The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Marekani utafiti umeonyesha kwamba ni vigumu sana kufanya kazi na kizazi Z ama generation Z ambao wamezaliwa kuanzia mwaka 1997.
Meneja na wakurugenzi wa wakuu wa utumishi walioulizwa kwenye utafiti wamesema ni ngumu sana kufanya kazi na kizazi Z kwani ni wabishi, wajuaji, hawana nidhamu wala heshima.
Kizazi Z hujiamini kupita kiasi, hujiona wanajua kila kitu, hutaka hata kuwafundisha wakuu wao wa kazi.
Huko China serikali inalalamika kwamba wasomi wa sasa hasa kizazi Z hawataki kazi ngumu, hawataki kazi za shamba wanataka kazi laini za online, za kuvaa suti na kula kuku kwa mrija.
Je, unakubaliana na utafiti huo?
Fox News