Utajiri/ umasikini ni akili na tabia yako

Utajiri/ umasikini ni akili na tabia yako

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,439
Reaction score
166,897
Ukimwambia Bakhressa kuwa [HASHTAG]#mihogo[/HASHTAG] ni biashara nzuri atakuita board room muongee vizuri apate kujua vizuri lakini ukimfata msomi mwenye labda masters ya biashara ukamwambia kitu kile kile anaweza kukuona huna idea kichwani.
Nilipoona video ya [HASHTAG]#DiamondPlutnumz[/HASHTAG] akizindua biashara yake mpya ya [HASHTAG]#DiamondKaranga[/HASHTAG] nikawaza tena. Nikamforwadia mdogo wangu mmoja anasoma "ELIMU YA JUU" kwa sasa.

Alipoiangalia nikamuuliza maswali machache:
1. Hiyo ni video ya Diamond na karanga?
Akajibu [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG] BRO
2. Nikamuuliza: Diamond amechuja kimuziki ndo maana kakimbilia karanga?
Akajibu [HASHTAG]#HAPANA[/HASHTAG]
3. Nikamuuliza: Diamond alisomea biashara Chuo?
Akajibu [HASHTAG]#HAPANA[/HASHTAG]
4. Nikamuuliza: Ana akili ya kibiashara?
Akajibu [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG]
5. Nikamuuliza: Ana hela nzuri nzuri benki?
Akajibu [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG]
6. Nikamuuliza: Sasa haoni aibu kuuza karanga?
Akajibu [HASHTAG]#HAPANA[/HASHTAG]
7. Nikamuuliza: Kwa nini haoni aibu? Akajibu nadhani sababu ya pale juu NAMBA 4
Nikajisemea: Good.
8. Nikamuuliza: Wewe umesoma kuliko Diamond?
Akajibu: [HASHTAG]#NDIYO[/HASHTAG] KAKA.
9. Nikamuuliza: Unaweza kuuza karanga? ......... (KIMYA).......
10. Nikataka kuuliza tena ..nikaona "Typing......"
Jibu likaja: INATEGEMEA

Anyway mpaka hapo nikawa nimeelewa jibu sahihi ni lipi. Kwamba nikimpa huyu msomi option mbili baada ya masomo yake. Moja apate AJIRA pale Azikiwe CRDB, mshahara labda laki 9 kwa mwezi na mkopo nafuu wa kununua IST... halafu option nyingine iwe idea ya kuuza karanga kuanzia zero ipi atachagua?
Nadhani jibu wote tunalo.

Kuna binti mwingine wa "Elimu ya Juu" alikuja kwangu akiomba msaada wa kutafutiwa mahali
Hili ni [HASHTAG]#JANGA[/HASHTAG].

Tuna wasomi wetu wengi ambao wanachotaka ni AJIRA TU. Serikali nayo inadhani itaweza kutatua tatizo la ajira kwa a one-sided view. Kwamba mtu asiye na ajira dawa yake kumpa ajira. Si kweli kwamba hiyo ndo dawa pekee. In fact tuendako hiyo ni wrong solution. Mfano mdogo ajira za madereva kwa dunia ya leo zinaondoka moja moja.

Fikiria: Siku jiji hili la Dar es Salaam kwa mfano hili likiwa na Mwendokasi kila Kona ya jiji na huko mbali na city centre kote kuanzia Bunju (au Bagamoyo) hadi Mbagala na hadi huko Chalinze.

Halafu treni za umeme ziko
Halafu self driving cars
Halafu drones za kudeliver mizigo kwa wateja (yani uko zako nyumbani labda Bunju unaagiza chakula KFC Posta unalipia kwa M-PESA kinaletwa na drone ndani ya robo saa tu hadi mlangoni kwako)

Hapo mtu aliyesomea udereva ataendesha nini?
Licha ya hayo mambo kukawia yatafika. Lakini hata kabla hayajafika ajira ngapi zipo na nani atapata nani akose.

Wasomi wetu ni lazima waanze kuwaza tofauti na wasomi wa mwaka 1970. Lazima kuwaza option ya kusurvive nje ya mfumo wa ajira.

Tatizo wengi wanachotaka ni MSHAHARA tu. Ndo maana wakikutana na wewe utasikia: "BRO NIUNGANISHE BASI HATA KWA RAFIKI ZAKO NIPATE KAZI". Ndo lugha yao. NIUNGANISHE. Yaani utadhani wewe umekuwa fundi welding... Ukimpa idea nyingine HATAKI.

Ndo maana watu wasio na shule ndeefu ndo wanakuwa matajiri. Si bure. Katika matajiri wote 2000+ kwenye Forbes wenye MBA unaweza kuta hata 10 hawafiki. Na hao wenye hiyo MBA siyo kuwa ndo imewafanya wa excel in bness.

