheria ya Kimataifa nchi huitwa nchi iwapo ina eneo, ina watu wake, inaSerikali na ina uwezo wa kuingia mikataba ya kimataifa. Ni haya mamlaka ya mwisho ambayo Zanzibar hainana ambayo imeyasalimisha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  Hata hivyo, hojahii pia inapanguliwa na Zanzibar ambayo inasema kuwa bado Zanzibar inapaswakuwa na nguvu hiyo kwa vile suala la Ushirikiano wa Kimataifa lilotiwa katika Mambo ya Muungano limetiwa kinyemelana ndio sababu iliyoipelekea Zanzibar kujaribu kuingia katika Jumuia yaKimataifa ya Kiislamu OIC 1992 na kulazimishwa kujitoa na Serikali ya Muungano.

  Pia ni hoja yaZanzibar kuwa Serikali ya Muungano kwa mamlaka iliyonayo na kuingia mikataba yakimataifa haifanyi uzingatifu wa kutosha juu ya haki na mahitaji ya Zanzibarkwa vile kuna baadhi ya maeneo yanaihusu Zanzibar zaidi kuliko upande wa piliwa Muungano, ambao inaonekana dhahiri Serikali ya Muungano ndio inaousimamiazaidi katika picha ya kimataifa.

  Kwa kujaribukukabiliana na hali hiyo Zanzibar ilifanya Mabadiliko ya 10 ya Katiba yaZanzibar mwaka 2010 ambapo kifungu kiliingizwa ambacho kinaweka wazi kuwaZanzibar ni nchi na ni moja ya nchi mbili ambazo zinaunda Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

  Kuwepo kwakifungu hiki bila ya shaka kunalazimisha msimamo wa Zanzibar kwamba pamoja nakuingia katika Muungano bado Zanzibar inabakia kuwa ni nchi kamili ndani yaMuungano na kama ni nchi kamili inapaswa kupata kila lenye kustahikiakupatikana na nchi.

  11. Tawala zaMikoa

  Kuwepo kwa dhana ya Tanzania ni nchi moja kulipelekea kuingizwakifungu kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano, kwamba Rais wa Tanzania ndieataegawa nchi katika maeneo ya kimikoa na tabaan kiwilaya.

  Lakini zaidi ya mamlaka hayo, kila upandeumekuwa ukiendelea kusimamia suala la Utawala wa Kimikoa kwa vile haijawahikutokea Rais wa Tanzania kuchagua wakuu wa Mikoa wa Zanzibar japo kulikuwa nasharti la kikatiba kwa Zanzibar huko nyuma kwa Rais wa Zanzibar huchagua Wakuuwa Mikoa kwa kushauriana na Rais wa Tanzania.

  Dhana hii ya ugawaji wa Mikoa na uteuzi waWakuu wa Mikoa imekuwa yenye utata katika katiba zetu mbali mbali kuanzia ileya 1977 ya Jamhuri ya Muungano, Katiba ya Zanzibar ya 1979, na baadae piaKatiba ya Zanzibar ya 1984 ambayo mamlaka hayo yalikiriwa, lakini wengi wakiwahawaelewi wakati huo ulikuwa ni Mfumo wa Chama Kimoja na ambapo Wakuu hao waMikoa walikuwa na uhusiano moja kwa moja na Chama kilichokuwa kikitawala.

  Mabadiliko ya 2010 ya kurudisha nguvu zaugawaji wa maeneo na uteuzi wa Wakuu wa Mikoa yamelazimishwa pia na uhalisi wamambo ambapo haitakiwi tena Wakuu wa Mikoa kuwa na fungamano na vyama vyasiasa.

  Kwa hali ilivyo hivi sasa dhana nzima yautawala katika Tawala za Mikoa baina ya pande hizi mbili haifanani na hilo ni moja ya sababu muhimu ya Muungano wa Tanzania kujadiliwaili kujua pande hizi mbili zinaishia wapi katika uhusiano wao kwenye sekta hiiya Tawala za Mikoa.

