Utabiri wa anguko la wabunge wa chadema 2015

Utabiri wa anguko la wabunge wa chadema 2015

Mh. Sheikh, Nabii, Mtabiri au Mpiga Ramli, Kaka bwegebwege.
Naomba nikujibu au nikueleze yafuatayo:
Kuna chama kimoja tu huongoza kwenda Milingotini B'moyo kuupata oungozi. Ni Maccm. Vyama vingine vikilogwa vikaenda huko, viongozi wake watapewa ndumba fake.
Hivyo, tabiria Maccm siyo CDM. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:
Chama mbadala cha upinzani kamwe hakiwezi kuendelea kwa kungojea kudra ya chama Tawala. Ati tungojee neema ya chama tawala kututeulia wabunge wa kuteuliwa. No No Nooo.
Tumeshaanza kusikia minong'ono kuwa Mkuu wa kaya amchague M/Kiti fulani wa chama fulani ati ni Economist aliye bobea kwa mambo hayo. Hiyo ni kudra ya m/kiti huyo kusikia amkubali kama huko kwenye hilo lichama mfu lake hakuna wana uchumi waliobakia baada ya mwenzetu kututangulia kwenye haki.
1. Umesema at Mh. Mnyika hana mvuto tena Ubungo. Najiuliza, kachuja sura au? Tumpake wanja au? Kama ni maendeleo, tumemsikia alivyo tetea jimbo lake la Ubungo, kwenye barabara, madaraja na hata maji. Ulitaka afanyeje chini ya ugandamizi uliopo? Nakuambia, CCM kuleni hiyo pesa wala msipoteze muda wa kuigombea Ubungo. Msithubutu.
2. Arusha na Mh. G Lema. Unamwita Controversial leader. Ati anapenda vurugu. Vurugu hizo alizianzisha mwenyewe au? Hivi kweli waweza kuchukua bomu na kujilipua mwenyewe mahali unajua watu wote hapo ni mashabiki wako? Mbona ninyi watu mna mawazo potofu hivi?
3. Mh. Msigwa, Ati kaongea sana bungeni lakini anajichanganya mwenyewe kwenye mambo ya chama. Alichoongea bungeni ni kipi au ni kwa vile alivyo yataja Majangili yenu kwa majina? Hivi nikuulize zile siku 7 alizopewa na kiongozi mmoja wa ccm hazijaisha? Mbona hatuoni action? Au ni kwa vile yule jamaa mwingine alishikwa tena Dar na Tusker? Shame on yu.
4. Mh. Halima Mdee. Ati unasema kakaa kimya. Hivi katika wabunge wanawake wa ccm na cuf ni wangapi waliotoa michango bungeni wa kuweza kuwalinganisha na Mdee? Kweli mapenzi ni maradhi ya upofu. Ndo maana m/kiti wako kamteua huyo wa upinzani ili naye ajidunduiziye kidogo kidogo apate tena nguvu ya kuja kupambana na Mdee. Hao wengine woote wa ccm hawana cha kujitetea kwa jimbo hilo kwani Maisha ya Mtanzania sasa hivi ni mzigo. Yote haya yameletwa na hilo lichama mfu.
5. Unamdharau Mh. Tundu Lisu kuitwa Muongo hadharani akamnyamazia Rais. Hivi kweli unamwona Lisu hana akili? Angemjibu pale, ni nani angeaibika? People say; Never, Never argue with a F.o.o.l Tundu bwana ana akili za ziada. Hapo nampa Hekoooo.
Wapambe wakamwambia Rais, Lisu hana breki. Mtapishe kidogo atatoa nyongo. Waapi. Lisu akamthitishia Rais wake kuwa sivyo alivyo. Hekima ikamuumbua mshambuliaji wake Lisu. B/up Lisu

haya ni mawazo yangu tu. Nawasilisha

Mpashe mpashe huyu ----- mtozeni.
Inaonekana hata hajui anachozungumza kuhusu Wabunge wa CDM kudhihirisha ubwege wake.
 
Mpashe mpashe huyu ----- mtozeni.
Inaonekana hata hajui anachozungumza kuhusu Wabunge wa CDM kudhihirisha ubwege wake.

Kazi yetu ni moja tu hatutaacha kuwafungua macho hawa maccm. Wanabaki kusema tumeleta maendeleo mbona hatuoneshwi kile paleeee. Kuzaa sio kazi, kazi kulea kileleeke.
Miaka 50 mapinduzi Zanziba bado watu wana meli 1 ya mizigo na watu kwenda Pemba. Mtu anafuga ndevu badala ya kufuga mbwa akajipatia hata jina. Kule Darisalalma kuna mtaa unaitwa; ..Kwa mfuga Mbwa. CCM kweli majangaaaa
 
Nakubali utabiri kwa hao waheshimiwa
Kwani mi natokea kati hayo majimbo kweli wameacha kutetea maslahi ya wapiga kura na kuanza kutafuta umaarufu kwa kupinga hâta mambo ya maendeleo.
 
Kwa hiyo wabunge hawatacahguliwa kwasababu hawatekelezi ahadi zao kwa wananchi au kwa kwa kuto mtetea zito kwa makosa yake. Du Tanzania kuendelea kazi sidhani kama kuna viongozi wanaweza kuiendeleza Tanzania hii kama unaowaongoza wana fikra hizi
 
Nimekuwa nikitafakari mwenendo wa baadhi ya viongozi wa CDM na haya matukio yaliyotokea recently kwenye chama hiki ambacho wengi tulikuwa tunakiona ni chama mbadala! Migogoro iliyopo sasa, na Zaidi, kubwa ni suala la kukosekana kwa demokrasia ndani ya CDM na ongezeko la vibaraka wasio na ushawishi wala weledi wa masuala uchumi, maendeleo, siasa za ndani na za kimataifa kutasababisha CDM iporomoke Zaidi na ikose mvuto mbele ya wapiga kura!

Si hayo tu, wakati tunajiaandaa na uchaguzi mkuu mwakani, ni dhahiri CDM haitakuwa na nafasi ya kutosha kurekebisha hali ya mambo ndani ya chama na kupata nafasi ya kuunda timu ya ushindi 2015! Tukutane baada ya uchaguzi 2015, lakini kwa sasa naona wabunge wafuatao watapoteza viti vyao:-


2. Godbless Lema – controversial politician, anapenda vurugu ambazo zimesababisha wafuasi na wanachama wengi wa CDM na wananchi wa kawaida kupoteza maisha au kupata vilema vya kudumu kutokana na ushauri na ushawishi wake wa kutumia maandamano na ghasia dhidi ya vyombo vya dola…watanzania wameshtuka, Arush ahawatamuunga mkono


Tusubiri tuone
Bomu lilorushwa usiku tarehe moja na kusababisha vilema kwa wananchi wa arusha, chanzo ni lema? Mungu ni mwema, anaendelea kuwaumbua siku baada ya siku.
 
Back
Top Bottom