Utafiti: Wakenya walioajiriwa tz

Ntambaswala

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
255
195
Wasalaam,
Nafanya utafiti kujua idadi ya Raia wa Kenya wanaofanya kazi TZ. Huu ni utafiti ambao ni nyeti sana, naomba unayechangia ustick kwenye swali la utafiti kuliko kuleta hisia zingine. Utafiti huu ni wa kawaida kabisa. Hivi karibuni Kenya wamefanya utafiti na kubaini kuwa kuna Wakenya 300,000 wameajiriwa Rwanda (http://www.kenyansinrwanda.umutuzo.com/),
pia Kenya ni nchi ya tano Afrika kuwa na raia wake wengi Marekani(KENYANS IN DIASPORA). Pia kuna Wakenya wengi sana zaidi ya 70,000 huko Sudan ya kusini Are Southern Sudanese 'Jealous' of Kenyans Or.. Case of Insecurity? - SkyscraperCity.

Kilichonisuma kufanya utafiti huu ni kwa ajili ya kujiridhisha nafsi yangu, hasa baada ya Mkenya mmoja kuniambia ''eeh TZ ndo tukitaka kuja at tutachukua kazi zenyu wote maana nyie hamko na education na skills. Kwahiyo nafanya utafiti kuona je statement yake ni kweli? Kwa kuanzia nataka niaone aina ya kazi wanazofanya Wakenya, halafu ndipo nione kama kweli sisi hatuna elimu hiyo na skills hizo. Naomba ushirikiano

Naomba uorodheshe wadhifa au nafasi (title) na mahali anapofanya kazi mkenya hapa nchini. Usitaje jina la mtu. Naanza kutaja.

1. HRM wa NMB

meddie

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
432
250
Hongera kwa wazo vuri la kiutafiti....ila mimi kama ningepata nafasi ya kuweza kushauri on the focus ya research yako ningependa kujua ni vitu gani (qualities)vinawafanya Wakenya wawe wa tano Africa kuajiliwa Marekani, wawe wengi nchi zingine kama Rwanda ,TZ nk Wakati sisi Watz tumekaa tu na kurundikana hapa nchini bila ya kazi na kukalia kusema tumesoma!! Utafiti tunaohitaji ni ule utakao jibu mapungufu tuliyonayo Watz.....kitabia, elimu, kitamaduni, innovetiveness nk yanayosababisha tushindwe ku-export human resource na wakati huohuo ku-creat ajira zaidi hapa nchini!

Hardwood

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
997
1,000
Mi nadhani ungeweka pia factor zinazowafanya wawe juu kuliko sisi katika utafiti wako mkuu!!!

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
9,989
2,000
Kenya wako exposed kwenye mambo mengi kuliko tanzania.hapa bongo elimu yenyewe inatolewa kwa ubaguzi,ndo utataka kujicompare na mkenya.

Ntambaswala

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
255
195
Hongera kwa wazo vuri la kiutafiti....ila mimi kama ningepata nafasi ya kuweza kushauri on the focus ya research yako ningependa kujua ni vitu gani (qualities)vinawafanya Wakenya wawe wa tano Africa kuajiliwa Marekani, wawe wengi nchi zingine kama Rwanda ,TZ nk Wakati sisi Watz tumekaa tu na kurundikana hapa nchini bila ya kazi na kukalia kusema tumesoma!! Utafiti tunaohitaji ni ule utakao jibu mapungufu tuliyonayo Watz.....kitabia, elimu, kitamaduni, innovetiveness nk yanayosababisha tushindwe ku-export human resource na wakati huohuo ku-creat ajira zaidi hapa nchini!

Nashukuru kwa ushauri wako mzuri; unachosema kinaweza kuwa hatua ya pili ya utafiti. Kwa sasa najaribu "kuqualify au kudisqualify'' kauli aliyosema yule jamaa yangu. Kwa hiyo nataka kuona je kazi wanazofanya Wakenya hapa nchini, je ni kweli hakuna Watz wenye Elimu na Ujuzi nazo?. Kuna approach nyingi za namna ya kulitazama jambo. Mimi nimeona kwa kuanzia hapo itanipa majibu mazuri.

