Bull Bucka
Member
- Oct 5, 2023
- 34
- 46
Wananchi wanne wa Kijiji cha Ugwachanya Kilichopo Kata ya Mseke Mkoani Iringa wamekutwa wakimchuna Mbwa kwa ajili ya maandalizi ya nyama.
Akizungumzia kuhusu Mkasa huo Mmiliki wa Mbwa huyo Bi. Veronica amesema kuwa alipata taarifa ya Mbwa wake kupotea ambapo alifanya jitihada za kumtafuta na kuwakuta watuhumiwa wanne ambao ni Nicholaus lunyungu, Kalista Mhenzi, Jane kihaga na Charles Kihaga wakiwa wanamchuna Mbwa wake.
Amesema kuwa aliwakuta watu hao wakimchuna Mbwa huyo huku wakimwita mmiliki huyo kwa ajili yakuzungumza faragha jambo ambalo alilipinga na kuwaita majirani kwani tukio la kupotea mbwa mtaani hapo limekuwa likijirudia.
Kwa upande wao wao wanaotuhumiwa kumchuna mbwa huyo wamesema kuwa walimkuta mwenzao Kalista Mhenzi akimchuna Mbwa mara baada ya kusikia vishindo ndani kwake.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Igavilo Kijiji cha Ugwachanya Bi Ester Mkini amekiri kuwepo kwa tukio la Mbwa kuchunwa kwa ajili ya nyama ambapo watuhumiwa hao wanaitumia kwa ajili ya kula wao wenyewe.
Aidha amewaonya wananchi wa eneo lake kuacha tabia hiyo kwani haikubaliki huku watuhumiwa wa tukio hilo wakishurutishwa kununua mbwa mwingine na kumkabidhi mmiliki wake.
Chanzo: NURU FM, Iringa