dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,125
- 49,384
Kwa muda sasa kumekuwa na madai kwamba utabiri wa hali ya hewa nchi hii ni feki. Kufuatia madai hayo, niliamua mwenyewe msimu huu kufuatilia kwa karibu ili niweze kuthibitisha.
Katikati ya Septemba 2018 haoooo wakaibuka. Wakatabiri kwamba mvua za vuli zingeanza mwishoni mwa mwezi huo au mapema Oktoba na zingenyesha juu ya wastani kwa maeneo mengi nchini. Leo ni Oktoba 16 na wakulima wengi tulishaandaa mashamba na kupanda zaidi ya wiki mbili zilizopita tukisubiria "utabiri" kutimia lakini HOLAAA! Imekula kwetu; hasara juu ya hasara.
Utabiri nchi hii ni kizungumkuti. Inawezekana zikanyesha pengine hata juu ya wastani kama walivyotabiri na kama ambavyo imeanza huko Uganda lakini timing yao imekuwa ya hovyo kabisa. Nawashauri wakulima watumie njia za asili za utabiri wa majira badala ya kutegemea mamlaka hii labda kwa mawio na machweo tu.
=== UPDATES - 01.11.2018 ===
Baada ya mwanzoni mwa Septemba 2018 kutabiri kwamba mwishoni mwa mwezi huo zingenyesha mvua za "hatari" ambazo zingeleta maafa sehemu kubwa ya nchi; utabiri ambao haukutimia, Hali ya Hewa waliibuka na tabiri kadhaa kurekebisha ule wa awali na kuwashauri wakulima kuandaa mashamba ili kutumia "vizuri" mvua tarajiwa. Hata hivyo, hakuna utabiri uliotimia.
Pengine kwa kugundua tabiri zao za awali hazikutimia, Oktoba 18, DG mwenyewe aliitangazia dunia kwamba Oktoba 20 ndio ingekuwa siku yenyewe na "akatabiri" sehemu kubwa ya nchi zingemwagika mvua kubwa sana. Wakulima walishauriwa kuanza kupanda mbegu kwani muda ulikuwa "umekwisha". Leo ni Novemba 01, 2018 hizo mvua hazioneshi hata dalili kwamba zitanyesha badala yake ni jua kali kila kona ya nchi. Naendelea kuwashauri wakulima kutumia njia za asili za utabiri wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa ni muhimu wakajitafakari kwani tabiri zao zinakosa uhakika japo kwa 10%.