Jamani mbona hamnipi majibu......................au hawapo?

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
519
500
Utapata majibu tuu. Utafiti wako ni mzuri labda utasaisia pia kuwajuza watz wafocus kwenye vitu gani zaidi ili kupata soko la kimataifa zaidi ya hapa Bongo. Kiukweli nasikia watu wanasema kuwa hawa jamaa ni wengi ingawa ninapofanyia kazi hakuna hata mmoja.

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,015
2,000
Magazeti yenu ya TZ ya English yanatupa job kwa vile ati watized hawajui kusema kwa English.
Lakini hata ukikuja kwa hotel nyingi hapa Arusha utakuta mawaiters karibu yote ni kutoka kenya.
Ati watized hawana skills za customer care.
Siwezi sema security companies...banks...english medium school teachers za private... to mention few.

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,015
2,000
Wasalaam,
Nafanya utafiti kujua idadi ya Raia wa Kenya wanaofanya kazi TZ.

Kilichonisuma kufanya utafiti huu ni kwa ajili ya kujiridhisha nafsi yangu, hasa baada ya Mkenya mmoja kuniambia ''eeh TZ ndo tukitaka kuja at tutachukua kazi zenyu wote maana nyie hamko na education na skills. Kwahiyo nafanya utafiti kuona je statement yake ni kweli? Kwa kuanzia nataka niaone aina ya kazi wanazofanya Wakenya, halafu ndipo nione kama kweli sisi hatuna elimu hiyo na skills hizo.

Naomba uorodheshe wadhifa au nafasi (title) na mahali anapofanya kazi mkenya hapa nchini. Usitaje jina la mtu. Naanza kutaja.
1. HRM wa NMB
Review your research methods.

vena

JF-Expert Member
Apr 14, 2011
313
0
Magazeti yenu ya TZ ya English yanatupa job kwa vile ati watized hawajui kusema kwa English.Lakini hata ukikuja kwa hotel nyingi hapa Arusha utakuta mawaiters karibu yote ni kutoka kenya. Ati watized hawana skills za customer care.Siwezi sema security companies...banks...english medium school teachers za private... to mention few.
acha hizo we nyie mmekimbia njaaa coz kwenu kuna ukame...hahahaaa, karibu bongo ukarimu ule bata..thanks to EAC.

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,015
2,000
acha hizo we nyie mmekimbia njaaa coz kwenu kuna ukame...hahahaaa, karibu bongo ukarimu ule bata..thanks to EAC.
Sio Kenya yote kuna drought.
Iko kwa north na north east peke yake.
South kenya, central kenya ni evergreen Jan-Dec.
Iyo red: ukiona nchi ina export its citizen abroad kufanya kazi basi unapaswa ujue kuwa country in question has lots of pro-active professionals.
Think tena.

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
9,989
2,000
Sio Kenya yote kuna drought.

Iko kwa north na north east peke yake.

South kenya, central kenya ni evergreen Jan-Dec.

Iyo red: ukiona nchi ina export its citizen abroad kufanya kazi basi unapaswa ujue kuwa country in question has lots of pro-active professionals.

Think tena.

huyu jamaa anachosema ni cha kweli.ila ce watz serikali ye2 ndo inayo2angusha kwenye masuala mengi.

Mutambukamalogo

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
397
0
Sitaji vyeo,lakini utawakuta hawa jamaa kwa wingi kwenye ofisi za makampuni yafuatayo: Mwananchi newspaper company,DT DOBIE(NOW CFAO MOTORS),COCA COLA,SERENGETI BREWERIES. ITV,EAST AFRICA TV,SUPERDOL TRAILERS, AZAM,MAHOTELI MENGI N.K. Humu kwenye makampuni haya wapo wamejaa tele wanapiga mzigo ambao kuna watz wenye elimu na skills walizonazo kibao wanaweza.Wenye maeneo zaidi muweke hapa jamvini....

newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,377
1,500
nimemuajiri - operations officer kdk care services ltd
pia yupo mwingine sales rep mohamed enterprieses
pia namjua mwingine Sales personnel BATA ltd

kwa ufupi inatia hasira ,ila hawa jamaa wao wanaabudu pesa kuliko watanzania,and thats why wanajituma zaidi

Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
1,331
1,500
Ni kweli wakenya ni wengi hasa kwenye tour companies na hotel za kitalii wamejazana Arusha na Dar! Na hii wala sio la kuwalaumu wao jamaa hawa ni risk takers wanacourage ya kujaribu mambo na hawakati tamaa vitu ambavyo waTz wengi tunavikosa na pia hawana uoga kitu kinachowafanya wawe wazuri katika kujieleza so kufauku interview nyingi zisizo na ubaguzi wa utaifa!

