Utajiri wa nssf | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa nssf

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ami, Dec 29, 2011.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ukiwa mfanyakazi serikalini au katika mashirika ya umma na binafsi kuna sheria kabisa ya nchi inayolazimisha kuwa lazima uwekeze kwenye NSSF.Na pesa yenyewe si ndogo,ni takriban 20% ya basic salary ya mwajiriwa.Mlimbikizano wa pesa hizi umeifanya NSSF kuwa tajiri sana.Cha ajabu hao wanachama wanapotaka pesa yao huzungushwa na hatimae wengine kufikia kufa kabla hawajazitia mkononi.
  Hivi sasa NSSF imehemkwa kutokana na utajiri wake uliopindukia.Mara wanajenga daraja la juu ya bahari,mara maghorofa yasiyo na idadi,mara inalima mkonge.Jee ni halali kufanya yote hayo bila kushauriana na wenye pesa zao?.
   
 2. s

  sawabho JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Yaani hao tu wapo wenzake akina PSPF, PPF, LAPF n.k makato kutoka kwenye mishahara kiduchu ya wafanyakazi inawachanganya na kuwafanya hata wasiwajali hao wanaokatwa hizo pesa.
   
 3. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hivi nani mwanzilishi wa sheria? namchukia kama aliyeanzisha matumizi ya pesa. ........Nimemaliza!
   
 4. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hii nayo ni huruma ya NSSF au kuturudisha kwenye vijiji vya ujamaa?.Baadhi ya wanaolazimishwa kuchangia NSSF wala hawana haja na nyumba zenye michoro ya NSSF zilizopangwa kama kota au za Kibutz.
  ..............................................................................
  MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) inatarajia kuwekeza katika ujenzi wa hoteli ya kitalii na nyumba za kuishi, jijini Mwanza ambazo wanatarajia kuziuza kwa wanachama wao na kwa wananchi.

  Katika mradi huo zaidi ya nyumba 687 zinatarajiwa kujengwa katika maeneo ya Bugarika pamoja na Kiseke ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapunguzia wanachama gharama za ujenzi.Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mipango na Uwekezaji, Yacoub Kidula alisema mpaka sasa wameishalipa fidia kwa watu wote ambao walitakiwa kuhama kwenye maeneo hayo na asilimia 40 ya fedha kwa halmashauri ya jiji ili kutengeneza miundombinu ya barabara katika maeneo hayo.

  “Michoro yote ya ujenzi wa nyumba pamoja na hoteli imekamilika, muda siyo mrefu tunatarajia kunza ujenzi ambao utachukua mwaka mmoja kukamilika,”alisema.Alisema wanaharakisha ujenzi wa nyumba hizo ili kushindana na mfumuko wa bei na kuzifanya nyumba hizo kuwa za gharama nafuu ili kila mmoja amudu gharama za kununua.

  Kwa upande wa ujenzi wa hoteli alisema wameamua kuwekeza katika mradi huo kwa kuwa mji wa Mwanza unakua kwa kasi.Alisema katika awamu ya pili ya mradi huo watajenga shule pamoja na vituo vya afya katika maeneo hayo mawili ambayo watakuwa wamejenga nyumba za kuuza ili kusogeza huduma karibu wa wateja wao.

  “Mchakato wa kuomba viwanja kwa ajili ya huduma muhimu unaendelea na halmashauri ya jiji imetuhakikishia kutupatia viwanja hivyo,”alisema Kidula.Waziri wa wa Kazi na Vijana Gaudensia Kabaka alisema Serikali inatakiwa kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wa ndani ili kuongeza thamani ya ardhi.

  “Ujenzi wa nyumba hizo ni wagharama kubwa na serikali haiwezi kujenga, ninaomba kusiwapo na vikwanzo vyovyote ili kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo pamoja na hoteli hiyo ya kitalii,”alisema Waziri Kabaka.
  MWANANCHI
   
 5. E

  Edo JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nakushauri tafuta wastaafu waliolipwa na hiyo mifuko uwaulize kama wanaona kuna umuhimu wa hii mifuko au la! Pia tafuta muda uhudhurie mikutano yao ya wadau utajibiwa yote unayouliza au waone maafisa habari wao watakujibu na kufafanulie haya yote. Naomba tusipende kulalamika wakati wapi pa kupata majibu hayo panajulikana!
   
 6. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mimi mwenyewe ni mwanachama lakini siridhiki na hii mipango.Na nakumbuka kuna mwalimu alikufa njiani akifuatilia mafao yake ya NSSF,sioni sababu ya kufuata bla bla kwenye ofisi zao.
   
 7. Baba Imani

  Baba Imani Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Edo mkuu acha hizo! Mifuko ya pensheni siku zote, duniani kote ni sawa na ng'ombe wa maziwa kwa mfugaji. Mfugaji wote tunamjua, ni wanasiasa walioko madarakani. Ninyi kinda Edo na wenzio mnaotumika kwenye mifuko hii ni cowboys tu. you have an interest to serve. Nakushauri unyamaze pale wananchi wanapoamka na kuanza kuhoji hizi Ponzi Schemes zenu. Naturally hamtapenda watu waamushwe, it is a class struggle.
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwanini NSSF haifanyi mfumo kama wa kibati ili kila mwanachama muda wake ukifika akapewa kitita cha pesa na kuchagua mradi anaopenda badala ya wao kufanya miradi na kutangaza magazetini.
   
Loading...