Gwele
JF-Expert Member
- Jun 7, 2016
- 2,296
- 2,854
Kulingana na ubora walio uonyesha klabu ya simba katika mechi hizi 3 za hatua ya makundi ya Caf confederation cup ni wazi vigogo hawa wa soka la afrika huenda wakaenda kutwaa taji hilo kubwa afrika msimu huu 2021/2022
Simba imeonekana kuwa bora sana kwenye mechi 3 hizi za mwanzo ambapo imekuwa timu pekee katika kundi D kupata walau point ugenini na hii inatoa ishara kubwa kuwa huenda simba akamaliza kundi hili akiwa kileleni na kutinga hatua ya robo fainali
Kwa namna nilivyoziangalia timu shiriki za michuano hii ni wazi simba ana nafasi kubwa si ya kupita tu hatua ya robo fainali bali hata nusu fainal hali itakayopelekea kuingia fainali ya michuano hii na kubeba taji hilo kwa mara yao ya kwanza.
Simba kiuchezaji ina imarika kila siku benchi la ufundi linafanya kazi kubwa sana hivyo mpira watakaoucheza robo na nusu fainali utawashtua watanzania wengi hasa waliodhani labda simba imeshuka makali yake.
Tuendelee kusubiri muda lakini kwa zaidi ya 90% simba anaenda fainali ya hii michuano na kwa 60% atabeba hii ndoo kwa mara ya kwanza na kusimika rasmi ubabe barani afrika huku tukilielekea kombe la klabu bingwa barani afrika msimu unaofuata