  Ieleweke kuwa suala la Tawala za Mikoa sila Muungano ambapo kila upande unaendesha mfumo wake wenyewe, na ambaounatofautiana kwa kiasi kikubwa.

  12. Mambo ya Zanzibar ndani ya Katibaya Muungano

  Kulizuka mjadala mkali mara baada ya Zanzibar kufanyaMabadiliko ya Katiba ya 2010 na ambapo baadhi ya wanasiasa na wanasheriawalisema yamefanywa kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ni haramu na hayawezikukubalika.

  Kubwa zaidi imeelezwa kuwa Mabadiliko ya 10ya Katiba ya Zanzibar yanatishia kuvunjaMuungano wa Tanzania kwavile yanakinzana na misingi ya Muungano wenyewe na kutaka Zanzibar ichukuliwe hatua kwa kitendo hicho.

  Zanzibar haijawahi kusalimisha Wimbo waTaifa toka siku ya awali ya Muungano baina yake na Tanganyika; kwa muundo wakeimendelea kuwa na Vikosi Maalum kwa muda wote wa Muungano na Zanzibarimerudisha Bendera yake baada ya kuipoteza mwanzo wa Muungano wa 1964 bainayake na Tanganyika.

  Baadhi ya Mambo yaliotajwa hapo juuyametajwa katika Katiba ya Tanzaniakwa mfano kuwepo na Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,lakini baadhi ya mengine kama bendera ya Tanzania na Wimbo wa Taifahayakutajwa katika Katiba.

  Kwa hatua ya Zanzibarkuyaondoa masuala kama ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kugawamikoa yalizusha mvutano na sababu kubwa ni kwa vile yametajwa ndani ya Katibaya Jamhuri ya Muungano, jambo ambalo watu wengine wanadhani toka mwanzolisingepaswa kuwemo kwenye Katiba ya Muungano.

  Kuna mambo mengi mengine ambayo yasingefaakutajwa katika Katiba ya Muungano na katika Mjadala wa Katiba Mpya hatua lazimaichukuliwe kuhakikisha kuwa hilo linatizamwa ilikuzuia kuingiza ndani ya Katiba ya Muungano mambo ambayo ni ya mamlaka ya Zanzibar na ambayo Zanzibarikitaka kuyaondoa isiwe ni tatizo la kikatiba.

  13. Zanzibar na Jumuia yaAfrika Mashariki

  Jumuia ya Afrika Mashariki hivi sasa inawanachama 5, yaani Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na Tanzania na nchi ambayo hivi sasaiko njiani kuwa mwanachama ni ile ya Sudan Kusini.

  Lakini Zanzibar ingeweza kuwa mwanachama waasili, lakini hilo halikuwezekana kutokana na kuwa kikatiba ni sehemu yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa hivyo imo kwenye Jumuia hiyo kupitiamwemvuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Ila inaeleweka kabisa kuwa Muungano wa Tanzania unasimama katika Mambo ya Muunganoambapo kati ya 22 yaliyomo hivi sasa basi, Zanzibar inajisimamia wenyewe katika orodhamwengine mrefu. Na katika Mambo ya Jumuia ya Afrika Mashariki kuna mambo ambayoTanzania haiwezikuiwakilisha Zanzibarkwa sababu ni Zanzbiar ndiyo yenye miliki ya mambo hayo.

  Mambo hayo ni pamoja na Elimu, Kilimo,Biashara na mengineyo, lakini kwa hali inavyokwenda hivi sasa Serikali yaJamhuri ya Muungano imejichukulia mamlaka ya kuiwakilisha Zanzibar katika mamboyasiyo ya Muungano na kwa hivyo hili si kinyume na Katiba ya Tanzania lakiniyanafanya uwakilishi huo usiwe halali kwa kukosa msingi wa kisheria nakikatiba.