Lazima kuwaza kwa mapana. Wasomi hawataki kuumiza kichwa wanataka ready made things. Hii si njema kwa afya ya uchumi wa taifa letu.
Ukitazama [HASHTAG]#DiamondPlutnumz[/HASHTAG] na karanga unashangaa kwa nini msomi akikuona unaanzisha biashara yako anataka umpe tu AJIRA hataki umfundishe afanye.

Makanisani nako wasomi wanaombewa tu wapate AJIRA. Basi. Kweli? Ina maana hakuna MAONO mengine kwa wasomi wetu isipokuwa ajira?
Elimu ya juu kwa vijana wengi imepeleka creativity yao na uthubutu wao CHINI!
So sad!

Sikiliza kijana msomi:
Ni muhimu kuyatazama maisha yako kwa mapana na kwa upya kabisa pasipo kuyahusisha na elimu yako ya darasani kabisa.
Mungu awabariki sana.

Jifunze Kuthubutu tusiwe na kikomo cha kufikiri.
Fikiri hata mara 1000 usiochoke unapoanguka ndo inakuongezea uwezo wa kutatua Changamoto zinazokukakabili.

UNAWEZA WAKATI NI SASA.
 
gud..[emoji122][emoji122]betta..[emoji122][emoji122]best[emoji122][emoji122]..

Sent from my SM-J120F using JamiiForums mobile app
 
Hakika.

Na siku zote ukiwashauri Biashara za kubangaiza, wanakuona huwatakii mema.

Ukiwashauri japo miradi midogo, midogo kujiendeleza wakishatoka Makazini, hawatokuelewa hata kidogo.

Siku zote Biashara ndogo ndogo ndizo zinazoleta Biashara kubwa.

Hizi hizi Biashara mnazoziita za Kimachinga, ukituliza kichwa baadae/hapo mbeleni zitakuinua Kimaisha kuliko hiyo Mishahara ya Kusubiri Mwisho wa Mwezi
 
mjadala wa kujiajiri una poteza kabsa idea kubwa nayo ni kubadilisha mfumo wetu wa elimu, usiwe wa kupoteza muda na umjenge anaye toka awe na uwezo wa kujiajiri.

pia mjadala wa kujiajiri unge i lenga serikali ifanye reforms kuweka mazingira mazuri kwa private sectors na uanzishaji wa biashara.
mfano Tanzania ni ya 136 katika nchi 186 katika mazingira mazuri ya uanzishaji na uwezeshaji wa ki biashara.
ndio utakuta viongozi wetu wenye PHD wana sisitiza kujiajiri lakin wakifukuzwa kazi wanaomba kazi ingine na hawaoneshi mfano huo.

nakubaliana na mwandishi lakini tuna mengi ya kufanya ili kujiajiri kusiwe kuna vikwazo visivo lazima
 
brazaa , natoka kusoma naingia jf nakutana na huu uzi wa kwanza mzuri wa namna hii, ya nikweli nasoma chuo kikuu huwa nawaza sana about my future, i knw my future is largely unknwn, mm ni mtt wa kiume i knw ipo siku mama ataniomba mm pesa, ndoto ni nyingi lakini vikwazo ni vingi zaidi, mwanamke asipopata kazi ataolewa how about mwanaume,,?? nmepata somo kwako.
 
Hakuna kitu hapo
Mond hakuanza na kuuza njugu kwanza

Sent from my SM-C5000 using JamiiForums mobile app
 
Bandiko safi kabisaa, limeandikwa na mtu mwenyw uelewa mzuri na mkubwa kabisaa, safi sana mkuu, i got you.
 
Aisee ni kweli mzee

Nimeanza kumuelewa jamaa yangu mmoja anachukua bachelor ya mambo ya afya mwaka wa 3 lkn tukiongea maswala ya maisha ananiambia "boy shule inanichelewesha sana mimi nashona vizuri sana,naikumbuka cherehani yangu home mpk naumwa nikimaliza chuo naifufua cherehani yangu ajira zina stress nisizoziweza"

Mara kwanza nilidhani analeta masihara wala sikumtilia maanani lkn kashanambia ilo jambo zaidi ya mara 4 sasa tena tukiwa siriaz tukijadili ni jinsi gani tunaweza kuyamudu maisha na kwa kuwa alishafanya kidogo hiyo ishu kipindi amemaliza A level kwa michanganuo anayonipa ana uhakika cherehani ita mpush zaidi kuliko ajira baada ya chuo,ananiambia anasoma ili asije jutia fursa ya elimu hapo baadae coz yupo vizuri pia kichwani na boom linatema kila baada ya miezi miwili lkn ndoto yake ni kucheza na cherehani kwani anaamini ina maslahi zaidi

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom