Utamaduni wa wahaya na kifo cha kanumba

Huyo mama ake kanumba inaonekana alikuwa mcharuko wa hatari! Inawezekanaje kila mtoto akawa na baba yake kivyake?
Nway,kwa sisi wakurya angezikwa TARIME/SERENGETI/BUNDA. Na si either kwa mama(BK) au kwa wasanii(DAR) regardless baba kamlea or not!!!

RIP KANUMBA 'THE GREAT',umetangulia,sisi tupo nyuma yako!
 
Mila Nyingi za kiafrica mtoto akifariki huzikwa kwa maagizo ya baba mzazi!
Sasa ili la Kanumba mama yake kufanya maamuzi inaonesha
1.kuwa labda Baba yake alimtelekeza Kanumba
2.Kanumba alikuwa mtoto wa nje ya ndoa
3.Baba yake Kanumba hakutoa mahari ya kumuoa mama wa Kanumba
4.Ubabe wa uyu mama wa Kihaya mara baada ya kutelekezwa na mumewe
Any of the above could be true
 
Nyie wote mnaojadili mambo ya watu mmeulizwa?
Pilipili ziko shamba nyie mnawashwa!
Angalieni yenu kwanza.
 
Acheni porojo wanajf, mtu akisha kufa hakuna majadiliano kama haya mnayojadiliana hapa, nashangaa wasomi wazima humu mnabonyeza keyboard kuzungumzia maziko ya maiti. Huu ni ufinyu wa kufikili kwa mapana kwa mila mlizorithi toka kwa mababu zenu. Binafsi nawapongeza wasanii kuzikia hapo Dar maana hakuna haja ya kupoteza pesa zetu kusafirisha maiti huku uchumi umekuwa mgumu. Kwangu mimi mtu akisha kufa azikwe sehemu alipo, wanaosafirisha maiti umbali wote huo ni sifa tu wanajitakia hakuna lolote la maana. Mambo ya kusafirisha maiti tuyapinge kwa nguvu zote maana utakuta kwa mfano mtu anakufa kwa kukosa laki mbili za matibabu lakini akifa watu wanatumia million moja kusafirisha maiti, it can't bring any sense. Take care Tanzanians
 
jamani naomba tusihusishe huamuzi wawapi azikwe kanumba na maswala ya roho za wanawake baadhi,sisi sote hatujui sababu za kutengana kati ya mama na baba kanumba,tunakosa utu kuwatuhumu wanawake wote kisa tuliona mwanamke fulani kafanya vile.Na swala la kuhusisha kabila natabia ya mtu sijui inatoka wapi? mimi nahamini mtu ubebe tabia yake,wala hakuna mtu anaye beba tabia ya kabila. Amani kwenu

Maoni mazuri. Ni kosa kuwahukumu watu wa kabila fulani au taifa fulani kutokana na kosa, tabia au mwenendo wa mtu fulani au kikundi fulani ndani ya kabila au taifa hilo. Napenda nikiri kuwa nilikuwa simfahamu Kanumba licha ya kusikia jina lake mara chache pale wanasanii mbalimbali walipokuwa wakimtaja. Hii ni kutokana na kuwa alipoanza kujitokeza na kujulikana ndipo niliondoka nyumbani na kuja huku na hata ninapokuja nyumbani sijawahi kuangalia filamu zake. Aibu kwangu. Nimefurahi kuona kuwa Watanzania wengi walimkubali na kujihusisha naye hiki ni kitu kizuri ni kama wengi watu tulivyohuzunika na kuomboleza sana pale Gibson Sembuli, Mbaraka Mwinshehe, Edward Sokoine na baadaye Amina Chifupa walipofariki. Vilevile ni kama ambavyo Salum Abdalah na Shabani Robert walivyofariki vifo vyao vilileta huzuni mkubwa kwa Watanzania wa miaka ya 60.

