Utajibuje swali hili kwenye interview?

Utajibuje swali hili kwenye interview?

dereva wa roli aliyesota sana, hujibu, mi nipe gari na pesa ya safari, mshahara wako baki nao...wengine wanagoma kuongezewa mishahara wengine wapo tayar kufanya kama hayo...samahani kwa kutoka nje ya mada, hili ni jiwe gizani
 
Sasa Ww mshajika mbona hujanishitua na mm nasaka ajira jamani Ungesema Naomba nilipwe kulingana na kiwango kwa elimu niliyonayo kama navyotakiwa kulipa na kampuni
 
Na kuna jamaa yangu mmoja last week amekosa kazi bank moja kubwa tuu, aliulizwa hilo swali akajibu hivyo. Akaambiwa usipotaja kiwango ndio ushakosa kazi,jamaa hakutaja. Basi mpaka leo anasubiri call
 
Mhhhhhhhhh hili swali niliwahi kujibu Kama wadau hapo juu kuwa wanilipe kulingana Na salary scheme yao ,SEMA MIMI NILIKUWA NIMEJIANDAA MPAKA NIKAJUA KWA LEVEL YANGU MSHAHARA NI SHILING NGAPI....Nilitaja fasta tu pay me 1.4M.
 
1. Ni vizuri ujue kwenye industry hyo watu wa level yako wanalipwaje kisha waambie hiyo Range.
2. Mshahara haujawahi kuwa tatizo ninachohitaji ni pesa ya kukidhi mahitaji yangu yatayofanya utendaji kazi wangu kuwa rahisi,
3. Nilipe kutokana na viwango vyenu mlivyopanga kwa kuzingatia uzoefu na kiwango cha elimu.

Jibu kizungu utakuwa umetisha

Mfano - umesema mult lateral, case study coca cola

Hawa wanalipwa 1.5 - 2M muhasibu mwenye degree na experience Ya miaka 2 nakuendelea

" you may pay me one point eight million as Sector range but the door is open for negotiation"

"Salary had not become a problem to me. what's matter is an experience and my career development , you may pay any salary that may smooth daily working activities as you see it may fits"
 
Huwa wengine wanakomaa wakitaka utaje kiwango,sasa ikiwa utaishia kuwapa uhuru wa kukuchagulia huoni kwamba unajishusha uwezo wako kwenye soko la ajira?
Huo ni mtego. Si vizuri kutaja kiwango wao wenyewe wanajua na kiwango chako cha kazi si kinaonekana. So ukiona unafanya kazi haiendani na maslahi unaweza kuwaambia wakuongee au wao wenyewe wapime kama itashindikana unatafuta sehemu nyingine.
 
Back
Top Bottom