Utajiri/ umasikini ni akili na tabia yako

Utajiri/ umasikini ni akili na tabia yako

Nilitaka kujenga hoja lakini nimegundua uwezo wako wa kufikir ni mdogo sana
Sasa Mkuu hoja si unajenga kutokana na Mada iliyoletwa kwenye barza hii au uwezo wake mdogo wa kufikiri umepelekeaje wewe kushindwa kujenga hoja?
 
Hii mada kwa watu wa imani inapelekea kwenye kukufuru.......

Unaposema umasikini nini na Mafanikio nini.....!!!?

Umasikini ni hali ya mtu kutokumudu mahitaji yake ya msingi kwa wakati stahiki.......

Mafanikio ni kufanikisha ambacho umekatarajia kukifanya au ulipanga kukifanya kwa wakati muafaka.....

Mafanikio yanatofautiana na mtu na mtu......

Au kila mtu ana tafsiri yake ya mafanikio.......

Unaposema kuwa Umasikini ni ukosefu wa akili maana yake ni kwamba umekengeuka......

Masikini( kwa tafsiri yako) anapanga mikakati inayotumia akili kubwa sana ili kufikia Mafanikio.....na wengine mipango inafeli na kubaki hapo hapo ambapo kwa mtazamo wako uwaona masikini......
 
Sasa Mkuu hoja si unajenga kutokana na Mada iliyoletwa kwenye barza hii au uwezo wake mdogo wa kufikiri umepelekeaje wewe kushindwa kujenga hoja?
Hapa magufuli ameingiaje au ni hoja ya kisiasa
 
Umaskini ni matokeo ya siasa mbovu za watawala duniani hasa afrika
 
Mimi siamini kabisa kwamba Waliofanikiwa Kimaisha ndio wana akili kuzidi sisi akina Yakhe yaani Akina Karubandika, ninachoamini ni Kwamba ni Mapenzi ya MUNGU, maana wako watu wana haso hadi huruma lkn Mafanikio ni Ziro.
 
Ingekuwa vizuri serikali ibadilishe mfumo wa elimu kabisa.

Wengi wanakuwa wanatafuta ajira pekee sababu waliaminishwa ukisoma na ukimaliza basi utapata ajira na utakuwa na maisha mazuri.
Sasa maisha sio simple kihivyo.

Then wakiangalia muda waliotumia shuleni alafu uwaambie ukaanze biashara chini kabisa inakuwa ngumu kukubali.
 
Back
Top Bottom