haya mambo ya utabiri wala sio kitu kigeni katika hii dunia, inategemea na imani yako tu na kwa jinsi gani unavyoyachukulia haya mambo,
haya mambo yanakuwa na maelezo au majina tofauti kulingana na imani au upeo wa wahusika, ningependa nizungumzie mifano ambayo tunaipata kwenye biblia
1. joseph (yusufu), baada ya kutiwa gerezani, alifanikiwa kutoka na kuwa mtu mkubwa sana baada ya kutafsiri ndoto kwa kumweleza pharaoh kuwa kutakuwa na miaka ya neema na miaka ya balaa, sasa watu wa dini watatuambiwa ni mipango ya Mungu, vipi shehe Yahaya asiwe mpango wa Mungu, kutafsiri ndoto kwamba mambo fulani yatatokea huo sio utabiri
2. wakati wa Yesu kuzaliwa, wataalamu wa nyota (kama shehe Yahaya) kutoka far east (labda India au China)Mamajusi, katika kutazama mambo yao ya nyota wakaona kuna mtoto kazaliwa Yelusalem ambaye atakuwa mtu mkubwa sana, hivyo wakaamua kuja Yelusalemu kuja kutoa zawadi zao wakiongozwa na hayo mambo yao ya nyota, na moja kwa moja Herode akajua ujio wa watu hao maarufu na Herodi akawaambia wakimwona waje wamweleze, lakini Biblia inatuambia Malaika wa Mungu, akawatokea na kuwaambia wasirudi kwa Herode, swali ni kuwa hawa jamaa ni watabiri kama shehe Yahaya tu, na waliuona mipango ya Mungu kwa kutabiri ujio wa mtu asiye wa kawaida na still Mungu akawa upande wao,
kwa hiyo bac kwa mtazamo wangu, shehe Yahaya anaweza kuwa mtabiri wa kweli lakini kwenye kiwango chake, yaani anaweza kutabiri kutakuwa na vifo mwezi wa sita na hapo ndio ukawa ni mwisho wake yaani hawezi kusema ni nani na tarehe hipi lakini wapo wengine wenye uwezo huo, Kwa wenye imani
tafakuli zangu tu