Utafiti Synovate: Dk Slaa ang’ara urais

Utafiti Synovate: Dk Slaa ang’ara urais

hawa hawana maana yoyote, ni wa kupuuza kabisa. nia yao ni kuanza kuchafua majina ya watu na kugombanisha watu hasa wale wenye nia na malengo ya kuchukua ikulu 2015. wametumia kigezo gani kumuweka JK pembeni?, mbona vitu wanavyotafiti havieleweki malengo mahususi?, hawa ni mawakala wa shetani tu!
 
Hao jamaa wazushi, wamejua majibu yao hayana impact yoyote ktk siasa za bongo. Synovate hovyooo!
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Dk Slaa ang’ara urais
[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"]Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 03 August 2011 23:11
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Dk Slaa ang?ara urais

NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.
Leon Bahati
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate yanaonyesha kwamba iwapo Rais Jakaya Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa Uchaguzi Mkuu sasa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.
Dk Slaa anaongoza kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (asilimia 14), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe asilimia tisa.
Synovate inaeleza kwenye ripoti hiyo kwamba matokeo ya utafiti huo yanatokana na watu mbalimbali wenye umri zaidi ya kuanzia miaka 18 walioulizwa maswali ya ana kwa ana vijijini na mijini.
Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: “Mbali na Rais Jakaya Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa Rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?”
Kwa mujibu wa matokeo hayo, iwapo uchaguzi ungefanyika sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu licha ya kwamba CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kuaminika mbele ya umma ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 29, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.

CCM wamtaka Dk Slaa
Utafiti huo unaonyesha kuwa wanachama wengi wa CCM walionyesha kuvutiwa na Dk Slaa ikilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho tawala.Hii inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kati ya waliohojiwa katika utafiti huo, wengi wanatokana na CCM, lakini wakamchagua Dk Slaa.
Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuwa kati ya waliohojiwa, walipoulizwa kuhusu vyama vyao asilimia 51 walisema ni CCM, asilimia 35 wakasema Chadema, 10, CUF na TLP asilimia moja.
Mbali na Dk Slaa, Profesa Lipumba, Pinda na Zitto wanasiasa wengine wanne wanaofuatia ambao asilimia walizopata zimo kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).
Kadhalika, vigogo tisa waliofungana kwa kupata asilimia moja ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.
Katika utafiti huo, Synovate iliegemea nyanja tatu za utafiti ambazo ni siasa, uchumi na masuala ya kijamii na utamaduni.
Mgombea urais CCM 2015
Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.
Wanaofuatia kwa mvuto pamoja na asilimia walizopata kwenye mabano ni Membe (8), Sitta (3), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (3), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (3) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (2).
Vigogo tisa ndani ya CCM walifungana kwa kupata asilimia moja nao ni Makinda, Dk Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim.
Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.
Uvuaji gamba CCM
Utafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanatofautiana juu ya uelewa wa mpango wa CCM wa kujivua gamba.
Katika mpango huo ripoti hiyo inasema asilimia 41 walisema ni mpango wa kuwataka watu kujiuzulu kwenye uongozi wakati asilimia 29 walisema ni mpango wa kutaka kukisafisha chama.
Inaonyesha kuwa asilimia 15 ya waliohojiwa walielezea kujivua gamba kuwa ni mabadiliko ya uongozi kwa kuondoa viongozi wabovu na asilimia tano wakasema ni mpango wa kuondoa viongozi wote watuhumiwa wa ufisadi.
Asilimia mbili walisema ni mpango wa kukifanya chama hicho cha siasa kiwe na mfumo wa wazi na unaoeleweka wakati asilimia moja walisema ni suala la kujizuzulu, kutafuta viongozi wachapakazi na wenye tija. Kuna wanaouchukulia kuwa ni mkakati wa kisanii wa kuwadanganya wananchi.
Kwa ujumla, taarifa hiyo ilisema ni asilimia 45 tu ambao wana taarifa kuwa kuna Sekretarieti ya CCM ilijiuzulu na Mwenyekiti wake, Rais Kikwete amekwishateua wengine kushika nafasi hizo.

