Utafiti: Masikini wana uwezekano Mkubwa wa kutoa Rushwa kupata huduma za msingi kuliko matajiri

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Shirika la Kupinga Rushwa na Ufisadi la Transparency wa Mwaka 2013 uliohusisha kuangazia mitazamo mbalimbali ya watu kuhusu Rushwa, watu wenye hali duni ya Kiuchumi na wanakabiliwa na athari za rushwa kwenye huduma za Umma kwa kiwango kikubwa zaidi.

Utafiti huo umefafanua kuwa familia zenye kipato cha chini zina uwezekano mkubwa wa kutoa Rushwa ili kupata huduma za Msingi kuliko tajiri

Kutokana na sababu kama upatikanaji mdogo wa huduma, upendeleo au kutokujua haki zao watu wenye kipato cha chini huona kutoa rushwa ndio njia pekee ya wao kupata huduma za msingi kwa haraka

Rushwa na Ufisadi katika Utoaji na Upatikanaji wa Huduma za Kijamii zinaathari kubwa katika Ustawi na Ubora wa maisha ya Wananchi.

Rushwa katika Utoaji wa Huduma muhimu kama Elimu, Afya na Usafiri imebainika kuwa na athari hasi katika viwango vya Umaskini, Viwango vya Vifo hasa vya Mama na Mtoto, Viwango vya Watoto wanaoacha Shule huku Imani ya Wananchi kwa Serikali ikishuka kwa kasi

.....................


Corruption in service delivery is the form of corruption most frequently encountered by citizens, and can
plague all kinds of interactions with the state.


According to Transparency International’s 2013 Global Corruption Barometer, 27 per cent of respondents worldwide claimed they had experienced corruption while dealing with a public service provider.

5 This primarily affects marginalised and vulnerable groups, as wealthier, more powerful groups of society are
less reliant on state assistance.

As such, corruption undermines the “redistributionary” nature of public
services, distorts policy decisions away from the public interest and diverts available public resources into the hands of corrupt groups inside, outside and straddling
the state apparatus.

6 By undermining the quality and
quantity of public services, this type of corruption can fatally erode citizens’ confidence in public institutions7 and ultimately undermine political stability, as reflected by studies that have found a correlation between civil unrest and low-quality service supply.

As well as reducing the quantity of public resources available for redistributionary purposes, corruption undermines the quality of services. This can happen in a number of ways. Suppliers can use fraudulent or lower-grade inputs in infrastructure projects or essential
supplies (like pharmaceutical products, equipment
or textbooks) to increase their profit margin at the expense of intended beneficiaries.

Bribery and extortion at the point of delivery can render public services unaffordable for a large segment of the population, effectively depriving the poor of access to key basic services they are entitled to.9


The malignant effect corruption has on the quantity and quality of public services has profound implications
for human development outcomes and citizens’ well-being and quality of life.

Corruption in service delivery
has been shown to have negative effects on poverty rates,10 human development indicators,11 mortality
rates,12 child mortality rates,13 school drop-out rates trust in governments,15 and civil unrest.16 It has also been revealed to have devastating effects on the natural environment,17 which in some cases can lead to food and water insecurity and mismanagement of precious resources.


The world’s poor are disproportionally affected by the
impact of corruption on public services.

Research shows that low-income households are more likely to have paid bribes to access basic services than wealthier households.

18 Corruption in service delivery thus exacerbates the effects of poverty19 and may undermine the outcome of development policies.

Source: Global Corruption Barometer Report 2013
 
Iko wazi hata haihitaji utafiti.Ukienda ofisi za umma umevaa zako smart na unaonekana pesa.ipo.hakuna anaekusumbua na wanakuogopa.

Tajiri anatoa Rushwa Ili Apate kitu Cha kuingiza pesa au anunue Haki na sio Rushwa Ili ahudumiwe.
 
Sasa ni kipi kifanyike ili swala la rushwa liweze kupunguzwa kama si kutokomeza kabisa maana mnyonge mwananchi wa Hali ya chin ndiye anaye umia na siyo matajiri
 
Ukiwa na muonekano wa kitajiri, celebrity ni rahisi kupapatikiwa, sasa mimi pangu pakavu tia mchuzi, nimevaa mitarawanda, masulupwete nani wa kunipapatikia, nahitaji wepesi ndio hapo ninapoambiwa nipenyeze rupia
 
Sasa ni kipi kifanyike ili swala la rushwa liweze kupunguzwa kama si kutokomeza kabisa maana mnyonge mwananchi wa Hali ya chin ndiye anaye umia na siyo matajiri
Kitu cha kwanza ni kujielimisha kuzijua haki zetu katika sehemu tunazoenda kupata huduma. Wengi tunatumbukia kwenye mtego wa rushwa kwa sababu hatutambui haki na wajibu wetu. Pia kila mmoja anao wajibu wa kutekeleza katika mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni pamoja na kuripoti vitendo vya rushwa,kutotengeneza mazingira ya kutoa au kupewa rushwa na kuzishinikiza mamlaka kutimiza wajibu wao wa kisheria
 
Back
Top Bottom