Utajiri/ umasikini ni akili na tabia yako

Utajiri/ umasikini ni akili na tabia yako

Akiwa na miaka 5 Alifiwa na Baba yake,
Akiwa na miaka 16 aliamua kuacha shule,
Akiwa na miaka 17 tayari alikua kapoteza ajira 4,
Akiwa na miaka 18 aliamua kuoa,
Akiwa na miaka kati ya 18-22, alikua msimazi wa
njia za reli lakini alishindwa,
Alijiunga na Jeshi lakini aliondolewa,
Akatuma maombi shule ya sheria ila hakupata
nafasi,
Akawa muuzaji wa Bima lakini alishindwa pia,
Akiwa na miaka 19, alifanikiwa kuwa Baba,
Akiwa na miaka 20, Mke aliamua kuondoka na
mtoto,
Hatimaye Akawa mpishi na mwosha vyombo wa
mgahawa mdogo,
Alishindwa hata katika jaribio la kumteka mwanae,
na kuamua kumshawishi mkewe kurejea nyumbani,
Akiwa na miaka 65 alistaafu,
Siku moja baada ya kustaafu alipata mafao yake
kutoka serikalini kama Tsh 231000 (105$),
Alidhani serikali imemuona kama hajiwezi kabisa,
Akafanya jaribio la kujiua, akiamini hakuna thamani
ya kuishi tena, na kwamba ameshashindwa sana,
Akaamua kukaa chini ya mti na kuandika matarajio
yake, Ila aliona ayaandike yale aliyoyakamilisha
tayari,
Akagundua kuna mambo mengi hakuyafanya bado,
Akagundua lipo jambo moja ambalo anaweza
kulifanya zaidi kuliko mtu yeyote yule
anayemfahamu,
Na Ilikua ni namna gani ya Kupika,
Akaamua kuchukua Tsh 191400 (87$) kutoka
kwenye Hundi yake na kununua kuku na
kuwakaanga akiwachanganya na mchanganyiko wa
aina yake,
Akaamua kupita mlango kwa mlango kuwauza kwa
majirani zake huko Kentucky,
Kumbuka akiwa na miaka 65 alikua tayari kujiua
lakini akiwa na miaka 88 Colonel Sanders,
Mwanzilishi wa Kentucky Fried Chicken ( KFC)
Alikua tayari ni Billionaire ($)
Haujakawia kuanza Upya bado.... Kitu kikubwa ni
"Mtazamo" ( Attitude).
Usikate tamaa .... Haijalishi mambo ni magumu kiasi
gani.
Una kila kitu cha kukufanya Ufanikiwe, Amua
kubadilisha mtazamo ili kubadili Stori yako.
 
Bill Gates ni mwekezaji wa marekani, Programa wa kompyuta, Mwekezaji na mwenyekiti wa zamani wa Microsoft (Kampuni kubwa ya programu duniani). Tangu mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3.

Unaweza usijue lakini kila sekunde Bill Gates anainginza takribani dola 250 za kimarekani, Na kwa dakika nzima anaingiza takribani dola 15000. Unashangaa??. Kwa kukushangaza zaidi, endelea kusoma mambo 16 ya ukweli wa kuvutia kuhusu Bill Gates

1. Bill Gate alianza kuandika program za kompyuta alivyokua na umri mdogo (miaka 13). na programu yake ya kwanza ilikua ni game ya ‘tic tac toe’ amabayo mchezaji alikua anacheza na kompyuta

2. Alijua atakua milionea siku moja. Hii ilimpelekea mpaka kujisifia mbele ya mwalimu wake. Bill Gates alitabiri atakua milionea akiwa na miaka 30 lakini akawa bilionea akiwa na miaka 31.

3. Aliuza ‘software’ yake ya kwanza akiwa na miaka 17 kwa dola 4200 za kimarekani kwa shule ya sekondari na ilikua ni ratiba ya shule.

4. Alishinda maksi 1590 kati ya 1600 kwenye SAT (Scholastic Aptitude Test). Matokea hayo ya 1590 yalikua yanajumuisha IQ ambayo alikua na alama 170. Baadae kulingana na matokeo yake, chuo kikuu cha Havard kilimsajili.