Kero kubwa nchini
Asilimia 56 walisema tatizo kubwa linalowakumba ni kupanda kwa bei ya vyakula, gharama za maisha na umaskini na asilimia 46 walisema njaa na tatizo kwenye kilimo.
Tatizo la ufisadi nchini lilichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 36, ukosefu wa ajira (31), tatizo la nyumba, barabara na umeme (27), elimu (23), afya (21), maji (16), uharibifu wa mazingira (12), taasisi za siasa (10), haki za binadamu, uhalifu (6) ubeberu na usafirishaji wa dawa za kulevya (3).

Katiba Mpya
Miongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kuwa ni vikwazo kwa Tanzania kupata Katiba Mpya ni rushwa (26), kukosekana kwa umoja (19), maslahi ya kisiasa (18), ufahamu mdogo (11) na kukosekana kwa msukumo wa kisiasa (9).
Hata hivyo, asilimia 78 walisema wanataka yawepo mabadiliko ya katiba nchini wakati asilimia 21 hawaoni umuhimu wake.
Lakini asilimia 42 walisema wana uhakika kwamba mpango wa Katiba Mpya utafanikiwa.
Lakini pia makosa ya Katiba iliyopo yalielezwa kuwa ni kupitwa na wakati, kuandikwa kwa Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili, kukosekana kwa utawala bora, kutokuwepo kwa sheria za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kwa nini na JK asingepigiwa poll opinion kwa sababu kipindi chake akijakwisha? Synovate mnajipendekeza kwa JK kwa kumwondoa kwenye opinion poll au mmeficha hayo matokeo ya JK sio nzuri kwa independent istitution kama hiyo! Nafikiri katiba mpya iwe na kifungu kwamba katikati ya term ya Urais wananchi waulizwe kama wanaridhishwa na mwnenendo/ utendaji wa Rais na kama asilimia zaidi ya 50 hairidhishwi basi uchaguzi mkuu kuitishwa na Rais aliyeko madarakani kupoteza sifa kabisa ya kuwa mgombea Urais.
 
Kwa nini hawakumuweka Jk katika kinyang'anyiro? Synovate walihofu 'mtu' wao angepata almost asilimia sifuri. Na pengine awali walimuweka na baadaye kumuondoa walipoona ni disaster.
 
hata kikwetw mwenyewe anajua kuwa wananchi hawampendi......anajua kabisa ana anajua kabisa kuwa aliiba kura za slaa.......na anajua kabisa kuwa hakushinda uchaguzi..........ndio maana yupo tu kama rubber stamp
 
huyu ndiye rais aliyechaguliwa na wananchi 2010
Mbona hayupo Ikulu kama kweli alichaguliwa?
Hizo zote ni ndoto tu kaka,
Chukua jembe na nyundo tuendelee kulijenga taifa letu!
 
Mbona hayupo Ikulu kama kweli alichaguliwa?<br />
Hizo zote ni ndoto tu kaka,<br />
Chukua jembe na nyundo tuendelee kulijenga taifa letu!

Yupo "Ikulu ya Nguvu ya Umma," ndio maana Magamba hayana usingizi, hayana amani, hayana raha, kila kukicha!
 
hawa hawana maana yoyote, ni wa kupuuza kabisa. nia yao ni kuanza kuchafua majina ya watu na kugombanisha watu hasa wale wenye nia na malengo ya kuchukua ikulu 2015. wametumia kigezo gani kumuweka JK pembeni?, mbona vitu wanavyotafiti havieleweki malengo mahususi?, hawa ni mawakala wa shetani tu!
Mkuu unataka kujua sababu kwanini JK amewekwa kando? Mkuu hivi unaishi Tanzania kweli au unaishi magogoni? Kwa mtu yeyote hata mtoto mdogo ukimuliza sababu za jk kukaa pembeni atakuambia..maisha magumu, wizi, ufisadi, kauli tata za jk, safari za nje, mengine ongezea na wewe...
 
