Utajuaje kama wewe ni shujaa?

Ngosi

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
386
179
1. Kama ulikata daftari mara mbili. Kipande kimoja ukaacha nyumbani na kingine ukaenda nacho shule. We ni shujaa.
2. Kama ulitumia kipande cha kandambili kama ufutio.
3. Kama ulikanyagia kisigino ulipotoka kuoga ili usichafuke kwa kuwa hauna kandambili....nakusalimu.
4. Kama kwenu mlianika betri za national ili ziongezeke chaji kwenu ni mashujaa.
5.Kama ulilala na sare za shule ili asubuhi usichelewe halafu asubuhi ukajikuta umejikojolea wewe ni shujaa.
6. Kama ulienda choo porini na ukajipangusa kwa nyasi hongera aisee.....
7. Kama uliweka chumvi kwenye uji mweupe ndio ukanywa....
8. Kama ulilamba sukari ukapangusa mikono na ukasahau mdomo....sema kichapo heheeee
9.Kama uliogea karai la chuma wewe ni shujaa
10.Kama uliambiwa ushike sikio la kulia kwa kupitisha mkono wa kushoto juu ya kichwa ndio uende darasa la kwanza.....we ni rika na Anko J Kitime
11.Kama ulipaka mafuta yanaitwa RAYS ya bluu....wewe ni shujaa kama Kaka Gano
12.Kama sare yako ya shule ilikuwa na viraka vingi hadi watu wasitambue rangi ya sare ya shule yenu.....duh!
13.Kama ulivalishwa nepi na sio papmpers.....
14.Kama ulikunywa maji kwa kata na ukaogea sabuni ya REXONA wewe ni......
15.Kama wewe ni mwanamke na unakulaga maparachichi mawili peke yako......shujaa ni wewe.
16. Kama ulipenya njaa ya mwaka 1984 na bado unaijua facebook wewe ni shujaa.
17.Kama ulipakwa Giv au mafuta ya breki ya AGIP kwenye kidonda.....
18.Kama ulienda shule peku huku umebeba kuni na maji ya kuwapikia walimu...hakika wewe ni rika na Kingunge Ngombale Mwiru.
19.Kama ulivaa kandambili mikononi wakati mnacheza mpira wa makaratasi "one touch".....
20.Kama uliweka kioo chini ya dawati ili uwachungulie wasichana...
21.Kama mpiga picha alishakuambia picha yako imeungua basi wewe pia ni shujaa
 
naiboresha no 6

Kama ulienda choo porini na ukajipangusa kwa mchanga,, yaan uka_SOTA mchangani
Wew ni shujaa
 
Back
Top Bottom