Utajibuje swali hili kwenye interview?

Utajibuje swali hili kwenye interview?

Jibu la hivi sitoi hata siku moja.
Yaani sijui nini ninataka! Siku zote nilizoenda kwenye interview nilikuwa na namba yangu kichwani.
Naomba mnilipe kutokana na salary scheme ya shirika inavyosema kulingana na elimu yangu
 
Hii ndio namna ya kujibu swali hilo;

  1. Kwanza kabla ya kwenda kwa interview fanya utafiti mdogo kujua kwa wastani watu wanofanya kazi kama hiyo huwa wanlipwa kiasi gani
  2. Fuatilia pia hali ya kampuni unayoenda kufanya kazi we unavoona huwa wanalipa kiasi gani
  3. Angalia mshahara unaolipwa sasa hivi ni kiasi gani
  4. Angalia gharama za maisha yako kulingana na life style mfano rent,meals,transport na majukumu mengine unaweza ukahitaji kiasi gani kwa mwaka
  5. Ukishapata hizo data chukua kubwa kabisa zidisha mara mbili halafu toa ndogo kabisa Jibu linalobaki kama ni chini au sawa na mshahara ambao wao wanalipa basi watajie hio au inayozidi hapo kwa 10-20% na iwapo ni kubwa kulika msharaha wanaolipaga kwa mujibu wa taarifa zako basi taja sawa au pungufu 10-20% ila jambo la muhimu usisahau kusema I am open to negotiation na itategemea na other benefits za kwenye mkataba mf,bima ya afya,transport,na alowances nyingine ambazo zitakuwepo kwenye mkataba
 
1. Ni vizuri ujue kwenye industry hyo watu wa level yako wanalipwaje kisha waambie hiyo Range.
2. Mshahara haujawahi kuwa tatizo ninachohitaji ni pesa ya kukidhi mahitaji yangu yatayofanya utendaji kazi wangu kuwa rahisi,
3. Nilipe kutokana na viwango vyenu mlivyopanga kwa kuzingatia uzoefu na kiwango cha elimu.

Jibu kizungu utakuwa umetisha

Mfano - umesema mult lateral, case study coca cola

Hawa wanalipwa 1.5 - 2M muhasibu mwenye degree na experience Ya miaka 2 nakuendelea

" you may pay me one point eight million as Sector range but the door is open for negotiation"

"Salary had not become a problem to me. what's matter is an experience and my career development , you may pay any salary that may smooth daily working activities as you see it may fits"

1. "You may pay me between 1.8 million and 2.5 million as a sector range, but the door is open for negotiation"

2. "Salary has never been a problem for me. What matters is the experience and career development I will get while working with you. You may pay me any salary that may make for a smooth working environment as you see fit."
 
kiasi ambacho ninyi mmepanga, na kinalingana na kazi yangu
Ukijibu hivo imekula kwako sanaaa. Kumbuka mshahara unawekwa kwenye mkataba, sasa watajuaje kazi yako wakati unasain kabla hata ya kuanza kazi yenyewe.
Jibu sahihi LA swali hilo Ni kufanya utafiti angalau kabla hunaenda kweny usaili ujue mishara ya kampun hiyo inarange wwapi, hata Kama Si exactly. Then kweny usaili taja amount kabisa halafu malizia kwa kusema Ni negociable. Mwajari huwa anataka kuona unajiamini vipi pia,
 
Jana nilikuwa kwa interview na Multnational Company moja hivi na mwisho wa interview nikaulizwa:

"UNGEPENDA ULIPWE MSHAHARA WA SHILINGI NGAPI?"

Nimependa kushare nawewe, Ungejibu je swali hilo?
Mkuu hapa watu wengi hujibu kwa uoga wa kunyimwa kazi ila infact maana ya swali hili ni to show your real price,usiogope kutaja kiasi. Kiasi hapa kinatofautiana kulingana na type of job, your experience, level ya ajira unayoomba(junior or senior post) etc. Ila ni vzr km utaweza kujua kwa kudadisi kabla ya interview mtu wa nafasi hiyo analipwa kiasi gani kwny kampuni husika. Ushauri wangu tell the figure then be prepared to defend it,watu wengi wanaliaga kazi ngumu,mshahara mdogo ila walipoulizwa wakijibu nyie nikadirieni tu. Na baadhi ya companies unaweza kukosa kazi kwa kutojua price yako maana yake hujielewi.
 
Back
Top Bottom