  Hali hii, kama ambavyo imejitokeza katikamasuala ya kimataifa kama vile uwakilishi katika nchi na mashirika ya kigeni,basi pia kuna utata ambapo ikitokezea maslahi ya Zanzibarna Serikali ya Muungano yakigongana ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki au piamambo ya Zanzibarkukosa kipaumbele mbele ya mambo yanayohusu Jamhuri ya Muungano.

  Mpango uliopo hivi sasa ni Zanzibarkushauriwa katika masuala ya Jamuia kupitia uwakilishi ndani ya ujumbe waJamhuri ya Muungano na kumeshindikana hadi sasa kuwa na mfumo imara wa kuipasauti Zanzibar ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki, na njia pekee ni hii yakutengeneza mazingira ya Zanzibar kujisemea wenyewe kwenye Jumuia hiyo, lasivyo siku zote Zanzibar itapunjwa hata katika haki zake.

  Njia itayowezesha Zanzibarkuwa na sauti yake si ya sasa hivi ambapo Jamhuri ya Muungano imejitwishakuyabeba ya Muungano na yasiokuwa ya Muungano; wala si Serikali tatu au moja,ila njia pekee ni kila nchi kujisimamia wenyewe kamataifa kamili ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki.

  14. Muungano mgando

  Dhana ya Muungano wa Tanzania ilikuja katika wakatiambapo kulikuwa na vuguvugu ambapo ilitarajiwa muungano wa kimaeneo baada yakuundwa kwa Umoja wa Bara la Afrika (OAU) basi ingekuwa rahisi kuwa na taifamoja la Afrika mfano wa Marekani.

  Lakini kosa la kwanza kabisa lilofanywaambalo lilikwamisha uwezekano wa nchi nyengine kujiuunga na Muungano wa Tanzaniani muundo wake kupitia Mkataba wa Muungano ambapo hapakujengwa uwezekano wanchi nyengine kujiunga.

  Pili, muundo huo ukajidhihirisha kuwa nikikwazo kwa sababu Muungano umeundwa kwa Katiba bila ya kuwa ni wa Mkataba, nakwa hivyo sio tu imekuwa haiwezekani kujitoa katika Muungano huo, lakini piaMkataba umetengenezwa bila ya kuwa na fursa za kukaribisha wanachama wengine.

  Pia Katiba imekosa kuwa na kipengele chakujitoa katika Muungano, na kwa hivyo hata iwapo Zanzibar inazuilika kutumiafursa zake, basi haiwezi kujitoa kwenye Muungano kikatiba, na huku Muunganoukibakia kuwa ni mgando kwa kukosa kuungwa mkono na wanachama wengine.

  Wakati Muungano wa Tanzania ukiwa nimgando, ule wa Jumuia ya Afrika Mashariki umeendelea kuwa mpana na mkubwa nakwa hakika jambo hili sasa limefikia wakati kuwa lazima lijadiliwe ili kujua niMuungano upi tunaotaka tuendelee nao. Wanachama wawili tu bila ya fursa zawanachama kuukataa, au uwezekano wa kukaribisha wanachama wengine, ili hataikitokezea wengine kujitoa bado utabaki kwa sababu ya wingi wa wanachama?

  Madhumuni ya Muungano wowote ule lazimayajumuishe kulinda maslahi ya kiuchumi, utamaduni, siasa na maendeleo na kwa kiasikikubwa kwa hali ilivyo hivi sasa Zanzibar haijapiga hatua nzuri katika maeneohayo kwa sababu ya Muungano wenyewe, ila kama kuna kusonga mbele basi ni kwajuhudi za Zanzibar wenyewe.

  15. Mgawano wa haki za Muungano

  Kuna haki nyingi za Muungano ikiwa ni zakiuchumi lakini hata fursa za ajira ambazo kwa hali ya sasa zinachukuliwa zaidina upande wa Tanzania Bara hata ikiwa ni za Kimuungano wazi wazi.

  Inaeleweka kuwa mpaka sasa hakuna utaratibumaalum uliowekwa wa kujua nini kinapatikana kutokana na vyanzo vya kiuchumi vyaMuungano na kwa namna gani Zanzibarinapata sehemu yake.

