Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Speaker, Feb 8, 2012.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  UTAFTI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.
  Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya mwaka 2009 na Septemba 2010 unaonyesha, asilimia 47.05 ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba.
  Malengo ya utafiti huo uliosimamiwa na Dk Henry Mwakyoma, yalikuwa ni kubaini ni kwa kiasi gani wanaume huweza kuathiriwa katika via vyao vya uzazi na hatimaye kushindwa kutungisha mimba.

  Utafiti huo ulionyesha kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na asilimia 17.02 walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.
  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dk Mwakyoma alisema, ugumba kwa wanaume limekuwa tatizo sugu katika miaka ya hivi karibuni.

  alisema Dk Mwakyoma.Alisema hapo awali ilikuwa vigumu kupata idadi kamili ya wanaume wenye ugumba kwa sababu walikuwa hawajitokezi kupima.
  alisema Mwakyoma.

  Sababu za ugumba

  Mwakyoma alitaja sababu za ugumba kwa wanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii.
  Alitaja sababu nyingine kuwa ni kemikali zinazoingia katika miili yetu, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo.

  Dk Mwakyoma aliongeza kuwa, wanaoathirika zaidi ni wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda mrefu
  alisema.

  Dk Mwakyoma akifafanua jinsi kitengo chake kinavyopima manii ili kujua kama zina matatizo au zipo salama, alisema, [quote rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ili kutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, mbegu zenye rangi aidha kijivu au nyeupe si salama.[/quote]

  Kwa upande wake, Dk Innocent Mosha, ambaye ni daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Muhimbili alisema, wamefanikiwa kupata takwimu hizo kutokana na wanandoa wengi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kujua sababu ya kutokuwa na watoto katika ndoa yao.
   
 2. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Kudadeki!!Hii sasa hatari aisee!!
   
 3. A

  Aine JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mhhhh!!!! ngoja nisikie wanaume mna coment vipi hapa, maana mwanamke asipozaa wao ni wa kwanza kumrushia mwanamke lawama oooh huzai, ooooh nazeeka sina mrithi, kumbe na wenyewe ni wagumba?????????? Natamani wanaume wooote wwsome gazeti hili au hapa jf
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  MMh hali ni mbaya sana.............kuna haja ya kutoa elimu pana sana kwenye makundi yaliyopo hatarini................lakini naona kicha cha habari kinapigiwa upatu sana...........NUSU ni statistics kubwa sana na wakati huo huo tukumbuke kuwa nusu ya watu Tanzania ni watu wa jamii ya kawaida wanaondesha shughuli za kawaida...........mbali kdg na athari zilizotajwa za kimazingira ama kishughuli.
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  huyo dr................... njaa tu inamsumbua..................... uongo......................... uongo.................. uongo......................
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Haiwezi kuwa kweli na huu utafiti ni feki kabisa tena wasingetakiwa hata kuutoa. Kama tatizo lingekuwa ni kubwa kiasi hicho lazima tungeona wakina mama wanaohitaji watoto wakibaka...watuambie walipataje hizo mbegu wakapima kama siyo walichukua za wanaume waliokuwa wagonjwa....nakataa kabisa huu utafiti ni aibu kwa walioutoa!
   
 7. m

  mtuporimtupori Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ingekuwa tatizo ni kubwa kiasi hiki tungeona hata mitaani tunakoishi. Karibu kila nyumba au familia ina mtoto. What a fake research!
   
 8. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utafiti huu haujazingatia taaluma za kitafiti.

  1) huwezi kugeneralize kuwa 50% wanatatizo kwa kuwa ina makosa mengi ya kitaalamu ikiwepo biasness, wanaume wowote wanaoenda kucheki afya zao za uzazi ni wengi wao obvious wana tatizo hilo, hivyo hawawakilishi wanaume wote wa tanzania.

  2) kama kweli sababu zilizotolewa kama visababishi vya tatizo joto, laptop use n.k basi haifai kuchukua sample toka dar kwa kuwa joto ndio nyumbani kwake na ni miongoni ya mikoa ambayo kuna matumizi makubwa ya laptop n.k

  kama kweli alikua na nia ya kufanya utafiti wa aina hii basi angechagua watu randomly toka jamii mbali mbali zenye exposure tofauti katika mikoa mbali mbali na sio wale tuu walioenda hospitali kucheki tatizo hapo ingekuwa imetulia.

  Haya ni matatizo ya madaktari wetu wasio na ujuzi wa utafiti.

  poor research design will lead to poor results which will always lead to contradiction.


  NB: Gazeti lililotoa taarifa hii ni mwananchi, na bahati mbaya huenda waandishi wetu wa mwananchi wameshazoea kutoa habari za Chadema, CCm ,JK,Slaa N.k. pia kuna uwezekano hawa waandishi wakawa hawana uwezo wa kuanda matokea ya kitafiti za afya.
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  Kwa upande wake, Dk Innocent Mosha, ambaye ni daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Muhimbili alisema, wamefanikiwa kupata takwimu hizo kutokana na wanandoa wengi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kujua sababu ya kutokuwa na watoto katika ndoa yao.
   
 10. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Kuna upotoshaji mkubwa sana katika huo utafiti.. majibu yanahusisha wale ambao walienda hospitali kwa matatizo ya infertility which is obvious kupata hiyo asilimia kwani tunategemea wagonjwa ndio wanatafuta matibabu..
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa.
  kama ni nusu basi wangekua wame mpima kila mwanaume.
  Mimi hawajanipima bado so utafiti wao sio sahihi.
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Well said mkuu.
  Nahisi haya ndo yale yale ya Redet kulipua mambo.
  Tanzania utafiti una fanyiwa ofisini na sio kutoka kuangalia ulimwengu halisi
  uko vipi....No wonder wana siasa wakiugua hawatibiwi tanzania na hawana hata mda wa
  kuwasikiliza madaktari.
   
 13. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Kuna haja ya kufanya utafiti wa kina na kuomba ushauri au kuisoma taarifa yenyewe vyema kabla ya kuitoa kwenye vyombo vya habari.

  1. Si kweli kwamba nusu ya wanaume ni wagumba. Nasema hivi kwa sababu watu waliokwenda kupima tayari walikua na tatizo, hivyo ukiwapima lazima utakuta kuna tatizo. Huwezi kwenda kupima manii kwa shida ya kuumwa jicho, bali unaenda pale baada ya kuona kuna shida kwenye issue za uzazi, hivyo basi uwezekano wa kukutwa na tatizo ni mkubwa kwa wale waliokwenda hapo. Aendeaye sipitali lazima ana shida, na ukiona zinduma ambari iko nyuma.

  2. Ili kuwa na matokeo sahihi, utafiti huu ungepaswa kupima watu toka kwenye jamii (random sampling) na siyo kwenda kupima watu wenye shida tayari. Huwezi kwenda kupima kama baharini kuna mchanga ama la? bali ukitaka kujua kama msitu una mchanga ama la hapo unaweza kupima na unaweza kujua kama kuna mchanga au hapana.

  3. Hiyo asilimia 50% kati ya watu 221 walopimwa haiwiani na idadi yote ya wanaume waliopo hapa nchini, tena walau wale ambao tayari wameshajaribu kutafuta mtoto.
   
 14. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  [SUB]Safari hii wanaume tumeshikwa pabaya[/SUB] - mbona hii ni hatari sasa
   
 15. mkuyati og

  mkuyati og JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 723
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Nadhani kuna makosa katika kuelewa tafsiri halisi ya matokeo ya utafiti huo. Tafiti haijasema kwamba nusu ya wanaume wote tz ni wagumba, imesema nusu ya wale wanaofika hospitali kupata ufumbuzi ya maswala yao ya uzazi hukutwa ni wagumba. Nadhani si swala la kushangaza sana, sababu hatutegemei wanaume ambao hawana matatizo ya uzazi kwenda hospitali kusaka msaada. Ingekuwa hii study ni randomized clinical study hapo kweli tungesema kwamba kiasi fulani matokeo yake yanawakilisha kile ambacho kipo katika jamii. None the less, ujumbe ni kwamba ugumba kwa wanaume upo, na ni significant kama ilivyo kwa wanawake so tuache kunyanyapaa wakinamama.
   
 16. sister

  sister JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,028
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  huyo mtoto ni kweli wa huyo baba?
   
 17. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi specimen wanaichukuaje?
   
 18. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  MWANANCHI liache propaganda zisizo na tija ,magazeti mmeshauza ila huu upotoshaji ipo siku utawagharimu,
  Hiyo 50% ya watanzania ni analysis yenu na wala si ya huyo Dr ,
  Kama alikuwa anataka kujua ni % ngapi ya watz imeathiriwa , si angechukua random samples za watz ?
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Khatari kubwa!!
   
 20. S

  Semanao JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  study hii ina mapungufu mengi sana. Pamoja na mapungufu yaliyotajwa, pia hatujaonyeshwa muda uliotumika na age groups. na kama walienda wanandoa comperative study ingeonyeshwa hapa. Mara nyingi study za namna hii ni kwa ajili ya kufurahisha donors wa nje ili waendelee kuomba misaaada
   
Loading...