5. Bill Gates ni mmoja kati ya wale walioacha shule! Aliacha chuo katika miaka yake ya mwisho. Hata hivyo mwaka 2007 alipata Degree yake kutoka Havard. Hii ni pale Chuo cha Havard kilipompa Degree ya kuheshimiwa kwa mambo alioyafanya.

6. Aligundua Microsoft katika umri wa miaka 20, yeye na Paul Allen mnamo Aprili 4, mwaka 1975. Mpaka sasa Microsoft ndio kampuni kubwa ya software duniani

7. Mmoja kati ya wakubwa wa kampuni alisema baada ya kumuonyesha gemu Bill Gates na kumfunga kwa pointi 37 na Bill akiwa na pointi 35. Alivyokutana nae mwezi uliofuata, Bill alishinda au kutoa Dro kwa michezo yote waliocheza kwenye gemu hiyo hiyo. Katika huo mwezi mmoja aliisoma hiyo gemu.

8. Bill Gates alitangaza kuwa hatawaachia wanawe utajiri wake ila atawapatia kila mmoja dola milioni 10 za kimarekani (watoto wapo wa 3) kati ya utajiri wake wa dola bilioni 72 za kimarekani.

9. Tangu Mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3 akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 58 za kimarekani. Mwaka huo Bw. Warren Buffet ndio alikua mtu namba mmoja akiwa na utajiri takribani dola za kimarekani bilioni 62 akifuatiwa na Bw.Carlos Slim akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 60 za kimarekani

10. Kama Bill Gates angekua ni nchi, basi angekua ni nchi ya 37 kwa utajiri duniani!

11. Bill Gates anaweza akagawa Dola 15 za kimarekani kwa kila mtu duniani na bado akabakiwa na dola milioni 5 za kimarekani mfukoni.

12. Kama akiangusha dola 1000 za kimarekani hana haja ya kuziokota kwa sababu ndani ya sekunde 4 ambazo angeweza kuziokota angekua tayari ameshazirudisha.

13. Kama ukizibadili (change) hela za Bill kuwa katika noti ya dola 1 ya kimarekani utaweza kutengeneza bara bara ya kutoka duniani hadi mwezini mara 14 kwenda na kurudi.

14. Gates ameokoa maisha zaidi ya milioni 5 kwa kuchangia zaidi ya nusu ya utajiri wake kwenye chanjo na sehemu zinazohusika na afya za watoto.

15. Bill ana miaka 40 sasa. Tukichukulia kwamba ataishi miaka 35 zaidi, itamlazimu kutumia japo dola milioni 6.78 za kimarekani kwa siku ili amalize hela zake zote kabla hajaenda peponi (ha!)

16. Ukiachana na kompyuta, pia Bill Gates ni muandishi. Mpaka sasa ana vitabu viwili amabavyo ni ”The Road Ahead'” na ‘Business at the Speed of Thought’.
 
Warren Buffett alizaliwa mwaka 1930 katika mji wa Omaha, Nebraska, Marekani. Baba yake mzazi Howard Buffett, alikuwa akiuza dhamana katika benki ya Union Street, Omaha 1931.

Benki hiyo ambayo baba yake alikuwa ameajiriwa ilianguka na kufilisika hivyo kujikuta hana ajira na kupoteza akiba yote. Baba yake aliamua kuanzisha biashara ya udalali wa dhamana, huku akimsihi mwanae kusoma zaidi.

Warren Buffett alipokuwa shule ya sekondari aliwaeleza wanafunzi wenzake kuwa atakuwa milionea kabla ya kufikia umri wa miaka 35. Na alifanikiwa kuwa na dola milioni 6 alipofikia miaka hiyo 35. Warren alisoma shahada ya uzamili ya uchumi katika Chuo kikuu cha kolombia.

Alijiunga na chuo hiki kwa kuwa alitaka afundishwe na mwalimu bigwa wa masuala ya uwekezaji, Benjamin Graham. Alipomaliza shahada ya pili, alijiunga katika biashara ya mwalimu wake Benjamin Graham. Akiwa chini ya mwalimu wake huyo aliweza kujifunza zaidi masuala ya uwekezaji.