  Utaratibu wa sasa wa kusema kuwa Zanzibaripate 4.5 haukutokana na maelekezo ya Kikatiba hasa kwa vile Zanzibar inamsimamo kuwa wakati haidai sawa kwa sawa kwenye mgawano, lakini kwa uchacheinastahiki asilimia 11 kutokana na kiasi cha fedha ambacho Zanzibar ilitoawakati wa kuunda Benki Kuu ya Afrika Mashariki ikiwa ni fedha iliyohamishwakutoka East African Currency Board ambako Zanzibar ilikuwa mwanachama.

  Kwa sasa ijapo hakuna takwimu zakuthibitisha hayo, lakini ni jambo la wazi kuwa hakuna taasisi yoyote yaMuungano ambapo uwakilishi wa Zanzibar kiajiraunafanana na nafasi ya Zanzibarkwenye Muungano.

  Na hapajaonekana bidii yoyote ile katikahali ya upendeleo maalum ( positive discrimination) ili kuwezesha Wazanzibarikuingia katika ajira ambazo ni za Muungano na ambazo Zanzibar ina haki kamili kuzipata.

  Hesabu za rahisi zinaweza kuonyesha kuwasuala la tatizo la uajiri linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa iwapo kutakuwa nadhati ya kuwapa Wazanzibari nafasi za kazi katika ajira ya Muungano kwa vileidadi ya Wazanzibari ni tone dogo tu katika bahari kuu ya idadi ya Watanzania .

  16. Utata / Uwazi wa mipaka

  Tanzania ni mjumuiko wa nchi mbili za Tanganyikana Zanzibar.Dhana ya wazi na ya moja kwa moja iliyopo ni kuwa mipaka ya Tanzania ndani yake imo Zanzibarna kwa hivyo Zanzibarhaina mipaka yake wenyewe.

  Lakini kwa kuwa Zanzibar kwa aina na mfumo wa muungano ulioposasa ina sifa za kidola yaani Serikali, Watu na Eneo tabaan itakuwa na mipakayake.

  Vile vile kwa kuwa Zanzibar inajiendeshakikamilifu na inajisimamia kiuchumi ni wazi pia kuwa itakuwa na eneomaalumu inalotumia na hali kadhalika kwamaana hiyo ina eneo ambalo ina haki kulitumia kwa ajili ya kuhudumia wananchiwake.

  Ndipo baada ya utata na kutokuwepo uwazikwa muda mrefu na kudhirihirika pale Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilipokujana sheria iliyohusu uvuvi wa bahari kuu na kupingwa na Zanzibar,kuonekana kuwa ndani ya mipaka ya Tanzaniabasi Zanzibarinataka kuwa na mipaka yake.

  Katiba zote za Zanzibarna hata katika Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibarya 2010 hilo likajitokeza pale Katiba ilipotamkakuwa eneo la Zanzibar ni eneo lote ambalolilikuwa ni la Zanzibar kabla ya Muungano wa Tanzania wa 1964.

  Kwa maana hiyo eneo hilo linajumuisha eneo la bahari, na eneo labahari ni lile ambalo linatolewa na Umoja wa Mataifa kupitia kamati yake ambayoinatoa Kilomita 12 za kwanza kwa nchi lakini linatoa Kilomita 200 nyengine kwaajili ya kutafuta na kutumia rasilmali za bahari.

  Hadi sasa suala hili na haki ya Zanzibar katika hili kunautata na haliko wazi na kwa maana hiyo hii pia ni sababu madhubuti yaWatanzania kujadili Muungano ili hili liwekwe wazi na kuwemo ndani ya Katibaijayo.

  17. Upitizi wa Mambo ya Muungano

  Hadi sasa Mambo ya Muungano yamekuwayakiongezwa tu bila ya hatua yoyote ile ya kuyapitia kujua iwapo badoyanahitajika kuwemo katika Orodha ya Mambo ya Muungano au la.

  Kuendelea kuhitajika au kutohitajikakunaweza kuwa kwa sababu kadhaa. Sababu ya kushindwa kuwa ya kimuungano halisi,sababu za mabadiliko na maendeleo, sababu ya kiuchumi, sababu ya kiutekelezaji,sababu ya kwamba kila upande unajitosheleza n.k.

  Kwa mfano suala la Leseni za Viwandalimekuwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano lakini katika uhalisi hilihalijawahi kuwa jambo la Muungano kwa maana ya kutekelezwa kikamilifu.

  Hali kadhalika suala la Elimu ya Juu,lakini Zanzibar kwa muda wote imepata faidaisiyo kamilifu kwenye jambo hili kwa maana ya kukosekana uwekezaji wa Serikaliya Muungano katika eneo hili kwa Zanzibar hadi Zanzibar ilipoanza kujikwamua wenyewe kwa kuweka Zanzibar State Universityna kutengeneza mazingira ya kuanzishwa Vyuo Vikuu vyengine.

  Katika hili pia yapo mambo ambayoyamefanywa kuwa ni ya Muungano kwa sheria iliyoanzishwa kusema hivyoilhali kwa hakika si ya Muungano kama vile Bodi ya Viwango ya Tanzania (TBS) nakupelekea Zanzibarkuanzisha Bodi ya Viwango (ZBS).

  Pia kuna taasisi nyengine kadhaa kwa mfanoMamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania TPDC, Shirika la KuratibuMawasiliano Tanzania TCRA nk ambayo kiumuondo ni ya Muungano lakini yanataratibu zinazowatenga Wazanzibari kiajira.

  Mtu anaetaka kuomba kazi ya uanasheriakatika taasisi hizo hulazimika kufuata vigezo vya Tanzania Bara kwa maana yakuwa ni wakili anayetambuliwa na Mahkama Kuu ya Tanzaniana yule anaetambuliwa na Mahakama Kuu ya Zanzibarhawezi kupata nafasi.

  Ieleweke hili ni kosa la msingi kwa sababuinaeleweka wazi kuwa mamlaka ya Mahakama Kuu ya Tanzaniana Mahakama Kuu ya Zanzibaryako sawa sawa.  18. Haki yakizazi kipya

  Zaidi ya nusu ya Watanzania ni vijana ambaokuujua kwao Muungano ni kuukuta kama ulivyo na kamaulivyoundwa, kuendeshwa na wazazi hao. Wao vijana wa sasa na hata wazee wao hawakushirikishwakatika uundaji wa Muunganohuu tulionao hivi sasa.

  Kwa kuwa Muungano hivi sasa unaingia katikakizazi cha tatu, bila ya shaka zipo tashwishi, tamani, na matakwa mapya ambayo yanatokana na vizaziambavyo vina fikra mpya kuhusu Muungano wao.

  Vizazi vilivyokulia katika Muungano ingawavimeuona Muungano ukikuwa, lakini pia wameuona Muungano huo ukipita katikamisukosuko mingi na mara kadhaa ukiyumba na kwa hivyo kujiuliza hiviisingewezekana Muungano huu kuendeshwa kwa njia nyengine yoyote tofauti na hiiya sasa?

  Hii ni moja ya sababu muhimu sana ya kwa nini tujadili Muunganowakati huu ambao nchi itaingia katika kujadili Katiba Mpya kwa sababu bila yakufanya hivyo itakuwa ni kuendeleza udhaifu wa kuwa na umma ambao haujinasibishina Muungano na kwa hivyo wanaona kama si wao ila wao ni abiria tu katika gariambalo dereva wao hawajui anawapeleka wapi.

  19. Hitimisho

  Katika hali ambayo tumeieleza kwenyekijitabu hiki na hali ambayo kila Mzanzibari anaijua ni wazi kuwa tunalazimikakuujadili Muungano kwa kina na fursa adhimu iliyopatikana itumiwe kwa hoja,busara na umakini.