Kisheria na ninaomba nisahihishwe kwa wale wanaofahamu vizuri mahusiano ya wazazi wake. Kama wazazi wake hawakufunga ndoa basi Kanumba licha ya kuchukua jina la ukoo wa baba yake anahesabika ni wa ujombani. Hali inageuka tu kama licha ya kasoro hiyo baba yake alikwenda kulipa kikomboa mtoto kwa wazazi wa mama yake. Hii ndiyo sheria ya asilimia 80 ya makabila yote ya Tanzania ambako watu hurithi ubabani. Kikomboa mtoto akizidi shilingi 100 lakini wengi hawalipi.

Ninapenda kusema si vizuri kuhukumu kabila fulani na kusema hawa wanafaa wale hawafai. Sisi sote tu binadamu na kwa hali inavyokwenda Watanzania wengine watakuwa wale wanaotokana na mchanganyiko wa makabila mbalimbali na hivyo kuendeleza ujima wa ukabila ndiko kupitwa na wakati. Ni vema tupiganie utaifa wetu na mchangamano wa makabila na dini zetu. Huko ndio kujamiika au kuungwanika.
 
Acheni porojo wanajf, mtu akisha kufa hakuna majadiliano kama haya mnayojadiliana hapa, nashangaa wasomi wazima humu mnabonyeza keyboard kuzungumzia maziko ya maiti. Huu ni ufinyu wa kufikili kwa mapana kwa mila mlizorithi toka kwa mababu zenu. Binafsi nawapongeza wasanii kuzikia hapo Dar maana hakuna haja ya kupoteza pesa zetu kusafirisha maiti huku uchumi umekuwa mgumu. Kwangu mimi mtu akisha kufa azikwe sehemu alipo, wanaosafirisha maiti umbali wote huo ni sifa tu wanajitakia hakuna lolote la maana. Mambo ya kusafirisha maiti tuyapinge kwa nguvu zote maana utakuta kwa mfano mtu anakufa kwa kukosa laki mbili za matibabu lakini akifa watu wanatumia million moja kusafirisha maiti, it can't bring any sense. Take care Tanzanians
Kua uyaone mwanangu. Utoto tu unakusumbua.
 
WANAJF;
Kwanza naomba nitangulize pole kwa wafiwa wote na Watanzania kwa ujumla kutokana na kifo cha mpendwa wetu Steven Kanumba. Sasa hoja yangu hapa ni moja tu kuhusiana na utamaduni wa Wahaya na kifo cha Kanumba. Hivyo, ninaomba hasa wale wenye uelewa (hasa watani zangu Wahaya) waweze kutupa maelezo hapa.

Hoja yangu ni kwamba je marehemu Kanumba ni Msukuma au Muhaya? Nauliza hili swali kwasababu kwenye gazet la mwananchi inasema hivi " Dada wa marehemu, Abela Kajumolo alisema kuwa mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican.

Alisema familia imepanga mazishi ya Kanumba yatafanyika Jumanne wiki ijayo na kwamba bado hawajaamua kama atazikwa Dar es Salaam au Bukoba," alisema.

Tayari kamati ya mazishi imeundwa na ikiwajumuisha Gabriel Mtitu, Stephen Jacob (JB) William Mtitu na Issa Mussa (Cloud) ambao wote ni wasanii wa filamu nchini.

Kamati ya usafiri itakuwa na Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Vincent Kigosi (Ray)".

Sasa swali langu ni kwamba kama Kanumba ni Msukuma na babake mzazi yuko Shinyanga ni kwanini option za mazishi ziwe ni Dsm na Bukoba na siyo Shinyanga kwao? nadiriki kusema kwao, kwani hata yeye marehemu alitambua hilo ndiyo maana anatumia jina la babake (Kanumba-hili si jina la kihaya bali ni jina la kisukuma), na pia alishatangaza kwamba atakwenda kugombea Ubunge kwao (Shinyanga na si Bukoba). hivyo alitambua fika kwamba yeye ni Msukuma na si Muhaya. Huko Bukoba ni kwao Mama yake, sasa kwanini marehemu akazikwe kwa bibi yake wakati ana kwao (Shinyanga)?

