Utafanyaje?????

Utafanyaje?????

Vituka

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
2,268
Reaction score
1,267
We bwana Musa unatembea na Mke Wa jirani yako ila nyumba yako ina uzio na gate kuuubwa.

Hujaoa na unapata shida sana kujiiba na huyo mrembo. Ulipoanza likizo ukamchombeza uyo Mke Wa jirani yako amuage mumewe kuwa anasafiri kwenda kwa dadayake morogoro kwa wiki nzima ili aje apo kwako mle raha wiki nzima..

Kweli ukafanikisha adhma yako Mke Wa jirani kaja kwako bila kuonekana na MTU.

Siku moja ikakulazimu utoke kwako uende kigamboni na ukarudi jioni. Unaingia ndani unakuta Mke Wa jirani kalala sebuleni povu mdomoni. Unamtikisa unagundua hapumui! Ghafla unamuona nyoka mkuuuubwa anatoka karibu na mwili Wa Mke Wa jirani. Unajaribu kumuua unashindwa mana anacharuka ile mbaya! Unatoka nje kwa kiwewe unafungua gate hamadi jirani mwenye Mke kule ndani kwako anakushika na kusema vipi jirani una tatizo gani nikusaidie? Unajibaraguza anakushika mkono akikuelekeza ndani kwako, je utamueleza akusaidie kuua nyoka au!!!
 
Mmh da story iz so interesting kwakwel sintomruhusu aingie sebulen kwa aibu iyo
 
Du! Itabd nimzungushe nyuma ya nyumba ila nitamwambia ukweli kwamba kuna nyoka lakn yupo nje ila sasa yule mwanamke ndio kimbembe maana pakumzika sasa!!!!!
 
Mleta hii story hebu nambie ulifanikiwa kujua pa kumzika kabla hujaandika hii maana nimekwama hapo
 
Kila mchuma janga hula na wa kwao...... si ndiyo?
 
Duh kwani kigamboni ulikwenda kufuata nini?
 
Mtoa mada hebu tueleze vizuri unatafuta njia ya kumtoa mke wa jirani yako au kuua nyoka?
 
Back
Top Bottom