  Wengi wa Wazanzibari wanaaminiyaliojitokeza katika Muungano katika miaka yake hii yote na kupewa anuani yaKero za Muungano, yanatokana na kuwa wananchi hawakushirikishwa katika uundajiwa Muungano wenyewe.

  Pia imejitokeza kuwa Muungano una makosa yakimuundo na kiutekelezaji kiasi ambacho kamatulivyoona umelazimisha kutumiwa rasilmali nyingi kwa kuundiwa tume kadhaa wa kadhaa, ambazo kwa kuwahazikwenda katika tatizo kuu, kwa kurudi kwenye Mkataba wa Muungano, basimatatizo yamekuwa yakikumbiwa chini ya zulia.

  Kwa kuhitimisha ni vyema tuangalie muundowa mifumo kadhaa inayotajwa kuwa ni mnasaba kwa muungano wetu huu, uzuri wakena changamoto zake.

  1).Mfumo wa muungano wa serikali moja: Mfumohuu unawajibisha kupotea moja kwa moja kwa Zanzibarna Tanganyika,na kuundwa kwa Taifa moja lenye serikali moja na mamlaka moja. Ni mfumo ambaounaonekana wazi unapingwa mno na takriban na wazanzibari wote kwa vileutaiondoa milele Zanzibarkatika ramani ya dunia, kuifuta historiayake, utamaduni wake na hata kuwepo kwake. Huu ni mfumo ambao unaonekanahaufikiriwi kamwe na Wazanzibari.

  2). Mfumo wa serikali mbili: Huu ndio mfumouliopo hivi sasa katika Muungano wetu umekumbwa na migogoro mingi, umeonekanani mfumo uliokwama ila kutokana na utashi na ari ya wanasiasa wa Tanzaniakudumisha Muungano kwa gharama yoyote ndio maana Muungano huu umedumu. Mfumohuu unakasoro kubwa ya kimaumbile, kwa vile uliunda mamlaka tatu na baada yahapo ukachukuwa mamlaka mbili ukaziingiza katika udhibiti wa serikali moja, nahili ndio lililopelekea kuwa na kasoro kadhaa. Mfumo huu kwa fikra za watu wengini mgumu kutendea haki kwa usawa pande zote mbili za Muungano, kuanziaugawanaji wa rasilmali hadi usimamizi wa Serikali. Hofu ya Wazanzibari wengi nikuwa kuendelea kuwepo muundo wa Serikali mbili ni njia ya kuelekea kupoteakabisa mamlaka ya Zanzibar, kamailivyoonekana kwa kuongezeka Mambo ya Muungano kutoka 11 hadi yalivyo 22 hivisasa.
  3). Mfumo wa serikali tatu: Katika mfumo huuwa Serikali ambapo kutakuwa na Serikali kamilifu ya Zanzibarkama ilivyo hivi sasa, kurudisha Serikali ya Tanganyika na kisha kuunda SerikaliKuu ya Muungano. Imani ya wanaoamini mfumo huu ni kuwa kila upande utafanyakazi zake kwa kujitawala zaidi na Serikali Kuu ya Muungano itaratibu mambo yaMuungano.

  Zipo hofu nyingi katika hoja hii. Mojawaponi ya kuwa kuingia ndani ya mfumo huu ni kuuchujua Muungano na baadhi ya watuwanaamini ni kuelekea kudhoofika na pia hata kuvunjika.

  Hofu nyengine ni ile inayoelezwa ya gharamaambapo pande za Muungano zitabidi zichangie na huku uzoefu uliopatikana hadisasa unaonyesha ugumu wa kitu kama hicho nakila upande ukiona unabeba mzigo usiostahiki.

  Mfumo huu wa serikali tatu unaonekana naoumepitwa na wakati hasa kwa kuzingatia uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kwa mfano tunajiuliza baada ya kuundwa kwa serikali tatu, ni serikali ipi katiya hizo tatu itakayojiunga ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Endapoitakayojiunga ni serikali ya muungano (Serikali ya Shirikisho), je serikalihiyo itakuwa na mamlaka gani ya uwakilishi juu ya yale mambo ambayo kimsingi nakikatiba si ya Muungano bali yapo chini ya udhibiti wa serikali husika (Zanzibar na Tanganyika)? Vilevile endapo zitakazojiunga ni serikali zaTanganyika na Zanzibar ; je serikali hizo zitakuwa na mamlaka gani yauwakilishi juu ya yale mambo ambayo kimsingi na kikatiba ni ya Muungano baliyapo chini ya udhibiti wa serikali ya Muungano?

  Katika hili ndipo baadhi ya watu wanakwendambali zaidi na kutaka maamuzi magumu zaidi yafanywe nayo ni yale ya kila upandekuingia katika Jumuia ya Afrika Mashiriki kwa sifa kamili ya nchi yenye sifazote za nchi kwa mtizamo wa kimataifa.

  4). Mfumo wa Muungano wa Serikali mbili kwanjia ya Mkataba (treaty): Katika muundo huu tunakuwa na serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika/ Tanzania Bara, kilanchi ikiwa na serikali yake kamili, mamlaka kamili na uhuru kamili. Muungano wamashirikiano utakuwa unasimamiwa na mkataba (treaty) na sio kwa njia yakikatiba. Utaratibu wa Muungano kwa njia ya Mkataba (treaty) unaiwacha nchi namadaraka yake kamili. Mfano, Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaundwa nanchi tano (5) nchi hizo kila moja inamadaraka yake kamili na mashirikianoyanaratibiwa na Mkataba na sio katiba. Na pia European Commuinty (Umoja waUlaya) nchi wanachama zina mamlaka kamili na mashirikano yao yanaratibiwa na Mkataba.

  Katika kufikiria njia zote hizo, bilakuamini kuwa Muungano uvunjike, kuna umuhimu pia wa kuutizama mfumo wowote uleambao tutaufikiria na kuupendekeza kutizama na kuhakikisha kuwa Kero zaMuungano zilivyo hivi sasa hazitabebwa na kuingia katika zama mpya za Muunganozijazo.

  Kilio cha Wazanzibari cha Muungano kamakilivyo sasa ni kutokana na kero hizo ambazo zinaibana na kuikandamiza zaidiZanzibar na kuipendelea na kuinufaisha zaidi Tanganyika kama ambavyo haipendi kuitwa hivisasa kwa sababu ya kuwa jina hilo kikatiba halipo tena.

  Sisi Wazanzibari ndio wenye uwezo wa kuamuahatma yetu. Na hilolitafanywa katika hatua mbili. Kwanza ni kwa kutoa maoni wakati wa Mjadala waKatiba na kisha kupiga kura katika Kura yaMaoni ifikapo mwaka 2014.

  Zanzibar ni yetu,khatma ni yetu na chaguo ni letu  TAARIFA ZA ZIADA

  Mambo 11 ya Muungano ya asili
  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano
  2. Mambo ya Nje
  3. Ulinzi
  4. Polisi
  5. Hali ya Hatari
  6. Uraia
  7. Uhamiaji
  8. Biashara zaNje na Mikopo
  9.Utumishi waJamhuri ya Muungano wa Tanzania
  10. Kodi yaMapato, Kodi ya Mashirika, na Ushuru wa Bidhaa
  11. Bandari,Usafiri wa Anga, Posta na Simu

  Mambo 22 ya Muungano kwa mujibu wa Nyongeza yaKwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kama ilivyo tajwa katika Ibara ya 4ya Katiba ya 1977.