Nalazimika kuuliza hili swala kuhusu mila za watani zangu Wahaya kwasababu hata familia yangu haya yalitukuta mwaka jana tupofiwa na mke wa kaka yetu hapa Dsm. Kaka yetu alimwoa shemeji ambaye alikuwa ni muhaya na waliishi kama mwaka 1 kabla msiba haujamkuta shemeji. Sasa msiba ulipotokea ndipo Wahaya wakasema wanataka msiba ukafanyikie kwao mwanamke kwasababu mila zao zinawataka kufanya hivyo. Hili lilikuwa jambo gumu sana kwetu sisi ambao si Wahaya kwasababu binti yao alishaolewa na kaka yetu, hivyo kwa kuangalia mila zetu ni kwamba akiwa kwetu hawezi kuhamisha mila zao na kuzifanya ziwe za kwanza. Mke alipokubali kuolewa naye sasa anakuwa kwenye familia nyingine na taratibu za mila za kabila zake si rahisi zi operate kwenye culture nyingine. Tulivutana sana na kuwaeleza uhalisia wa tamaduni zetu na hata jinsi ukweli ulivyo na kuwaambia kwamba huyu ni mke wa kaka yetu na ni mwanafamilia yetu na hiyo msiba uko kwetu na atazikwa kwetu. Na ndivyo ilivyofanyika, japo na wao baada ya mazishi waliondoka na kuhaidi kwenda kuweka msiba kwao (sijui kama ilifanyika ama la, sina hakika kwasababu sikufuatilia zaidi baada ya kusafiri).

Hivyo, naomba ufafanuzi hasa toka kwa watani zangu Wahaya katika hili hasa inapotokea misiba ni kwanini Marehemu akazikwe kwa bibi yake wakati ana kwao?

NB: Nawaombeni radhi wale wote nitakaokuwa nimewakwaza kwa namna moja au nyingine, lkn nimelazimika kuandika kwasababu yaliwahi kunikuta na hata sasa yanatokea kwenye msiba wa marehemu Steven Kanumba.

Jibu lipo kwenye hii video



Ila kwenye gazeti moja huko siku za nyuma jamaa aliwahi kumponda babaye na kumsifu mamaye!
 
Last edited by a moderator:
Kwetu uhayani mke anaitwa 'mukyala' (meaning mgeni/aliyekuja kutembea), kwetu mwanamke akiolewa ndo imetoka hiyo kwao atakuja 'kutembea' tu. Hata iweje akifariki atazikwa kwa mmewe hata kama walishaachana.Actually zamani kwetu mke angeweza kuachika na bado mtoto atakayezaa na mwanaume mwingine atakuwa ni wa former husband (anaitwa 'omwana webisisi). The same applies kwa watoto,watoto wako kwenye himaya ya baba hata kama walizaliwa na kukulia ujombani(bunyinarumi). Ndio maana kama ingetokea Mungu hajamchukua Kanumba kikwetu kama angeamua kuoa baba yake ndiye angemuolea (okumushwelelela) nandiye angemkabidhi mkuki (sio wajomba).
Nawapa pole sana wafiwa wote,Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
RIP Steve,tulikupenda Mungu amekupenda zaidi.

Ulichosema ni sawa kabisa. nadhani marehemu hakuzaliwa kwenye ndoa! It is impossible mwanamke wa kihaya kungangania watoto/mtoto kama umeoa kama mila/sheria inavyotaka. Hawana utamaduni wa kulumbana kuhusu watoto kama ni wa ndoa. watoto wa ndoa ni wa baba,!!!kama sio wa ndoa, then hapo kila mtu anafanya lake kama yanayotokea hivi kwa kanumba.
 
