Utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafanyaje?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Icadon, May 17, 2008.

 1. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula. Basi wakaamua wapike uyoga kidogo, na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

  Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.
  Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

  Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

  Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.

  Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nami nitubu Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wako nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

  Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.

  Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza, Baba na Mama mnagombania nini humu ndani, badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nje?

  Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.

  Fikiria ni wewe ITAKUWAJE?
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni nzuri kwa weekend hii
   
 3. Kesa

  Kesa Member

  #3
  Jun 2, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vunja mbavu poa
   
  Last edited: Jun 2, 2008
 4. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  its not only a good joke , inatufundisha kuto kukurupuka na kubwabwaja hovyo bila kujuwa ukweli

  Thanks Icadon
   
 5. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2008
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mi sijui hata ningefanyaje..

  ila ungeniluliza before that ningesema kuwa yatupasa kutokukurupuka for Death, kwanza makosa si baina ya mtu na mtu ila ni wewe na Mungu wako.

  But its real Good.
   
 6. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #6
  Jun 4, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Moral of the Story:...Dont trust your woman for nothing and vice versa...LOL!!!...Icadon umenichekesha kweli hapo!
   
 7. k

  kalld Member

  #7
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kikubwa hapo ni kuwa waaminifu !duh inafurahisha na kuhuzunisha pamoja weeekend njema!
   
 8. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  dawa ni kusameheana!
   
 9. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dawa ni kusameheana na kuanza tena ufisadi wa ngono ...... lol
   
Loading...