  1. Katibaya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  2. Mamboya Nchi za Nje.
  3. Ulinzina Usalama.
  4. Polisi.
  5. Mamlakajuu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
  6. Uraia.
  7.Uhamiaji.
  8. Mikopona baiashara ya Nchi za Nje.
  9.Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watubinafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchiniTanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
  11. Bandari, mambo yanayohusika nausafiri wa anga, posta na simu.
  12. Mambo yote yanayohusika na sarafuna fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamojamabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni nausimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
  13. Leseniya viwanda na takwimu.
  14. Elimuya juu.
  15. Maliasili ya mafuta, pamoja namafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezoza mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
  16. Baraza la Taifa la Mitihani laTanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
  17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
  18.Utafiti.
  19.Utafiti wa hali ya hewa.
  20.Takwimu.
  21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
  22. Uandikishaji wa Vyama vya siasa naMambo mengine yanayohusiana navyo.

  Mambo31 ya Muungano yalivyo baada ya kunyumbuliwa

  1. Katiba yaMuungano2. Mambo ya nje3. Ulinzi 4. Usalama5. Polisi6. Hali ya Hatari7. Uraia8. Uhamiaji9. Mikopo ya Nje10. Biashara11. Utumishi katika Serikali ya Muungano12. Kodi ya Mapato13. Forodha (Ushuru)14. Kodi ya Bidhaa (exercise)15. Bandari 16. Usafirishaji wa Anga17. Posta18. Simu 19. Sarafu20. Mabenki21. Fedha za Kigeni22. Leseni za Viwanda23. Takwimu24. Elimu ya Juu25. Mafuta yasiyosafishwa26. Gesi asilia27. Baraza la Mitihani28. Usafiri wa Anga29. Utafiti30. Mahkama ya Rufaa31. Usajili na Shughuli za Vyama vya Siasa
  Kamati ziloundwa na Serikali ya Zanzibar kuhusuMuungano baina 1990-2003

  (a) Kamatiya Rais ya Kupambanua Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamhuna, 1997).(b) Kamatiya Rais Kuchambua Ripoti ya Kisanga (Kamati ya Salim Juma).(c) Kamatiya Rais ya Kuandaa Mapendekezo ya SMZ juu ya Kero za Muungano. (Kamati ya Ramia,2000).(d) Kamati ya BLM juu ya Sera yaMambo ya Nje.(e) Kamati ya Rais ya Wataalamu juuya Kero za Muungano (2001).(f) Kamati ya BLM ya Jamuiya yaAfrika Mashariki.(g) Kamati ya Mafuta(h) Kamati ya Madeni baina ya SMZna SMT.(i) Kamatiya Suala la Exclusive Economic Zone(EEZ)(j) Kamati ya Masuala ya Fedha naBenki Kuu.(k) Kamati ya Rais ya Masuala yaSimu – (1996 – 1999)(l) Kamatiya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992.(m) Kamati ya Mafuta(n) Kamatiya Suala la Exchusive Economic Zone (EEZ)(o) Kamati ya Masuala ya Fedha naBenki Kuu.(p) Kamati ya Rais ya Masuala yaSimu – (1996 – 1999)

  Kamatizilizowahi kuundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Muungano

  (a) Kamati ya Mtei(b) Tume ya Nyalali(c) Kamati ya Shellukindo(d) Kamati ya Bomani(e) Kamati ya Shellukindo 2, yakuandaa Muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT.(f) Kamati ya Harmonisation.(g) Kamati ya Masuala ya Simu(Kamati ya Kusila) Baadhiya mambo mazito ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikushirikisha Serikali ya Mapinduziya Zanzibar
  (i) Katika uanzishaji wa Benki Kuu,mwaka 1965 na marekebisho ya Benki Kuu, 1995.(ii) Uanzinshwaji wa Mamlaka yaMapato TRA.(iii) Katika suala la Jumuiya yaAfrika Mashariki.(iv) Sera ya Mambo ya Nje(v) Uraia na Uhamiaji na(vi) Sheria ya Deep Sea FishingAuthority.
  Mambo ambayo mabadilikoyake yahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wotekutoka TanzaniaVisiwani kama ilivyotajwa Katika Ibara ya 98 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano

  1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.
  2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais waJamhuri ya Muungano.
  3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuriya Muungano.
  4. Kuwapokwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
  5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.
  6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
  7. Orodha ya Mambo ya Muungano
   
Loading...