Prof., ahsante kwa ufafanuzi japo mimi concern yangu siyo kusafirisha maiti bali ni kwanini kuwe na option ya Bukoba badala ya Shinyanga/Mwanza? Hilo ndilo lilikuwa concern yangu.
of


Mkuu ktk hali ya kawaida jibu unalotaka huwezi kulipata kwa mtu mwingine nje ya wanafamilia ya Kanumba. Umeuliza utamaduni wa wahaya na Prof. kafafanua vizuri na huo ndo ukweli. Kwa hiyo kilichotokea kwa Kanumba ni swala la kifamilia zaidi na si swala la kimila kwa maana ya wahaya
 
Tusikimbilie kuangalia kuangalia yaliyotokea katika msiba wa marehemu na kuanza kulaumu. Haya tunayoyaona ni matokeo ya watu kutokuwajibika. Kama wanaume wangekua wanawajibika ipasavyo kwa watoto wanowazaa tusingekua na watoto wa mitaani, tumekua na utaratibu wa kuabebesha wanawake mimba halafu tunawakimbia. SK amewahi kutamka kua hatokaa asahau mateso aliyoyapata kwa mama wa kambo na akamlaumu baba yake kwa hilo. Zaidi ya 95% ya maisha ya SK alikua zaidi kwa mama yake kuliko baba yake, kama akiwa mzima alikua haendi shinyanga kwa baba yake unategemea nini. Baba alimtosa mama akamuangaikia mwanae, suala la kwamba wanapigana vijembe kwa ajili ya mali za marehemu sikubaliani na suala hilo. Ifikie wakati tuheshimu hata haki za marehemu.
 
Yalosemwa ni mengi, - tufikie mwisho!

Kuzaa si kazi kazi kulea.

Hivyo kama huyo mzee alifikiri kuzaa ndo kazi majibu ameyapata kwa wanaojua maana ya msemo huo hapo.

waitu muliwo mutai!
 
si unajuwa tena watu wakiwa na vijisenti
wanaona kuwa wana uwezo na kila kitu hata
kiwe na ugumu kama jiwe.
 
nimejifunza kiasi kuhusu mila za kihaya.sielewi kwa nini watu wanapenda kuwasema vibaya wahaya.kwani nina rafiki yangu ameolewa na muhaya,alivyoulizwa mume wako ni kabila gani,alivyotaja muhaya,watu waliguna.yeye ni mtu wa morogoro

Tatizo kubwa ni inferiority complex, wengi wao huwa wana kawaida yaku-build themselves up by tearing down HAYAS - hili la kuguna ni mojawapo ya tactics wazitumiazo kuonyesha kwamba WAHAYA wana walakini fulani. Jaribu kumuhoji huyo mtu wa morogoro akwambie ukweli kama ana TATIZO NA MUMEWE; UTASHANGAA ATAKACHO KUELEZA.
 
nimejifunza kiasi kuhusu mila za kihaya.sielewi kwa nini watu wanapenda kuwasema vibaya wahaya.kwani nina rafiki yangu ameolewa na muhaya,alivyoulizwa mume wako ni kabila gani,alivyotaja muhaya,watu waliguna.yeye ni mtu wa morogoro

Next time waulize kwa nini wanaguma.
Lazima kuna sababu.
Shoga yako anajua fika ni kwa nini watu huwa wanaguna.
 
wanaume bana hata ham eleweki, mwanamke humtaki ukamtelekeza na watoto wake, bado unataka akung'ang'anie,
ili iweje

kwa mwanamke mwenye uwezo wake atajilelea watoto wake kama alivyofanya mama Kanumba, watoto wakifanikiw ndo ujifanye ulizaaa acheni ukilaza bana
 
..................Actually zamani....................................

Huwa nafurahi sana nnapoona watu wanashusha vitu vya mila zao. Ni raha sana kwa kweli. Hata hivyo, ningeshangaa kama huto tu red and bolded word tungekosekana! kiw kwi kwiiiiii!
 
Back
Top Bottom