HTML:
Mgombea urais CCM 2015
Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.
Wameenda vizuri sana sehemu nyingi, ila wameniboa hapo waliposema kuwa katika Urais 2015 Pinda anaongoza katika polls!
Nchi hii ikikabidhiwa kwa Pinda ndiyo mwisho wake, itakuwa kila kitu ruksa, na itacollapse in just six Months of his stoogical regime!
 
Watu walio hojiwa ni 1994 kati ya wapiga kura 13,000,000 hii ni sawa na asilimia 0.00015. Duh kweli hamna kitu hapo, ni ubabaishaji wa hali ya juu ndungu zanguni
 
Mbona hayupo Ikulu kama kweli alichaguliwa?
Hizo zote ni ndoto tu kaka,
Chukua jembe na nyundo tuendelee kulijenga taifa letu!

Ha ha haaaaaa sidhani kama atarudia kukuuliza tena
 
hii ni ripoti ya taarifa rasmi ya nini hasa kilijiri kwenye uchaguzi uliopita. Bila shaka hizo ndo kura za Dr. Slaa alizochakachuliwa...
 
Mbona hayupo Ikulu kama kweli alichaguliwa?
Hizo zote ni ndoto tu kaka,
Chukua jembe na nyundo tuendelee kulijenga taifa letu!

Kaka, hapo penye redi siku hizi pashabadilishwa. Wanasemaga "Chukua Umma na Kisu tule nchi"
 
Huu utafiti unaonyesha CCM hawajatoa "posho" mwaka huu!!
 
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 100%, bgcolor: transparent"]Dk Slaa ang’ara urais
[/TD]
[TD="width: 100%, bgcolor: transparent"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]Wednesday, 03 August 2011 23:11
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]
1diggdigg​
NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.
Leon Bahati
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate yanaonyesha kwamba iwapo Rais Jakaya Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa Uchaguzi Mkuu sasa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.

Dk Slaa anaongoza kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (asilimia 14), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe asilimia tisa.
Synovate inaeleza kwenye ripoti hiyo kwamba matokeo ya utafiti huo yanatokana na watu mbalimbali wenye umri zaidi ya kuanzia miaka 18 walioulizwa maswali ya ana kwa ana vijijini na mijini.
Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: “Mbali na Rais Jakaya Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa Rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?”
Kwa mujibu wa matokeo hayo, iwapo uchaguzi ungefanyika sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu licha ya kwamba CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kuaminika mbele ya umma ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 29, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.

CCM wamtaka Dk Slaa

Utafiti huo unaonyesha kuwa wanachama wengi wa CCM walionyesha kuvutiwa na Dk Slaa ikilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho tawala.Hii inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kati ya waliohojiwa katika utafiti huo, wengi wanatokana na CCM, lakini wakamchagua Dk Slaa.

Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuwa kati ya waliohojiwa, walipoulizwa kuhusu vyama vyao asilimia 51 walisema ni CCM, asilimia 35 wakasema Chadema, 10, CUF na TLP asilimia moja.
Mbali na Dk Slaa, Profesa Lipumba, Pinda na Zitto wanasiasa wengine wanne wanaofuatia ambao asilimia walizopata zimo kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).
Kadhalika, vigogo tisa waliofungana kwa kupata asilimia moja ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.
Katika utafiti huo, Synovate iliegemea nyanja tatu za utafiti ambazo ni siasa, uchumi na masuala ya kijamii na utamaduni.
Mgombea urais CCM 2015
Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.

Wanaofuatia kwa mvuto pamoja na asilimia walizopata kwenye mabano ni Membe (8), Sitta (3), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (3), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (3) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (2).
Vigogo tisa ndani ya CCM walifungana kwa kupata asilimia moja nao ni Makinda, Dk Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim.
Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Uvuaji gamba CCM
Utafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanatofautiana juu ya uelewa wa mpango wa CCM wa kujivua gamba.

Katika mpango huo ripoti hiyo inasema asilimia 41 walisema ni mpango wa kuwataka watu kujiuzulu kwenye uongozi wakati asilimia 29 walisema ni mpango wa kutaka kukisafisha chama.
Inaonyesha kuwa asilimia 15 ya waliohojiwa walielezea kujivua gamba kuwa ni mabadiliko ya uongozi kwa kuondoa viongozi wabovu na asilimia tano wakasema ni mpango wa kuondoa viongozi wote watuhumiwa wa ufisadi.
Asilimia mbili walisema ni mpango wa kukifanya chama hicho cha siasa kiwe na mfumo wa wazi na unaoeleweka wakati asilimia moja walisema ni suala la kujizuzulu, kutafuta viongozi wachapakazi na wenye tija. Kuna wanaouchukulia kuwa ni mkakati wa kisanii wa kuwadanganya wananchi.
Kwa ujumla, taarifa hiyo ilisema ni asilimia 45 tu ambao wana taarifa kuwa kuna Sekretarieti ya CCM ilijiuzulu na Mwenyekiti wake, Rais Kikwete amekwishateua wengine kushika nafasi hizo.

Kero kubwa nchini

Asilimia 56 walisema tatizo kubwa linalowakumba ni kupanda kwa bei ya vyakula, gharama za maisha na umaskini na asilimia 46 walisema njaa na tatizo kwenye kilimo.Tatizo la ufisadi nchini lilichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 36, ukosefu wa ajira (31), tatizo la nyumba, barabara na umeme (27), elimu (23), afya (21), maji (16), uharibifu wa mazingira (12), taasisi za siasa (10), haki za binadamu, uhalifu (6) ubeberu na usafirishaji wa dawa za kulevya (3).

Katiba Mpya
Miongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kuwa ni vikwazo kwa Tanzania kupata Katiba Mpya ni rushwa (26), kukosekana kwa umoja (19), maslahi ya kisiasa (18), ufahamu mdogo (11) na kukosekana kwa msukumo wa kisiasa (9).

Hata hivyo, asilimia 78 walisema wanataka yawepo mabadiliko ya katiba nchini wakati asilimia 21 hawaoni umuhimu wake.Lakini asilimia 42 walisema wana uhakika kwamba mpango wa Katiba Mpya utafanikiwa.
Lakini pia makosa ya Katiba iliyopo yalielezwa kuwa ni kupitwa na wakati, kuandikwa kwa Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili, kukosekana kwa utawala bora, kutokuwepo kwa sheria za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.

"'mwanzo mzuri mpaka kieleweke 2015''
http://reddit.com/http://del.icio.us/http://www.mixx.com/http://www.entirelyopensource.com/http://www.google.com/bookmarks/https://favorites.live.com/https://www.facebook.com/http://www.stumbleupon.com/http://twitthis.com/http://joomladigger.com/
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
bado siwaelewi hawa jamaa..kwanza ndo waliochangia uchakachuaji wa kura....
 
HTML:
Mgombea urais CCM 2015
Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.
Wameenda vizuri sana sehemu nyingi, ila wameniboa hapo waliposema kuwa katika Urais 2015 Pinda anaongoza katika polls!
Nchi hii ikikabidhiwa kwa Pinda ndiyo mwisho wake, itakuwa kila kitu ruksa, na itacollapse in just six Months of his stoogical regime!
hayo ni mawazo yako na yanakuwakilisha wewe, ila wengine nao wameona kuwa pinda anafaa kuwa rais. so usijifanye wewe ndo kila kitu, you are just a single one.
 
naamini hata uchaguzi ukifanyika leo slaa hawezi kuwa rais. hizo pool zenu mnazofanyia huko uchaggani haziwakilishi mawazo ya wote. mkitaka kuthibitisha hili hebu aende akagombee jimbo la Igunga 3 months to come then you will see the reality. Read me between my two lips.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom