Utafiti wa Kisayansi: "Kuna maisha baada ya Kifo"

I do believe kuna maisha mengine ya binadamu kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huu mwili. Kitu ka hicho kiliwahi kunitokea kujiona Niko kwenye ilimwengu mwingine na mwili mpya kabisa na nilikua najiona mwepesi na tofauti na ile hali ilinivutia na kunifurahisha kiasi nilikua na watu wengine nafurahia nakushangaa, nikawa nagoma kurudi kwenye hali ya umwili maana nilinogewa then wale watu kuna jinsi walinipiga mgongoni nikarudi hali ya kawaida. So I do believe kuna maisha mengine tofauti na haya tuyaishiyo kwenye ulimwengu huu wa kibinadamu
kuna mdada flani wa mbeya alitoaga story kama unavyosema wewe. alipelekwa ulimwengu mwingine na kuonyeshwa maisha ya huko
 
Einstein's theory is that matter plus energy is constant. Thus various forms of matter and energy are variations in the constant of unity. Another name for this constant and unity is GOD. All variations in this world are but vibrations in this constant unity of the Almighty GOD. Variations of energy in matter renders it with properties. Conscious energy directly influences variations of energy and property of matter. Conscious energy is the causal force in the variations of energy and matter and also causes variations in automated matter - energy variations. Conscious energy causes variations in automated thought processes. Mind is a pool of thought processes that is tied to body. Conscious energy resides in mind. This is Soul. Conscious energy - Soul is immortal - indestructible. In other words, it is not subject to the frequency of variations that matter - body is. The conscious energy Soul upon leaving body which then changes form very fast - deteriorates; while carrying automated thought processes along, upon entering different body, may manifest recall of past events from the carried forward thought processes providing evidence of reincarnation. Record of such events abounds in all cultures. A detailed explanation on reincarnation, among many other issues, is there for any interested person in Shrimad Bhagwat.
 
I do believe in God, but yet I don't believe much about these types of experiments. In any big operations, people can not die 100%. If you die 100%, you can not wake up. If you wake up, then, you was not dead.
This is called near death experience. Kuna shuhuda nyingi tu za watu ambao wameshapitia hali hii na mwili kurudi kufanya kazi kama kawaaida na kushuhudia waliyoyaona. Nitazitafuta na kuzionganisha hapa.
Binafsi naamini katika uwepo wa Mungu "The Creator" na life after death too
Einstein's theory is that matter plus energy is constant. Thus various forms of matter and energy are variations in the constant of unity. Another name for this constant and unity is GOD. All variations in this world are but vibrations in this constant unity of the Almighty GOD. Variations of energy in matter renders it with properties. Conscious energy directly influences variations of energy and property of matter. Conscious energy is the causal force in the variations of energy and matter and also causes variations in automated matter - energy variations. Conscious energy causes variations in automated thought processes. Mind is a pool of thought processes that is tied to body. Conscious energy resides in mind. This is Soul. Conscious energy - Soul is immortal - indestructible. In other words, it is not subject to the frequency of variations that matter - body is. The conscious energy Soul upon leaving body which then changes form very fast - deteriorates; while carrying automated thought processes along, upon entering different body, may manifest recall of past events from the carried forward thought processes providing evidence of reincarnation. Record of such events abounds in all cultures. A detailed explanation on reincarnation, among many other issues, is there for any interested person in Shrimad Bhagwat.

Utafiti huu umefanywa nchini Ujerumani kwa ushirikiano wa Wanasaikolojia, madaktari wa binadamu na chuo kikuu cha Technische Universitat of Berlin. Utafiti huu ulisimamiwa na daktari Berthold Ackermann.

Utafiti ulifanywa kwa watu 944 ambao walijitolea wenyewe kwa vipindi tofauti tofauti ndani ya miaka minne.

Mchanganyiko wa dawa za epinephrine na dimethyltryptamine zilitumika kwa ajili ya kuufisha mwili kwa muda wa dakika 20 wakati utafiti unafanyika. Mashine ya CardioPulmonary Recitation ilitumika kusisimua tena mapigo ya moyo ya watu hao waliokuwa wakifanyiwa utafiti.

