Utafiti wa Kisayansi: "Kuna maisha baada ya Kifo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti wa Kisayansi: "Kuna maisha baada ya Kifo"

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Shebbydo, Oct 26, 2016.

 1. Shebbydo

  Shebbydo JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2016
  Joined: Feb 12, 2015
  Messages: 970
  Likes Received: 1,169
  Trophy Points: 180
  Utafiti huu umefanywa nchini Ujerumani kwa ushirikiano wa Wanasaikolojia, madaktari wa binadamu na chuo kikuu cha Technische Universitat of Berlin. Utafiti huu ulisimamiwa na daktari Berthold Ackermann.

  Utafiti ulifanywa kwa watu 944 ambao walijitolea wenyewe kwa vipindi tofauti tofauti ndani ya miaka minne.

  Mchanganyiko wa dawa za epinephrine na dimethyltryptamine zilitumika kwa ajili ya kuufisha mwili kwa muda wa dakika 20 wakati utafiti unafanyika. Mashine ya CardioPulmonary Recitation ilitumika kusisimua tena mapigo ya moyo ya watu hao waliokuwa wakifanyiwa utafiti.

  Matokeo yaliyotokana na utafiti huu hayakutofautiana sana miongoni mwa wafanyiwa utafiti. Kwa maelezo ya kile walichokiona watafitiwa wakati walipokuwa katika hali ya kifo ni;
  Kuona hali ya kuuacha mwili(detachment from the body), kuhisi kuelea hewani(feelings of levitation), Kujisikia amani kabisa(total serenity), usalama(security) na uwepo wa mwanga mkali sana(overwhelming light).

  Mbali na utafiti huu uliofanyika Ujerumani pia kuna ushuhuda ambao uliwahi kutolewa na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Pam Reynoild. Mama huyu alipatwa na ugonjwa uitwao Basilar Artery Aneurysm unaosababishwa na mshipa uliopo nyuma ya ubongo(Basilar Artery).

  Ushuhuda huu upo kwenye kitabu cha daktari aliyekuwa akimfanyia utafiti mwanamke huyu, Dr. Michael Sabom, kiitwacho Light and Death.

  Dr. Michael baada ya kugundua tatizo la Bi. Pam, alimrufaa kwa daktari ambaye alikuwa ni "specialist" wa upasuaji wa ubongo wa ugonjwa huu upasuaji ambao ni hatari na hufanyika mara chache. Upasuaji huo unafahamika kwa jina la Hypothermic Cardiac Arrest lakini ulipewa jina la utani la "Standstill".

  Ili upasuaji huu ufanyike mgonjwa lazima afanyiwe taratibu zifuatazo(Procedures):
  1:Jotoridi la mwili lazima lishushwe hadi nyuzi 16 za centigredi kutoka nyuzi 36.6 za centigredi.
  2:Mapigo ya moyo na kupumua kuzuiliwe.
  3:Damu iondolewe kwenye kichwa na
  4:Ubongo usifanye kazi.
  Kwa kifupi ni kufa ndani ya muda fulani.

  Kwa mujibu wa Bi. Pam baada ya kufanyiwa mambo haya kwenye upasuaji wake, ulifika wakati akajiona anatoka kwenye mwili wake halisi na kukaa pembeni. Aliweza kuona jinsi madaktari walivyokuwa wakiufanyia mwili wake upasuaji. Akiwa pembeni alisikia sauti zikimwita "njoo" lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida. Alianza kusogea huku akiwa ameuacha mwili wake pale kitandani ukifanyiwa upasuaji akielekea kulikokuwa na zile sauti ambazo alianza kuzitambua, mojawapo ikiwa ni sauti ya bibi yake aliyefariki kipindi cha nyuma.

  Sauti hizo ambazo zilikuwa zikitoka kwenye mwanga mkali alipozifikia ndipo aliweza kuwaona ndugu zake mbalimbali ambao walishafariki. Bi. Pam alitaka kuingia katikati ya ule mwanga mkali lakini baba yake mdogo ambaye naye alikuwa miongoni mwa wale watu aliowaona alimzuia akimwambia kuwa endapo akiingia katika mwanga huo hawatakuwa na uwezo wa kumrudisha kwenye mwili wake.

