Utajibuje swali hili kwenye interview?

Utajibuje swali hili kwenye interview?

Jana nilikuwa kwa interview na Multnational Company moja hivi na mwisho wa interview nikaulizwa:

"UNGEPENDA ULIPWE MSHAHARA WA SHILINGI NGAPI?"

Nimependa kushare nawewe, Ungejibu je swali hilo?
I know your company/Organisation is reputable one,you have set your cake,I don't think if I can break your cake. Ndivyo nilivyojibu walicheka panel nzima.
 
Wengine majibu mloweka hapo juu sio sawa, waajiri wengi wanapenda mwajiriwa awe specific, so kwanza jua wenye elimu kama yako wanalipwa sh ngapi then taja kiasi hicho.
 
1. Ni vizuri ujue kwenye industry hyo watu wa level yako wanalipwaje kisha waambie hiyo Range.
2. Mshahara haujawahi kuwa tatizo ninachohitaji ni pesa ya kukidhi mahitaji yangu yatayofanya utendaji kazi wangu kuwa rahisi,
3. Nilipe kutokana na viwango vyenu mlivyopanga kwa kuzingatia uzoefu na kiwango cha elimu.

Jibu kizungu utakuwa umetisha

Mfano - umesema mult lateral, case study coca cola

Hawa wanalipwa 1.5 - 2M muhasibu mwenye degree na experience Ya miaka 2 nakuendelea

" you may pay me one point eight million as Sector range but the door is open for negotiation"

"Salary had not become a problem to me. what's matter is an experience and my career development , you may pay any salary that may smooth daily working activities as you see it may fits"
Majibu yako ni mazuri sana ila Kiingereza chako kitakukosesha kazi.

Jibu Kiswahili kama ukiruhusiwa.
 
Kuna namna 2 kama sio tatu za kujibu swali hili.
Mosi: Nilipwe kulingana na taratibu zenu, am lready .
Pili: Nilipwe kati ya elfu NNE mpaka nane. Ila hili ni mpaka ufanye kauchunguzi ujue taasisi inalipaje kwa kada yako . hapa utaenda chini na juu usitaje fixed itapendeza
 
Wengine majibu mloweka hapo juu sio sawa, waajiri wengi wanapenda mwajiriwa awe specific, so kwanza jua wenye elimu kama yako wanalipwa sh ngapi then taja kiasi hicho.
Hii itategemea na hali ya huyo anayetafuta kazi, kuna mwingine hana ajira na ameshakula msoto wa nguvu hata laki tano yuko radhi,sasa anaogopa kutaja nyingi akaachwa
 
Majibu yako ni mazuri sana ila Kiingereza chako kitakukosesha kazi.

Jibu Kiswahili kama ukiruhusiwa.
Ndio tunajifunza Boss. Embu nitoe tongotongo ili tuzipe thamani hzi points tena ni nzuri kama ikiwa kizungu maana swala la lugha linazingatiwa sana
 
Jibu la kuonyesha kwamba kiwango cha mshahara hakiwezi kuwa deal breaker at least kwa hatua hii - ni la msingi sana. Hasa kama huna idea ya viwango vya mishahara ya taasisi husika.
 
Lazima uwe na majibu mawiki kuchwani, na ili kuyapata kabla ya kuomba kuomba kasi lazima utafiti kiwango cha mshahara wanacholipwa watu wa nafasi kama yako hapo.

So, jibu la kwanza, ni "Nilipwe kulingana na salary scheme ya kampuni"

Wanaweza kukuambia hatuna hiyo scheme, taja kiasi, ndio unawapa jibu la pili, taja kiasi kadri ya utafiti wako na wape option ya kukuongezea kadri ya ufanisi wako wa kazi, ujuzi na elimu.
 
Kwa mwezi huu wa kwanza ntafanya kazi bure....mwezi wa pili tutakaa mezani ili mnilipe kutokana na productivity yangu kwenye kampuni.
 
Ndio tunajifunza Boss. Embu nitoe tongotongo ili tuzipe thamani hzi points tena ni nzuri kama ikiwa kizungu maana swala la lugha linazingatiwa sana

Ngoja tumalize kuhani msiba wa Manchester united mkuu, nakuahidi kurudi hapa.
 
huu uzi mtamu sana!!

hapo unatakiwa ufanye utafiti wa mshahara wanaolipwa wafanyakazi kwenye hilo kampuni

kisha..

kwenye interview unatakiwa utaje mshahara wa chini pia unataja mshahara wa juu unaopendelea!!
 
Ni serious issue hii....mimi yaliwahi nikuta nikawaambia wanilipe according my education wakagomea hilo jibu wakanilazimisha niwe specific
 
Back
Top Bottom