Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Wahadzabe wamekuwa na mfumo wa maisha unaoheshimika duniani, wakihusishwa na uwindaji wa asili, maarifa ya mimea tiba na mfumo wa kijamii usio na mpangilio wa tabaka. Lakini mabadiliko ya karne hii yameingia kwa kasi isiyozuilika.
Wageni na makampuni ya utalii wamevamia makazi yao kwa lengo la kuonyesha “utalii wa kiutamaduni,” huku mitandao ya kijamii kama TikTok, Instagram na Facebook ikitengeneza taswira mpya ya Wahadzabe—si kama jamii huru yenye thamani yake, bali kama vivutio vya kimaonesho.
View: https://www.facebook.com/share/v/1HxmousatS/
Ukienda Facebook kila picha na video inayopakiwa mtandaoni huwafunika kwa pazia la taswira nyepesi: jamaa wanaovaa ngozi, wakiimba au kucheza kwa ajili ya kamera. Chaba anavuta sigara mara wamempa Heineken anywe.
Hali hii inaharibu mizizi ya heshima kwa utamaduni wao na kugeuza mila kuwa bidhaa ya kitalii. Vijana wa Kihadzabe nao, wakiguswa na ulimwengu wa kidijitali, huanza kupoteza thamani ya mila walizorithi na kuvutiwa na maisha ya kisasa, ikiwemo vyakula vya viwandani, mitindo ya nguo na hata muziki wa kigeni. Mfano mzuri akiwa ni CHABA na DUDUKWE.
Hata hivyo, kuna ukimya unaotawala mazungumzo haya. Wale wanaojaribu kuibua hoja ya uharibifu wa utamaduni, mara nyingi hukumbana na ukinzani.
Wapo wengine hudai kuwa kuzungumzia hatari hizo ni kuzuia utalii, jambo linaloweza kuathiri mapato ya makampuni na hata uchumi wa taifa. Lakini je, tunapaswa kupima thamani ya jamii kama Wahadzabe kwa mizani ya dola na faida pekee?