pipi mti
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 764
- 515
Wakuu habari.
Leo katika pita pita zangu huko you tube nimekutana na video inayomuonesha Askofu Gwajima akitoa utabiri/prophecy kuhusu mwaka 2018 katika kanisa lake.Na kati ya vitu alivyozungumza ni pamoja na;
-Mwaka 2017 alitabiri utakuwa mwaka wa mabonde na milima(ups and down) na ikatokea ivyo.
-Mwaka huu 2018 anasema utakua hauna milima yani mambo yatakua safi mwaka mzima na kila mtu atafanikiwa katika mambo yake na taifa kwa ujumla.
Hapo ndio napata doubt na prophecy zake kama ni za kweli au anacheza na akili na psychology za watu, maana ukianza suala la kusema umetabiri kwamba watu watapitia ups and down katika kipindi cha mwaka hili ni suala la lazima maana haiwezi ikatokea nchi nzima kuneemeka mwaka mzima bila kupitia changamoto yoyote na haiwezekani ndani ya mwaka mzima watu wote nchini wakapitia magumu bila kupata hata siku moja ya mambo mazuri.
Pia kutabiri kwamba mwaka huu mambo yatakuwa mazuri tu katika taifa letu na si ups and down yaani kuanzia ngazi ya taifa hadi mtu mmoja mmoja ni suala ambalo haliwezekani..wapo watakaofanikiwa na wapo watakaoshindwa kufikia malengo yao ndani ya mwaka, na hiyo ndio nature ya ulimwengu. Kwa mfano Ukisema kila mtu atafanikiwa katika malengo yake it means kwa vijana wote ambao hawana ajira watapata Ajira mwaka 2018 ambapo ni suala ambalo ni unattainable.
Huenda Mimi ndio sijaelewa kitu Fulani.Naomba Mwenye uelewa na haya mambo afunguke.