Watu wengine alioweza kujifunza zaidi kutoka kwao ni Charlie Monger, Philip Fisher, Lawrence N. Boomberg, John B. Williams, Edga Smith, na John M. Keynes. Katika wote hao aliweza kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na uwekezaji katika soko la fedha na masuala ya hisa.

Akiwa kijana mdogo sana, alipita mitaani kuuza kinywaji cha Coke, akibisha hodi nyumba kwa nyumba na kuweka akiba kwa kila fedha aliyokuwa akipata na hapo akiwa na umri wa miaka 6. Alinunua chupa moja ya Coke kwa senti 25 na kuuza kwa senti 50.

Akiwa na umri wa miaka 11, alinunua hisa yake ya kwanza, hisa tatu (3) za kampuni ya Cities Service, kwa dola 38. Hisa zilishuka bei na kufikia dola 25, lakini hakubabaika katika hilo. Aliuza hisa zake baadaye na kupata faida ya dola 5. Lakini baadaye hisa hizi alizouza zilipanda bei na kufikia dola 200.

Alipofikia miaka 19, alianzisha biashara ya kuuza magazeti kwa chini ya saa mbili kwa kupitia mtandao wa kibiashara aliouanzisha na kujipatia dola 175 kwa mwezi, aliuza takribani magazeti 500 kila siku. Pia alijishughulisha na kuuza mipira ya gofu iliyopotea ili kuendelea kuongeza kipato chake. Aliwahi kumiliki gari ya Roll Royce kwa ubia na kujipatia dola 35 kwa siku.

Warren Buffett aliamua kuanzisha kampuni yake ya Berkshire Hathaway baada ya kugundua kuwa haitoshi kujifunza biashara kwa kusoma kitabuni au kuhudhuria kozi tu bali kwa vitendo zaidi.

Hadi hapo alikuwa amefanikiwa kusoma kitabu maarufu cha uwekezaji (The Intelligent Investor), kitabu anachokiri hadi kesho kuwa kilimfungua maisha yake kuhusu uwekezaji mwaka 1950, hapo akiwa bado na miaka 19.

“Price is what you pay. Value is what you get.” -Warren Buffett
Alipotoka shuleni, alipenda sana kusoma magazeti yenye habari ya soko la hisa la Marekani (Wall street journals) na taarifa za mwaka za makampuni mbalimbali. Alisoma zaidi ya vitabu 100 vya uwekezaji kwa kipindi kifupi.

Hata walimu wake shuleni, walipenda sana kumuuliza na kumwomba ushauri kuhusu uwekezaji. Pamoja na kupenda kusoma taarifa kuhusu masoko ya hisa na dondoo motomoto, majedwali na michoro hayakwenda vizuri sana. Hakuwa na mbinu na mikakati madhubuti ya uwekezaji mpaka alipompata mwalimu wake Benjamin Graham wa Chuo Kikuu cha Kolombia, mwaka 1950.

Warren Buffett alikuwa na bidii shuleni na kupata alama za juu A+ wakati akisoma shahada ya pili ya uzamili ya uchumi. Mwaka 1958 alinunua nyumba yake ya kwanza kwa dola 31,500 na bado anaishi katika nyumba hiyo hadi hivi leo. Ni mmiliki wa kampuni ya Berkshire Hathaway.

Ni kati ya wakurugenzi watendaji wanaolipwa mshahara mdogo kwa mwaka dola 100,000 ukilinganisha na wakurugenzi wengine katika makampuni mengine makubwa duniani. Hupenda kula katika hoteli za kawaida kuliko kwenda hoteli za kifahari, na kinywaji chake akipendacho cha Coke.

Warren siyo mfuja fedha na hana matumizi mabaya ya fedha na mojawapo ya tabia yake ni kuwa “fedha ni lazima ihifadhiwe na kutunzwa vizuri (preservation of capital).’ Aliwahi kutoa takribani dola bilioni 30 kwa Bill na Melinda Gates Foundation kusaidia miradi ya maendeleo.

