EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Mratibu wa Jamii wa Afya ya Uzazi na Jinsia wa mradi unaotekelezwa kati ya UMATI na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa mkoani Kilimanjaro (KNCU), Lilian Sizya amesema kuwa baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanashindwa kufuata njia za uzazi wa mpango kutokana na imani potofu, mila na utamaduni, itikadi za kidini na ulevi wa kupindukia.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea vyama vya msingi Kibongoto Wanri na Machame Wanri wilayani Hai, Sizya alisema matatizo hayo yalibainika zaidi wilayani Rombo. Amedai familia kadhaa vijijini wilayani Rombo zimebainika kuwa na wastani wa watoto 12 huku zikishindwa kuwatimizia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu, afya na malazi .
Matokeo hayo yalibainika katika utafiti uliofanyika katika vijiji vya Mrao, Keryo na Momwe kata ya Mrao Keryo na kwamba baadhi hawako tayari kufuata uzazi wa mpango kutokana na sababu mbalimbali. "Masuala haya ni tatizo kubwa wapo watu wanaamini kuwa wakifuata uzazi wa mpango watapata saratani ya kizazi, mila potofu, ulevi wa kupindukia unaosababisha kutozingatia njia za uzazi wa mpango na itikadi za dini, tunapaswa kutoa elimu zaidi," alisema.
Kwa upande wa wahudumu wa afya, baadhi yao wameelezea kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni wanaume kukaidi kutumia njia za uzazi wa mpango hali inayolazimu baadhi ya wanawake kuzitumia kwa siri ili kupunguza idadi ya watoto.