  Baba yake mdogo ndiye aliyemchukua na kumrudisha pale ulipokuwa mwili wake. Kwa mujibu wake Bi. Pam anasema hakutaka kurudi kwenye mwili wake ule kwa jinsi alivyokuwa akijisikia amani katika huo ulimwengu mpya. Anafananisha kurudi kwenye mwili wake halisi na tukio la kujitupa ndani ya bwawa la kuogelea.

  Je, kweli kuna maisha baada ya kifo? Ama ni mkanganyiko unaotokea kwenye ubongo? Lakini kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimfanyia upasuaji, vifaa kama electroencephalogram(EEG) ambacho hutumika kuonesha ubongo kufanya kazi kilionesha ubongo umesimama kufanya kazi na vipimo vingine vilionesha hakuna damu iliyokuwa ikienda kwenye ubongo.

  Hii inaweza kuwa kama hadithi ya kutunga lakini tuunganishe dot katika haya. Je, umewahi kuwa karibu na mtu ambaye anataka kukata roho huku akisema kuna watu wanataka kumchukuwa? Mimi binafsi niliwahi kuwa karibu wakati mjomba wangu anafariki alikuwa akiniambia nimshike mkono nimvute kuna watu wanataka kumchukua.
  Vipi kuhusu watu wa meditation hasa astral body projection, vinahusiana vipi na hii hali iliyosimuliwa na Bi.Pam Reynoild?

  Kuna mengi ya kujifunza katika dunia hii.
   
 2. KENZY

  KENZY JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2016
  Joined: Dec 27, 2015
  Messages: 6,262
  Likes Received: 5,280
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuna mengi ya kujifunza ktk dunia hii

  kuhusu hili mmmh! namashaka makubwa huyu bibie usikute alikuwa ameshaarifiwa kwamba hiyo operesheni itakwendaje (nusu kufa) so tayari ubongo unakuwa umeshaanza kucreat some action as a dream na kuhusu kuuzuia ubongo usifanye kazi kwa 0% hilo sidhani! hapo unakuwa chali kabisa lzm kuna asilimia kadhaa walizoziacha na ndizo zilizotenda kazi hiyo.
   
 3. s

  sugi JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2016
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Daa,visivyojulikana kwa mwanadamu ni vingi bado
   
 4. Shebbydo

  Shebbydo JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2016
  Joined: Feb 12, 2015
  Messages: 970
  Likes Received: 1,169
  Trophy Points: 180
  Aisee hii issue nipasua kichwa ukiifikiria katika upeo wetu. Hata mimi kuhusu Bi. Pam najiuliza maswali ambayo hayana majibu. Kama waliweza kumuua kwa muda na baadaye kuurudisha uhai wake, inashindikana je kurudisha uhai wa mtu aliyekufa?
   
 5. SANCTUS ANACLETUS

  SANCTUS ANACLETUS JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2016
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,546
  Likes Received: 1,772
  Trophy Points: 280
  Tekinolojia inaendelea kutafuta majibu ya yale tusiyokuwa na majibu yake bado.Muda utasema baadaye.
   
 6. a

  always am a Winner JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2016
  Joined: Nov 16, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Kuna mambo mengi sana yamefichwa, tena naamini Mungu kayaficha makusudi ili watu wanaomtafuta na kumpenda kwelikweli wayatafute na kuyapata kama anavyosema kwenye neno lake "Mkinitafuta mtaniona, tena mkinitafuta kwa bidii"
  Kila ninapoamka huwa nafikiri kuhusu Mungu na maisha. Sitakuja kuacha mpaka nipate majibu, currently I do believe in God, but yet I want to know as many things as possible.
   
 7. a

  always am a Winner JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2016
  Joined: Nov 16, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Naamini kadri unavyomtafakari Mungu ndivyo unaposogea karibu na Kweli yake.
   