Hadi hivi sasa Warren Buffett ni tajiri wa tatu duniani akiwa ana utajiri unaofikia $60.8 Bilioni kwa mujibu wa jarida la Forbes la nchini Marekani. Nakumbuka siku moja nilisoma kijana mmoja aliwahi kumuomba ushauri afanye kitu gani ili aweze kufanikiwa, Warren Buffett alimwambia asome kurasa (pages 500) kwa siku.

Hii ni wazi kuwa Warren anatuonesha umuhimu wa kusoma vitabu kama sehemu mojawapo ya kupata ufahamu na taarifa nyingi za kuweza kukusaidia kufanikiwa. Kama Warren anasoma kurasa 500 kwa siku pamoja ana kazi kubwa ya kuendesha kampuni aliyonayo, Jiulize mimi na wewe tunasoma kurasa ngapi kwa siku?

Mambo 5 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Warren Buffett:
1: Umri wako mdogo si kigezo cha kuacha kuifata ndoto yako na kuitimiza.
Wapo watu wengi huwa wanaona kama kuna muda fulani maalum kwa ajili ya kutimiza ndoto zao walizonazo, wengine wanaamini umri wa kufanikiwa ni kuanzia miaka 45 au 50 nakuendelea.

Wapo wanaoamini kuwa milionea au bilionea kwenye umri mdogo ni kitu kigumu sana, hapana. Warren Buffett akiwa na miaka 35 alikuwa tayari amefanikiwa kutimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuwa milionea. Unachopaswa kuelewa ni kufahamu unataka nini kwenye maisha yako, simamia kitu unachokipenda na shikilia ulichonacho hadi uone matokeo yakitokea juu yake. Usikubali umri uwe kikwazo cha kutimiza maono na ndoto yako kubwa uliyonayo katika maisha yako.

Kijana wa kimarekani Evan Spiegel ambaye ni mwanzilishi na mmiliki wa Snapchat ni miongoni mwa vijana wadogo duniani akiwa na umri wa miaka 25 hadi sasa, lakini ni miongoni mwa mabilionea duniani, mwenye utajiri unaofikia dola 2.1 bilioni (zaidi ya trilioni 5.2) na kumfanya kuwa kijana mdogo mwenye pesa nyingi zaidi.

Mara baada ya kusoma katika shule ya crossroads, akamalizia elimu yake katika Chuo cha Stanford kilicho nchini Marekani. Baada ya kuona mitandao ya kijamii ikishika kasi, akamua kuungana na mwenzake Bobby Murphy kwa ajili ya kutengeneza mtandao wao wa kijamii wa Snapchat ambao umekuwa maarufu duniani kwa sasa. Umri wako si kigezo cha kushindwa kufuata na kutimiza ndoto zako, amini unaweza na amka leo kuifata ndoto yako pasipo kusubiri kesho.

2: Tafuta maarifa na taarifa sahihi juu ya eneo unalotaka kufanikiwa.
Mara nyingi watu wengi wamejaribu kuingia kufanya biashara au uwekezaji fulani pasipo kupata taarifa sahihi zenye kuweza kuwasaidia katika kufanikiwa vyema katika maeneo hayo.

Hii ndio sababu ya watu wengi kuishia njiani na kushindwa kufanikiwa katika vitu vingi wanavyoanzisha na kuanza kufanya. Warren Buffett alijifunza uwekezaji wa Hisa baada ya kujenga tabia ya kusoma vitabu zaidi na mojawapo ya vitabu alivyovisoma na kumpa maarifa aliyokuwa akitaka, The Intelligent Investor, Security Analysis, na Common Stock and Uncommon profits .

Jiulize ni mara ngapi umetoa muda wa kujifunza au kutafuta ujuzi fulani kwa ajili ya kufanikisha malengo na ndoto yako kubwa uliyonayo?
Kwa mara ya kwanza nilishangaa sana kusikia Warren Buffett anasoma kurasa 500 kwa siku. Hii ni wazi tajiri huyu anafahamu umuhimu wa maarifa katika kumsaidia kufanikisha malengo yake aliyonayo.

Watu wengi wanaotaka kufanikiwa leo hii si wepesi wa kujitoa katika kutafuta maarifa na taarifa sahihi kwa gharama yoyote ili kujijenga kiufahamu katika vitu wanavyotaka kuvifanya. Jiulize mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni lini?

Huwezi kuvuka eneo moja kwenda eneo jingine kwa kupitia ufahamu au maarifa yale yale uliyokuwa nayo tangu mwaka jana.
“Some people dream of success, while others wake up and work hard at it.” -Mark Zuckerberg

3: Kuwa karibu na watu wenye uwezo kwa ajili ya kukuongoza na kukushauri.
Kuwa karibu na watu wenye uwezo na uzoefu kuliko wewe kunaweza kukusaidia katika kukupa mbinu nyingi zaidi za kukuwezesha kuvuka vikwazo na changamoto kwa wepesi ili kufanikisha ndoto yako.

Usijaribu kutafuta mchawi wa mafanikio yako kwa kujaribu kufanya kila kitu peke yako, ili uvuke changamoto zinazoonekana ni ngumu kwako ni vizuri zaidi utafute watu walio na uwezo na uzoefu kuliko wewe ili wakushauri mara kwa mara katika kitu unachotaka kukifanya. Jifunze kuwa na mshauri (mentor) kwenye kila eneo unalotaka kufanikiwa katika maisha yako.

4: Ili ufanikiwe kifedha unahitaji kuwa mwangalifu katika matumizi yako ya fedha ya kila siku.
Warren Buffett hakutokea familia yenye uwezo sana ila baba yake alikuwa mfanyakazi wa benki kabla benki hiyo haijafilisika na kutafuta kazi nyingine ya kufanya ili kujipatia kipato.

Akiwa na miaka 6 Warren ndio alipoanza kuzunguka mitaani na kuuza kinywaji cha Coke, na kila fedha aliyoipata alijifunza kuihifadhi kwa kuweka akiba hadi pale alipotimiza miaka 11 akaanza kununua hisa.

Hii inatuonesha wazi kuwa Warren Buffett alikuwa ni kijana smart na mwangalifu sana katika matumizi yake ya fedha na hiki ndio kitu kilichomsaidia kufikia kuwa milionea akiwa na miaka 35 kama alivyowatamkia wenzake akiwa shuleni.

Leo hii jiulize ni mara ngapi unapopata fedha baada ya kujishughulisha na kitu fulani unachofanya huwa unaheshimu na kutumia fedha zako kwa matumizi muhimu ili kutoa nafasi ya kuweka akiba na kuongeza thamani ya fedha yako kuongezeka. Usipojifunza namna nzuri ya matumizi ya fedha zako utabaki kuota ndoto za utajiri pasipo kuona uhalisi wowote katika maisha yako.

Hakuna utajiri anaoweza kuupata mtu nje ya nidhamu anayoweza kuijenga katika matumizi yake ya fedha. Jifunze kuweka akiba na kujua njia nzuri za kuwekeza fedha zako mahali sahihi palipo na faida ili kukutengenezea utajiri mkubwa.

5: Jifunze kutoa kuliko kupokea.
Warren Buffett inakadiriwa ndio tajiri aliyewahi kuweka historia ya kurudisha fedha nyingi zaidi kwa jamii baada ya kutoa takribani dola bilioni 30 kwa Bill na Melinda Gates Foundation kusaidia miradi ya maendeleo.

Hii ni wazi kuwa tajiri huyu anafahamu siri kubwa ya kufanikiwa zaidi ni kurudisha kwa jamii kile alichonacho. Kumbuka ili ufanikiwe zaidi unahitaji kujifunza namna ya kutoa kuliko kupokea tu. Kutoa ni pamoja na kidogo ulichonacho sasa, usisubiri ufanikiwe kama Warrren Buffett ndio uanze kujifunza kutoa.

Anza kujenga tabia ya kutoa kuanzia sasa ili utakapofanikiwa kesho watu wengi wazidi kufaidi matunda ya kufanikiwa kwako.
JIAMINI NA AMINI UNAWEZA. ISHI NDOTO YAKO.
 
Hakuna kitu hapo
Mond hakuanza na kuuza njugu kwanza

Sent from my SM-C5000 using JamiiForums mobile app
Perfecto bro...watu wanakurupuka tu humu.

Kuna tofauti kubwa ya kufanya biashara ukiwa na capital na connection at hand na ukiwa hauna. Jina pia.

Huyo mondi angeuza hizo Karanga before tumuone, mbona aliishia kuuza vimitumba na kucheza shoo kwenye mabaa.

Tusichanganye pia mafanikio na umuhimu wa elimu na pesa, ni vitu tofauti sana.

Nina Shangazi yangu ameuza sana karanga, baba yangu Mdogo pia anafanya biashara hiyo na ana machine pia ya kukoboa karanga, lakini maisha yao ni kawaida sana. Wengi tu wanauza Karanga huko mtaani..

In that case basi watu wote wakaimbe muziki kisa diamond kapata vijisenti kwenye muziki, hahahaaa

Inafika mahali wasomi wanakuwa na role model class 7 kisa kapata vijisenti vya unga kwa mgongo wa muziki, ni aibu kubwa. In that case basi shule zifungwe tu watu waingie kwenye biashara.

Kila MTU ana njia zake za kupata mafanikio ya pesa.

Hayo ni mawazo muflisi kabisa kwa upana wa maono yangu


Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Perfecto bro...watu wanakurupuka tu humu.

Kuna tofauti kubwa ya kufanya biashara ukiwa na capital na connection at hand na ukiwa hauna. Jina pia.

Huyo mondi angeuza hizo Karanga before tumuone, mbona aliishia kuuza vimitumba na kucheza shoo kwenye mabaa.

Tusichanganye pia mafanikio na umuhimu wa elimu na pesa, ni vitu tofauti sana.

Nina Shangazi yangu ameuza sana karanga, baba yangu Mdogo pia anafanya biashara hiyo na ana machine pia ya kukoboa karanga, lakini maisha yao ni kawaida sana. Wengi tu wanauza Karanga huko mtaani..

In that case basi watu wote wakaimbe muziki kisa diamond kapata vijisenti kwenye muziki, hahahaaa

Inafika mahali wasomi wanakuwa na role model class 7 kisa kapata vijisenti vya unga kwa mgongo wa muziki, ni aibu kubwa. In that case basi shule zifungwe tu watu waingie kwenye biashara.

Kila MTU ana njia zake za kupata mafanikio ya pesa.

Hayo ni mawazo muflisi kabisa kwa upana wa maono yangu


Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
Hapo kwenye wasomi kua na ma role model wa darasa la 7 umeongea ukweli mtupu.
 
Perfecto bro...watu wanakurupuka tu humu.

Kuna tofauti kubwa ya kufanya biashara ukiwa na capital na connection at hand na ukiwa hauna. Jina pia.

Huyo mondi angeuza hizo Karanga before tumuone, mbona aliishia kuuza vimitumba na kucheza shoo kwenye mabaa.

Tusichanganye pia mafanikio na umuhimu wa elimu na pesa, ni vitu tofauti sana.

Nina Shangazi yangu ameuza sana karanga, baba yangu Mdogo pia anafanya biashara hiyo na ana machine pia ya kukoboa karanga, lakini maisha yao ni kawaida sana. Wengi tu wanauza Karanga huko mtaani..

In that case basi watu wote wakaimbe muziki kisa diamond kapata vijisenti kwenye muziki, hahahaaa

Inafika mahali wasomi wanakuwa na role model class 7 kisa kapata vijisenti vya unga kwa mgongo wa muziki, ni aibu kubwa. In that case basi shule zifungwe tu watu waingie kwenye biashara.

Kila MTU ana njia zake za kupata mafanikio ya pesa.

Hayo ni mawazo muflisi kabisa kwa upana wa maono yangu


Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
Wangapi wana mitaji na hawafanyi biashara nyingine yoyote apart from sanaa? Kuwa na side businesses kuna ongeza financial freedom
 
Haya mambo tuyachukulie kiutu uzima aisee...sio tunasoma tu vitabu af tunakuja tu humu nakutafsiri mambo tunayosoma kwa vitabu.Hakuna mtu ambaye hataki kujiajiri ....trust me on this.Tatizo linakuja kwenye mtaji.We unasema hakuna msomi ambaye hawezi kuuza karanga??...kwa nini mnapenda kudanganya umma?...Huyo Diamond unaemuelezea unadhan anaeza kaa barabarani jua kali kuuza karanga.Usitegemee mtu mwenye degree akae barabarani eti auze karanga eti au awe anazibua vyoo...thats unrealistic!...Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila msomi anapata ajira.Nchi zilizoendelea unaona wasomi wanalipwa allowance na serikali if at all ana academic papers lakini ajira bado ajapata.Leo tunataka eti kila ambae amesoma ajiajiri....sidhani kama hiyo kitu ni sahihi bali porojo za wanasiasa kukwepa wajibu wao kwamba kila mtu msomi ana haki ya kupata ajira whether private or public sector.Nachukia sana msemo kwamba wahitimu wa vyuo eti wajiajiri.Unataka aende azibue vyoo kama aloishia darasa la saba?....

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Haya mambo tuyachukulie kiutu uzima aisee...sio tunasoma tu vitabu af tunakuja tu humu nakutafsiri mambo tunayosoma kwa vitabu.Hakuna mtu ambaye hataki kujiajiri ....trust me on this.Tatizo linakuja kwenye mtaji.We unasema hakuna msomi ambaye hawezi kuuza karanga??...kwa nini mnapenda kudanganya umma?...Huyo Diamond unaemuelezea unadhan anaeza kaa barabarani jua kali kuuza karanga.Usitegemee mtu mwenye degree akae barabarani eti auze karanga eti au awe anazibua vyoo...thats unrealistic!...Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila msomi anapata ajira.Nchi zilizoendelea unaona wasomi wanalipwa allowance na serikali if at all ana academic papers lakini ajira bado ajapata.Leo tunataka eti kila ambae amesoma ajiajiri....sidhani kama hiyo kitu ni sahihi bali porojo za wanasiasa kukwepa wajibu wao kwamba kila mtu msomi ana haki ya kupata ajira whether private or public sector.Nachukia sana msemo kwamba wahitimu wa vyuo eti wajiajiri.Unataka aende azibue vyoo kama aloishia darasa la saba?....

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
you got it right

Sent from my SM-A800F using JamiiForums mobile app
 
Good point naanza kuuza majaksi a.k a karanga hapa stand

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
unakuta mtu katumia zaidi ya nusu ya maisha yake akiwa shule (msingi 7yrs, Sec. 6yrs, Univ. 3yrs. = 16), umri wake ni miaka 30.
Lakini sasa, they're complaining on anything and everything. Huwa nashindwa kuelewa.
 
mjadala wa kujiajiri una poteza kabsa idea kubwa nayo ni kubadilisha mfumo wetu wa elimu, usiwe wa kupoteza muda na umjenge anaye toka awe na uwezo wa kujiajiri.

pia mjadala wa kujiajiri unge i lenga serikali ifanye reforms kuweka mazingira mazuri kwa private sectors na uanzishaji wa biashara.
mfano Tanzania ni ya 136 katika nchi 186 katika mazingira mazuri ya uanzishaji na uwezeshaji wa ki biashara.
ndio utakuta viongozi wetu wenye PHD wana sisitiza kujiajiri lakin wakifukuzwa kazi wanaomba kazi ingine na hawaoneshi mfano huo.

nakubaliana na mwandishi lakini tuna mengi ya kufanya ili kujiajiri kusiwe kuna vikwazo visivo lazima
Hata ukijiajiri kwa kulima huruhusiwi kuuza nje kwenye bei nzuri, unalazimishwa kuuza ndani ya nchi ambako unapata kafaida kadogo au hasara. Wakati huo huo tuna import nyama hadi matunda.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom