Huu Ndio Utajiri wa Msanii Diamond Platnumz
by
Frumence M Kyauke.
Nasibu Abdul Juma Issack, almaarufu
Diamond Platnumz, ni msanii Afrika mwenye kipaji kikubwa cha uimbaji vilevile ni msanii tajiri zaidi.
Umaarufu wake umeanza kuonekana mwaka 2010 baada ya kuachia albamu kwa jina
Kamwambie.
Bingwa huyo wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania amefanikiwa kuachia vibao vikali na vinavyovuma ikiwemo
Tetema, Inama, Sikomi, Marry You, Jeje, Waah, IYO na vinginevyo vingi vinavyokosha mioyo ya shabiki wake.
Kujituma na kutokukata tamaa ameweza kupata tuzo nyingi kama ifuatavyo:
| Totals | |
|---|
| |
| Awards and nominations | | |
|---|
| Award | Wins | Nominations |
|---|
| HiPipo Music Awards | 1 | 0 |
|---|
| Top Ten Tube Music Awards | 1 | 0 |
|---|
| The Future Africa Awards | 1 | 0 |
|---|
| Nzumari Awards | 1 | 0 |
|---|
| MTV Europe Music Awards | 1 | 1 |
|---|
| MTV Africa Music Awards | 1 | 5 |
|---|
| BET Awards | 0 | 2 |
|---|
| African Muzik Magazine Awards | 1 | 4 |
|---|
| Tanzania Music Awards | 17 | 11 |
|---|
| IRAWMA Awards | 1 | 1 |
|---|
| AFRIMMA Awards | 1 | 2 |
|---|
| HIRONIMO MHAPA Awards | 0 | 1 |
|---|
| |
| Wins | 22 |
|---|
| Nominations | 28 |
|---|
Anamiliki Record label kubwa ya
WCB ambayo inavuna mafanikio makubwa na umaarufu mwingi hapa nchini Tanzania, media ya
Wasafi Tv pamoja na
Wasafi Fm, na mali nyingi za thamani ya mamilioni ya pesa ikiwemo gari aina ya Rolls Royce yenye thamani zaidi ya
$343,350, pamoja na mali nyingine za thamani kubwa nyumba za kifahari nakadhalika. Kutokana na mafanikio yake, mali na deal nyingi, unahisi
Diamond Platnumz ni tajiri kiasi gani?
Bila shaka
Diamond Platinumz ni kipenzi cha wengi. Kando na kuwa na kipaji, ni mwanamuziki anayeiheshimu kazi yake na anayechapa na kuipenda kazi yake.
Kwa sababu hii pekee, ameweza kupata mafanikio ambayo hakutarajia miaka ya nyuma. Kutokana na mafanikio makubwa tunaweza kutambua kwa nini yeye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi Tanzania.
Je, utajiri wa
Diamond Platnumz ni wa kiasi gani? Mamilion ya shabiki zake hujiuliza swali hili mara kwa mara. Utajiri wa staa huyu wa Bongo Flava ni mkubwa kulingana na mapato ya kazi zake, anavyoishi, mali na uwekezaji. Mnamo mwaka wa 2014, utajiri wa Diamond Platnumz ulikisiwa kuwa wa thamani ya dola za Marekani
$4 milion hivi sasa umeongezeka na kufikia zaidi ya
$7 Million.
Diamond Platnumz ni msanii namba moja kwa mapato mengi nchini Tanzania kutokana na mali anazomiliki.
Diamond Platnumz Net Worth.
| Net Worth: | $7 Million |
|---|
| Country: | Tanzania |
| Source of wealth: | Singer |