SoC03 Utalii mamboleo kwa maendeleo ya taifa

Stories of Change - 2023 Competition

Mofassa

Member
Jun 6, 2023
7
3
Utalii; Ni kitendo cha mtu au kundi la watu kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa lengo la burudan, biashara, kujifunza au makusudi mengine (Wikipedia, 2023). Utalii kwa Tanzania hivi sasa imekua ni sekta inayochangia takribani 25% ya pato la taifa na hii ni kwa mujibu wa hotuba ya waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mh. Mchengelwa. Hata hivyo sekta hii ya utalii imekua ni sekta inayoingiliana na srkta nyingine za kimaendeleo ikiwa pamoja n barabara, maji, umeme na sekta nyingine za kimaendeleo ili kuhakikisha sekta hii (Utalii) inaleta maendeleo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Sekta ya Utalii nchini Tanzania ni moja ya sekta muhimu inayotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi. Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya asili kama vile mandhari za kuvutia, maeneo ya kihistoria na ya kiakiolojia, hifadhi zenye wanyamapori wengi na baionuai mbalimbali, fukwe zisizochafuliwa na wingi wa utamaduni wa makabila 158. (Tovuti kuu ya Serikali, 2023)
download.jpeg










Kundi la watalii katika hifadhi ya serengeti wakifanya shughuli za utalii. Picha kutoka Wikipedia.

Mamboleo; Neno hili linamaana ya kitu chochote ambacho kinaweza kufanyika au kufanywa kwa njia au mbinu mpya. (Enye-mbinu mpya).

Taifa; Ni kundi lolote la binadamj lenye utamaduni wake maalum na mapokeo yake katika kihistoria ya eneo fulani. Mara nyingi umoja wake unatengeneza pia lugha. (Wikipedia, 2023).

Utalii mamboleo; Hii ni aina ya utalii ikiwa inahusisha vitendo vya kusafiri kwalengo burudani, kujifunza au makusudi mengine kwa kutumia njia au mbinu mpya tofauti na zile zilizozoeleka. Mfano kusafiri kidigitali badala ya kutembelea vivutio kiuhalisia. Na hii inatakiwa kuendana na mabadiliko na ukuaji wa kidigitali kwa dunia ya sasa.

Maendeleo ya taifa; Tunapozungumzia maendeleo ni hali ya kutoka ngazi moja kwenda nyingine ambayo ni ya juu zaidi kwa minajili ya kiuchumi,kijamii, kisiasa, kielimu na hata kisayansi. Kwa Tanzania maendeleo ya taifa hua yanaambatana na sera za maendeleo ambazo huwekwa na serikali ambazo zinachagiza ukuaji wa taifa letu. Maendeleo haya ya taifa hulinganishwa kwa vipindi ambavyo ni kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na hata baada ya ukoloni hadi hivi leo.

Pamoja na hayo ninapenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mh. Mchengrwa kwa kufanya juhudi hadi kuifanya sekta ya utalii kuwa ni miongoni mwa Wizara inayochangia 25% ya pato la taifa . Lakini sekta hii imekua ni chachu ya upotevu wa fedha nyingi za ndani na nje ya nchi ambazo zingeongeza pato hilo la taifa kutoka hiyo 25% na kwenda mbali zaidi. Hivyo basi sekta hii ya utalii inapaswa kufanya mageuzi makubwa ambayo yatafanya utalii kufanyika kisasa na kulifanya taifa kuongeza pato lake ili kufanya maendeleo zaidi kwa taifa.

Mageuzi ya sekta ya utalii ili kuendana na utalii mamboleo

Kama nilivyosema hapo awali ili kuifanya Sekta hii ya utalii iongeze tija ni lazima serikali ichukue juhudi za makusudi kuifanya sekta ya utalii kuwa mamboleo ambapo sasa itaweza kuongeza pato la taifa na kuchochea maendeleo ya taifa na raia wake kwa ujumla. Kutokana na kulitambua hilo muandishi amebainisha njia kuu moja ya kufanya mageuzi ya sekta ya utalii kutoka kwenye ukawaida kuja kwenye utalii mamboleo.

  1. Kuboresha mifumo ya kieletroniki, njia hii ndo njia kubwa ambayo kama ikitumika kikamilifu na kwa ustadi mkubwa basi inaweza kuongeza mapato zaidi. Kupitia hili mambo mawili yanatakiwa kufanyika, mambo hayo ni kama ifuatavyo.

 Njia ya kwanza ni kutumia mifumo hii ya kieletroniki katika kufanya matangazo; Hii inatokana na kwamba, kama tunaweza kukusanya 25% ya pato la taifa kutoka kwenye utalii bila kufanya matangazo kwa kiwango kikubwa hii inamaana kama tukifanya matangazo maana yake kutakua na matokeo chanya kwenye pato la taifa na linaweza kupelekea maendeleo makubwa kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

 Kubuni makusanyo kwa kutumia kurasa na mitandao ya kijamii; Hii inaweza leta mapato kwa kutumia mifumo ambayo inawafaidisha hata wasanii mfano kwa kuweka video za utalii kwenye chaneli rasmi ya Wizara ya Utalii ambapo itaweza kuongeza pato la taifa na hiii itapelekea kuongezeka kwa maendeleo kwa taifa. Lakini njia hii ni pendekezo la muandishi ili kuongeza mwanya wa ukusanyaji wa mapato kupitia sekta ya utalii. Vivyohivyo kuwekwa tozo kwenye vinjari na tovuti rasmi za sekta ya utalii na kumfanya mtu au mtalii kuweza kulipa pesa kidogo kwaajili ya kutafuta vitu mbalimbali kama vile mbuga za wanyama, na vivutio vingine na hii pia itaweza kuongeza makusanyo na kufanya utalii uwe bora kwa kutumia mbinu mpya. Hii itaongeza pato la taifa na kupelekea hata maendeleo kwa taifa.

Hivyo basi muandishi anasisitiza kua kama sekta ya utalii ikitumiwa kwa ustadi mkubwa hata wa kufikia asilimia 90 kwapamoja kuendana na mabadiliko na ukuaji wa sayansi na teknolojia inaweza kufanya utalii kuwa mamboleo na kuleta maendeleo makubwa sana kwa taifa hili.
 
Back
Top Bottom