 8. a

  always am a Winner JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2016
  Joined: Nov 16, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  I do believe in God, but yet I don't believe much about these types of experiments. In any big operations, people can not die 100%. If you die 100%, you can not wake up. If you wake up, then, you was not dead.
   
 9. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2016
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  m
  Napita..nitarejea
   
 10. Shebbydo

  Shebbydo JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2016
  Joined: Feb 12, 2015
  Messages: 970
  Likes Received: 1,169
  Trophy Points: 180
  Inabidi urejee utoe uonavyo kwa mujibu wa ubongo wako

  Sent from my HUAWEI Y511-U30 using JamiiForums mobile app
   
 11. Z

  ZEE LA HEKIMA JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2016
  Joined: Aug 10, 2015
  Messages: 921
  Likes Received: 924
  Trophy Points: 180
  Mungu ameficha mengi sana kwetu. Lakini ni wazi kabisa there is life after death. Watu hawataki kuamini kwa sababu eti there is no scientific proof. Maajabu ya Mungu ni mengi mno. Hivi umeshajiuliza inakuwaje kila binadamu ana thumbprint (alama ya kidole gumba) tofauti na watu wengine wote ambao idadi yao ni mabilioni? Umeshajiuliza mchwa kwenye kichuguu wanapangianaje kazi na nani anawaamrisha? Umeshajiuliza nyuki anapokuta mahali penye maua anaendaje kueleza wenzake wakamwelewa mpaka wakaenda kwenye hayo maua? Kama maajabu hayo yapo kwa nini tusiamini kuna maisha baada ya kifo? Ukweli ni kwamba mtu akiwa anataka kukata roho na ana amani moyoni lazima anawaona wale walioko upande ule mwingine. Wengi wanaona watu waliovaa nyeupe na wanasema. Wengine wanawaona jamaa zao waliotangulia mbele ya haki na kuwataja kabisa majina. There is life after death
   
 12. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2016
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Jibu linapatikana katika maneno haya;

  "ULITOKA KWA UDONGO NA UTARUDI KWA UDONGO"

  Kwa maneno haya, jaribu kukumbuka ulikokuwa kabla hujazaliwa, huko huko utakuwa baada ya kufa.
   
 13. KENZY

  KENZY JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2016
  Joined: Dec 27, 2015
  Messages: 6,262
  Likes Received: 5,280
  Trophy Points: 280
  naona mahubiri yameshika wasaa wake!:D
   
 14. z

  zed123 Member

  #14
  Oct 27, 2016
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 90
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 25
  Njia za Mungu hazichunguziki yeye mwenyewe amesema ktk biblia takatifu
   
 15. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2016
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kiranga yuko wapi, natamani kuona reaction yake kuhusu hili
   
 16. okonkwo jr

  okonkwo jr JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2016
  Joined: Jun 14, 2015
  Messages: 2,427
  Likes Received: 1,466
  Trophy Points: 280
  You was=you were
   
 17. d

  dplus Member

  #17
  Oct 27, 2016
  Joined: Jun 14, 2016
  Messages: 30
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  mshana jr jongea huku pamoja na Apolo
   
 18. t

  time theory JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2016
  Joined: Nov 22, 2013
  Messages: 735
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  What is death?
   
 19. t

  time theory JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2016
  Joined: Nov 22, 2013
  Messages: 735
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  What is death?
   
 20. t

  time theory JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2016
  Joined: Nov 22, 2013
  Messages: 735
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  Vingi ya unavyoamini uliambiwa na vingine ulisimuliwa,sasa hivi unaambiwa habari nyingine ambazo zinapingana na habari ambazo umezifahamu maisha yako yote.

  Nikushauri,fanya utafiti wako kisha uamue ni kipi cha kuamini. Jaribu kuwa huru,usikubali dini iteke ufahamu wako kwenye kutaka kuujua ukweli.

  Binafsi nimeshajiridhisha kwamba kulikuwa na maisha kabla ya kizaliwa na kutaendelea kuwa na maisha baada ya kufa kwa mwili.

  Roho haifi.
   
Loading...