Matokeo yaliyotokana na utafiti huu hayakutofautiana sana miongoni mwa wafanyiwa utafiti. Kwa maelezo ya kile walichokiona watafitiwa wakati walipokuwa katika hali ya kifo ni;
Kuona hali ya kuuacha mwili(detachment from the body), kuhisi kuelea hewani(feelings of levitation), Kujisikia amani kabisa(total serenity), usalama(security) na uwepo wa mwanga mkali sana(overwhelming light).

Mbali na utafiti huu uliofanyika Ujerumani pia kuna ushuhuda ambao uliwahi kutolewa na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Pam Reynoild. Mama huyu alipatwa na ugonjwa uitwao Basilar Artery Aneurysm unaosababishwa na mshipa uliopo nyuma ya ubongo(Basilar Artery).

Ushuhuda huu upo kwenye kitabu cha daktari aliyekuwa akimfanyia utafiti mwanamke huyu, Dr. Michael Sabom, kiitwacho Light and Death.

Dr. Michael baada ya kugundua tatizo la Bi. Pam, alimrufaa kwa daktari ambaye alikuwa ni "specialist" wa upasuaji wa ubongo wa ugonjwa huu upasuaji ambao ni hatari na hufanyika mara chache. Upasuaji huo unafahamika kwa jina la Hypothermic Cardiac Arrest lakini ulipewa jina la utani la "Standstill".

Ili upasuaji huu ufanyike mgonjwa lazima afanyiwe taratibu zifuatazo(Procedures):
1:Jotoridi la mwili lazima lishushwe hadi nyuzi 16 za centigredi kutoka nyuzi 36.6 za centigredi.
2:Mapigo ya moyo na kupumua kuzuiliwe.
3:Damu iondolewe kwenye kichwa na
4:Ubongo usifanye kazi.
Kwa kifupi ni kufa ndani ya muda fulani.

Kwa mujibu wa Bi. Pam baada ya kufanyiwa mambo haya kwenye upasuaji wake, ulifika wakati akajiona anatoka kwenye mwili wake halisi na kukaa pembeni. Aliweza kuona jinsi madaktari walivyokuwa wakiufanyia mwili wake upasuaji. Akiwa pembeni alisikia sauti zikimwita "njoo" lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida. Alianza kusogea huku akiwa ameuacha mwili wake pale kitandani ukifanyiwa upasuaji akielekea kulikokuwa na zile sauti ambazo alianza kuzitambua, mojawapo ikiwa ni sauti ya bibi yake aliyefariki kipindi cha nyuma.

Sauti hizo ambazo zilikuwa zikitoka kwenye mwanga mkali alipozifikia ndipo aliweza kuwaona ndugu zake mbalimbali ambao walishafariki. Bi. Pam alitaka kuingia katikati ya ule mwanga mkali lakini baba yake mdogo ambaye naye alikuwa miongoni mwa wale watu aliowaona alimzuia akimwambia kuwa endapo akiingia katika mwanga huo hawatakuwa na uwezo wa kumrudisha kwenye mwili wake.

Baba yake mdogo ndiye aliyemchukua na kumrudisha pale ulipokuwa mwili wake. Kwa mujibu wake Bi. Pam anasema hakutaka kurudi kwenye mwili wake ule kwa jinsi alivyokuwa akijisikia amani katika huo ulimwengu mpya. Anafananisha kurudi kwenye mwili wake halisi na tukio la kujitupa ndani ya bwawa la kuogelea.

Je, kweli kuna maisha baada ya kifo? Ama ni mkanganyiko unaotokea kwenye ubongo? Lakini kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimfanyia upasuaji, vifaa kama electroencephalogram(EEG) ambacho hutumika kuonesha ubongo kufanya kazi kilionesha ubongo umesimama kufanya kazi na vipimo vingine vilionesha hakuna damu iliyokuwa ikienda kwenye ubongo.

Hii inaweza kuwa kama hadithi ya kutunga lakini tuunganishe dot katika haya. Je, umewahi kuwa karibu na mtu ambaye anataka kukata roho huku akisema kuna watu wanataka kumchukuwa? Mimi binafsi niliwahi kuwa karibu wakati mjomba wangu anafariki alikuwa akiniambia nimshike mkono nimvute kuna watu wanataka kumchukua.
Vipi kuhusu watu wa meditation hasa astral body projection, vinahusiana vipi na hii hali iliyosimuliwa na Bi.Pam Reynoild?

Kuna mengi ya kujifunza katika dunia hii.
 
Naweza kuwait shuhuda wa hili maana kuna kipindi niliugua sana ilifikia hatua nikajiona kama ninaelea na nina amani wana ila nilishituka baada ya kupigwa drip.
 
kuna movie niliitazama mwaka jana,inaitwa dr. strange. ndani yake kuna scene inayofanana na tukio alilo eleza mtoa mada la mgonjwa kutoka nje ya mwili wakati anafanyiwa matibabu.inasisimua sana.hatari sana hizi habari.
 
Ni kweli kuna maisha baada ya kifo na maisha hayo yanategemea ulijiandaaje kabla ya kufa (kwa mujibu wa vitabu vitakatifu )mengine ya wazungu ni snema tu.
 
Meditation
Mkuu watu wa meditation huwa wanatoka nje ya mwili kwa mujibu wao
Na wana uwezo wa kukaa pembeni na kuangalia mwili waliouacha,
Kwenye hili swala maisha baada ya kifo nafikiria sana ila sifahamu kama kuna life after death...
Lakin cha kujiuliza ni kwa nini watu wengi wanapokuwa wanataka kukata roho huwa wanaona watu????
Ile ni hofu ya kifo ndomana anaona watu
 
Nafikir na hzi movie tunazo angalia mzungu anajaribu kufikiria baada ya kufa binadamu anaweza kuishi tena ndo wanafkiria kama inawezekana akawa kama zombi au vampire
 
Ni kweli hata wwe wawezajifunza elimu hio ya kuuacha mwili na kwenda sehemu nyingine inaitwa astral Kwa watu wa meditation wanajua,pia kidini yapo maisha baada ya kifo tusiogope IPO siku tutaungana na wapendwa wetu ndugu zetu wazazi wetu na tutakuwa nao Furaha na amani tena fikiria unakuja onana na ndugu au wapendwa ni Furaha ilioje,tusisumbukie sana dunia hii yapita tuishi na tuzidi kutenda mema Kwa wote, na tusiogope.Dunia ni kubwa na hatuwezi maliza elimu yote.
 
Huyu mleta uzi anajaribu ku infuse spiritualism, kuna study ya scientology ina mambo kama hayo sana tu, wao spirit wanaita theta, wanadai wanaweza kumfanya mtu awe clear na pia mtu anaweza kutoka kwenye mwili wake. Nimesomaa hadi nikaona sasa nafundishwa u satanism kwa vile kwanza study yenyewe ina deny existence ya Creator kwa namna ambayo hawaelezi directly lakini ukisoma utajua wanataka nini uelewe. Founder wa dianetics na scientology ni Ron Hubbard ambaye alikuwa ni nuclear scientist, nikajiuliza, elimu yote hii anayoitoa na akatoa na experience zake alizofanya kwa watu, mbona yeye hajaishi milele? Alikufa mwaka 1985, nikaona kumbe elimu zote hizi ni kutuvuruga tu, ni bora ukomae kumtafuta Mungu wa Ibrahimu, kwa kumuamini Kristo wake ambaye anakupa Imani (hapa namaanisha Faith sio belief) ambayo ukiipata hiyo Imani unakuwa na uwezo wa kufanya chochote duniani hata kama ni kuuhamisha mlima na mwisho wa siku Imani hiyo inakuokoa na kifo hichi tunachokipata, haya mambo ya astra body sijui nini ni i
upuuzi mtupu.
Mkuu hiyo ni neema umepewa bure! Nakupongeza sana kuyajua haya
 
Back
Top Bottom