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
0
Ukiwa na shule yako ambayo ni english medium afu wataka cheap labourers tafadhali consider kenya.

Nimekaa na wakenya, wengi ni wajanja kwenye lugha but ikija kwenye technical issues wengi wao ni wababaishaji mno.

Thus why utakuta wanafanya kazi ambazo zinahitaji kuongea zaidi, mfano sales rep, teaching, waiters and waitress jobs, call centres, front office desks, recruitment agencies etc

Mani H

Senior Member
Mar 25, 2011
180
0
sijui idadi kamili ni wangapi, ila nafasi nyingi za juu katika hotel nyingi za kitalii zanziabr zimekaliwa na wao wakenya.

Biohazard

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
2,109
2,000
This is hopeless watu wanatoa mada nzuri,badala ya kuchangia mnaanza kukosoa bila sababu, ulichoambiwa ni kutaja mkenya na position ya job na si kingine kama ofisi yako haina mkenya au haujaajiriwa basi you are not within the popultion so kaa kimya.

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,453
2,000
Ninadhani kupata kazi kwa waKenya katika nchi yetu, Marekani na kwingineko kunatoka aa juhudi zao binafsi na za kimfumo pia.

a) Mfumo wetu wa elimu ya juu ni wa kiingereza, na bado watu wengi waliohitimu elimu hiyo hawana ufahamu fasaha wa lugha hiyo.
b) Hakuna ushindani wa kweli "competencies" katika customer care na fani nyingine nyingi kama ilivo kwa wenzetu. Wakati wenzetu wanachagua ualimu, uhudumu ya hoteli, udereva nk kama trades wanazozipenda (au kwa urahisi wa kupata kazi au sababu nyingine) sisi fani hizo zinaonwa kama ni kimbilio baada ya mtu kufeli mitihani ya kidato cha nne au 6. Au kwa aliyemaliza darasa la saba ambaye lazima atakumbwa na tatizo la lugha ya kiingereza.
c) Tabia ya kuona kama anaykwenda nje kufanya kazi sio mzalendo (patriotic).
d) Kuwa na mfumo wa elimu usiokwenda na muda. Mitaala isiyohitaji maabara, ufundishaji wa kutumia "past papers" unaolenga kumwandaa mwanafunzi kujibu mtihani tu, sio kumjengea mazingira ya kukabiliana na current issues.
e) Kuwepo na mfumo wa kumwajiri mtu na kumfanya aamini atastaafu katika kazi hiyo. Sijui kama kuna "performance measurements" ukiachilia mbali "performance improvements". Kufanya kazi kwa mikataba ni jambo la maana ktk kujenga competencies na competitiveness ktk ajira. Mtu anakuwa kazini akiamini hatotoka. Leo hii kuna watu wamefanya kazi serikalini miaka 40!!! Unadhani hawa wana mwamko wa mabadiliko???

Takwimu za waKenya walioajiriwa itakuwa jambo gumu kulipata. Tuangalie kuja kwao kama udhaifu wetu kuliko ubora wao. Tukijifunza jambo moja au mawili kutoka kwao na KUYASHIKA, tutapunguza ujio wao. Ni vibaya kwa nchi ambayo lugha yake rasmi ya kufanyia kazi ni kiingereza lakini watu wake hawajui sehemu kubwa ya lugha hiyo.

Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,550
2,000
kenyans they are every where and almost every company and they deserve it kwani makampunii mengi yanamilikiwa na wakenya na nchi yetu imebaki kuwa soko wakati viwanda vyote vimeuliwa na serikali yenu ya CCM,so instead of complaining start doing something people.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom