Utabiri wa Leo Tanesco!

Utabiri wa Leo Tanesco!

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
772
Habari za saa hizi Mabibi na Mabwana.
Ufuatao ni utabiri wa hali ya Umeme kwa siku ya leo!
Pepo za umeme zitavuma taratibu kutoka upande wa kusini mwa Dar es Salaam kuelekea upande wa Kaskazini, hivyo kutakuwa na umeme mchache maeneo yote ya Jiji na ngurumo nyingi za Jenereta pande za Kivukoni, Kariakoo, Pugu road, Mwenge, Posta na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Na kwa wakati wa usiku watu wa Mbagala, Kigamboni, Kimara, Mtoni na maeneo yote ya jirani wilaya ya Temeke na Kinondoni kutakuwa na Kiza kisichojulikana mwisho wake ........ Maeneo ya Sinza, Mbezi na Tegeta kutakuwa na miunguromo ya jenereta hapa na pale nyakati za usiku , hii ni kutokana na familia chache zinazotumia jenereta nyakati za usiku
Ni kutoka mamlaka ya utabiri wa nguvu za umeme Ubungo Tanesco ghorofa ya Pili ....... Nawatakia siku njema. Ahsanten.:biggrin1::A S 103::biggrin1:
 
ingekuwavipi ngeleja aongozane na rostam aziz, tena wakapumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom